Mkuu wa nchi na ukimya kuhusu mawaziri

Comi

JF-Expert Member
Oct 2, 2011
3,329
1,500
Sasa ni takribani wiki moja na siku toka mawaziri watatu kusimamishwa na mmoja kujiuzulu kutokana na ripoti ya tokomeza majangili. Katika mawaziri hao kuna ambao wananchi walishawatilia shaka katika utendaji wao wa kuwahudumia wananchi. Kuna mawaziri wengine ambao kwa namna moja au nyingine shutma na hata viongozi waandamizi katika chama chao wamewatolea uvivu na kuwaambia kuwa ni mizigo na hiyo ni kabla ya rais kutengua uwaziri wa hao mawaziri wanne.

Swali langu ni kwamba, je! Rais hadi mda huu hana mawaziri wengine ambao tayari alishawafikiria? Au bado yuko mapumzikoni kama mwenzake Pinda aliyesema hawezi kuongea kwa mda huu. Au hajaona mbunge yeyote anayekidhi vigezo vya uwaziri?

Naomba kujuzwa kwa nini hakuna taarifa yoyote kuhusu swala la mawaziri.
 
tatanyengo

JF-Expert Member
Mar 30, 2011
1,134
1,195
Uteuzi wa viongozi unahitaji umakini na pia kushirikisha vyombo na watu wengine. Kazi hiyo itafanyika baada ya sikukuu za mwisho wa mwaka.
 
ilboru1995

JF-Expert Member
Oct 4, 2007
2,329
0

Wengi wetu humu hawaelewi kuwa urais ni taasisi na kwamba kazi ya kuwapata mawaziri unataratibu zake zinazoangalia uwakilishi mpana wa nchi mbali na elimu, ujuzi na uwezo wa kutunza siri za serikali iliyoko madarakani...siku hizi uzalendo si lazima japo yaweza kuchukuliwa kama kigezo pia...
 
katika hayo yote uliyotaja ni waziri gani ambaye anatumia elimu yake, ujuzi na mengineyo? Kama ingekuwa hivyo tungekuwa na mawaziri mzigo? Embu fafanua au tupe mfano halisi wa mawaziri ambao wametimiza hivyo vigezo vyako.
 
sikajiji

JF-Expert Member
Jan 23, 2012
586
195
Sasa ni takribani wiki moja na siku toka mawaziri watatu kusimamishwa na mmoja kujiuzulu kutokana na ripoti ya tokomeza majangili. Katika mawaziri hao kuna ambao wananchi walishawatilia shaka katika utendaji wao wa kuwahudumia wananchi. Kuna mawaziri wengine ambao kwa namna moja au nyingine shutma na hata viongozi waandamizi katika chama chao wamewatolea uvivu na kuwaambia kuwa ni mizigo na hiyo ni kabla ya rais kutengua uwaziri wa hao mawaziri wanne.

Swali langu ni kwamba, je! Rais hadi mda huu hana mawaziri wengine ambao tayari alishawafikiria? Au bado yuko mapumzikoni kama mwenzake Pinda aliyesema hawezi kuongea kwa mda huu. Au hajaona mbunge yeyote anayekidhi vigezo vya uwaziri?

Naomba kujuzwa kwa nini hakuna taarifa yoyote kuhusu swala la mawaziri.

kidamva

JF-Expert Member
Dec 3, 2013
2,584
2,000
Ni mapema mno kwa rais kuongea kitu kwa sasa. Tumsubiri keenye mkesha wa mwaka mpya.
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
105,520
2,000
Huyo ndio DHAIFU banaaa anaongoza nchi kimanatimanati.
 
ilboru1995

JF-Expert Member
Oct 4, 2007
2,329
0
katika hayo yote uliyotaja ni waziri gani ambaye anatumia elimu yake, ujuzi na mengineyo? Kama ingekuwa hivyo tungekuwa na mawaziri mzigo? Embu fafanua au tupe mfano halisi wa mawaziri ambao wametimiza hivyo vigezo vyako.

Mkuu vigezo vya Elimu, Ujuzi, Afya, Uwakilishi ni vya msingi ila kwa wenzetu huwa wanaenda mbali zaidi kuwafanyia screening kabla ya kuwapa madaraka! Ukiangalia kwa makini zaidi utagundua kuwa Uchapakazi na Uzalendo siku hizi zimewekwa kando! badala yake mtandao ndo wenye nguvu zaidi...
 
Mag3

JF-Expert Member
May 31, 2008
11,673

Je huyo anayewateua anakidhi vigezo hivyo? Ukipanda mbaazi huwezi kuvuna korosho!
 
  • Thanks
Reactions: BAK

Bijou

JF-Expert Member
Feb 25, 2011
1,192
1,500
Sasa ni takribani wiki moja na siku toka mawaziri watatu kusimamishwa na mmoja kujiuzulu kutokana na ripoti ya tokomeza majangili. Katika mawaziri hao kuna ambao wananchi walishawatilia shaka katika utendaji wao wa kuwahudumia wananchi. Kuna mawaziri wengine ambao kwa namna moja au nyingine shutma na hata viongozi waandamizi katika chama chao wamewatolea uvivu na kuwaambia kuwa ni mizigo na hiyo ni kabla ya rais kutengua uwaziri wa hao mawaziri wanne.

Swali langu ni kwamba, je! Rais hadi mda huu hana mawaziri wengine ambao tayari alishawafikiria? Au bado yuko mapumzikoni kama mwenzake Pinda aliyesema hawezi kuongea kwa mda huu. Au hajaona mbunge yeyote anayekidhi vigezo vya uwaziri?

Naomba kujuzwa kwa nini hakuna taarifa yoyote kuhusu swala la mawaziri.

Acha wale mwaka mpya kwanza
 
ilboru1995

JF-Expert Member
Oct 4, 2007
2,329
0
Je huyo anayewateua anakidhi vigezo hivyo? Ukipanda mbaazi huwezi kuvuna korosho!
Mkuu Mag3 ndo maana tunasema urais ni taasisi iliyokamilika... Inaonekana mamlaka ya uteuzi haijakaa vizuri na hapa Mkuchika na RO wanatakiwa wawajibike/wawajibishwe kwa kuteua watu kama akina Mulugo, Chawene, Muhongo, Magufuli, Kombani et al...
 
mcmalck

Senior Member
May 25, 2012
134
195
Wengi wetu humu hawaelewi kuwa urais ni taasisi na kwamba kazi ya kuwapata mawaziri unataratibu zake zinazoangalia uwakilishi mpana wa nchi mbali na elimu, ujuzi na uwezo wa kutunza siri za serikali iliyoko madarakani...siku hizi uzalendo si lazima japo yaweza kuchukuliwa kama kigezo pia...

Ivi ni dhambi kwani waziri kutoka chama cha upinzan katka siasa naomba nijuzwe hili mkuu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom