Baba Munah
Member
- Feb 7, 2017
- 19
- 49
Mkuu wa mkoa wa Tanga Martin Shigella ametangaza rasmi vita dhidi ya dawa za kulevya kwa kuwataka wenyeji wa maeneo ya mpakani kushirikiana na serikali kwa kutoa taarifa ya kuwafichua na uhalifu huo.
Kauli hiyo ameitoa wakati akizindua zoezi la uandikishaji wa wa wahamiaji walowezi mkoani hapa. Amesema viongozi wa vijiji watakaobainika kushirikiana na wauzaji wa dawa za kulevya hususan mirungi ambayo inatoka nchi jirani watashughulikiwa.
Aidha shigella amewaasa wananchi kuacha uvuvi haramu pamoja na biashara za magendo na kubainisha kuwa serikali ya mko imeunda kikosi maalum ambacho kitashugulikia wanajihusisha na uhalifu huo.
Mkoa wa Ruvuma umeingia makubaliano ya ushirikiano wa kibiashara na uchumi kati ya wilaya tatu za nchini Malawi Chitipa,Nkatabei na Kalonga zinazopakana na mikoa ya Ruvuma na Mbeya nchini Tanzania makubaliano ambayo yatawapa fursa wafanyabiashara wa nchini Malawi kutumia bandari ya Mtwara kupitia Ruvuma na kuvuka ziwa Nyasa badala ya kutumia bandari ya Beila ya nchini Msumbiji.Geofrey Nilahi anataarifa Zaidi.
Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake katibu tawala wa mkoa wa Ruvuma Hasan Bendeyeko amesema kuwa hivi karibuni timu ya viongozi wa mkoa wa Ruvuma pamoja na viongozi wa wizara ya mambo ya nje walikuwa na kikao cha pamoja cha ushirikiano wa kudumu kuimarisha mahusiano ya kibiashara kati ya Tanzania na Malawi wafanyabiashara waangalie namna wanavyoweza kuitumia fulsa hiyo kwa maendeleo yao na taifa.
Naye afisa biashara mkoa wa Ruvuma Nehemia James amesema kuwa kufunguka kwa barabara ya Mtwara Cordal Malawi itakuwa ni sehemu ya soko la bidhaa za Tanzania.