Dar: Kilogramu 614.12 za dawa za kulevya zateketezwa katika kiwanda cha saruji cha Twiga

Pfizer

JF-Expert Member
Mar 25, 2021
587
800
Kilogramu 614.12 za Dawa za Kulevya Zateketezwa Dar es Salaam

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya leo imeteketeza kilogramu 614.12 za dawa za kulevya katika kiwanda cha saruji cha Twiga, kilichopo Wazo, Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari katika tukio hilo, Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Aretas Lyimo alisema kuwa, kati ya dawa zilizoteketezwa, kilogramu 601.87 ni methamphetamine na kilogramu 12.25 ni heroin ambapo dawa hizo zilikuwa zinashikiliwa kama vielelezo, na mahakama za Hakimu Mkazi Kibaha na Kisutu ziliamuru uteketezaji wake kutokana na hatari ya kuharibika au kubadilika umbo wakati kesi husika bado zinaendelea.

"Uteketezaji wa dawa hizi unafanyika kwa mujibu wa Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Namba 5 ya mwaka 2015 pamoja na kanuni zake. Sheria hii inaruhusu uteketezaji wa dawa hizi kufanyika kabla, wakati, au baada ya shauri kumalizika mahakamani," alieleza Kamishna Lyimo.

Kamishna alifafanua kuwa uteketezaji huo unafanywa kwa njia zinazozingatia usalama wa afya ya watu na utunzaji wa mazingira, huku ukisimamiwa na wadau mbalimbali waliotajwa kisheria.

Aidha, Kamishna Lyimo alibainisha kuwa katika mwezi huu wa Desemba pekee, mamlaka imefanikiwa kuteketeza ekari 12 za mashamba ya bangi katika mkoa wa Tabora, pamoja na kilogramu 398.105 za dawa mbalimbali mkoani Mtwara. Pia, mamlaka inatarajia kuteketeza kilo 126.21 za mirungi mkoani Arusha katika siku chache zijazo.

Kamishna aliwapongeza wadau wote waliofanikisha uteketezaji wa dawa hizo na kuendelea kushirikiana na mamlaka katika juhudi za kupambana na biashara haramu ya dawa za kulevya. Alihitimisha kwa kusema kuwa zoezi la uteketezaji litaendelea nchi nzima, kadri mahakama zitakavyoendelea kutoa amri.

"Tunaendelea kushirikiana na wadau kuhakikisha kuwa dawa hizi haramu zinadhibitiwa kwa ustawi wa jamii yetu," aliongeza.
IMG-20241219-WA0053.jpg
IMG-20241219-WA0051.jpg
IMG-20241219-WA0049.jpg
IMG-20241219-WA0041.jpg
IMG-20241219-WA0039.jpg
IMG-20241219-WA0037.jpg
IMG-20241219-WA0034.jpg
IMG-20241219-WA0032.jpg
 
Ni illigeal , watoto wanuniliwe madawati in expense ya uraibu wa vijana wazidi kuharibikiwa?
Think deep
Wewe ndio you are not thinking deep.
Huoni watu wengine wameingia taharuki walioosikia kuna mtu anataka kuteketeza dawa?
Dawa usitoke kuzitafuta.
Lakini ukizipata zitaifishe.
Utamuharibu nani?
Zile dawa utaziuza mahali ambapo wanalipa vizuri.
We,go take a walk in the ghetto and tell me what you think.
 
Hizo kilo 126.21 za mirungi wanazotaka kuzichoma wangeziuza pale Kenya wangeingiza sh ngapi?

Isingetosha kujenga hata vyoo vinne vya kisasa shule za msingi?
 
Wewe ndio you are not thinking deep.
Huoni watu wengine wameingia taharuki walioosikia kuna mtu anataka kuteketeza dawa?
Dawa usitoke kuzitafuta.
Lakini ukizipata zitaifishe.
Utamuharibu nani?
Zile dawa utaziuza mahali ambapo wanalipa vizuri.
We,go take a walk in the ghetto and tell me what you think.
Umesoma kichwa cha habari? Ni dawa za kulevya, you know ni very illegal?
Hizo ni dawa za kulevya man? Hata kama zingeuzwa the cycle ingebaki pale pale , waathirike wengine ili wengine wapate faida? Come on man

Uzitaifishe for what? Unakaa nazo ili iweje?

Yaani serikal izikamate, iwafunge watuhumiwa. Wazi store, halaf waziuze tena!

Are you serious?
 
Sasa kama kuna Nchi Sheria zao zinaruhusu watu wake kutumia madawa , kwanini tusiwauzie wanaoona sahihi kutumia?
 
Kilogramu 614.12 za Dawa za Kulevya Zateketezwa Dar es Salaam

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya leo imeteketeza kilogramu 614.12 za dawa za kulevya katika kiwanda cha saruji cha Twiga, kilichopo Wazo, Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari katika tukio hilo, Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Aretas Lyimo alisema kuwa, kati ya dawa zilizoteketezwa, kilogramu 601.87 ni methamphetamine na kilogramu 12.25 ni heroin ambapo dawa hizo zilikuwa zinashikiliwa kama vielelezo, na mahakama za Hakimu Mkazi Kibaha na Kisutu ziliamuru uteketezaji wake kutokana na hatari ya kuharibika au kubadilika umbo wakati kesi husika bado zinaendelea.

"Uteketezaji wa dawa hizi unafanyika kwa mujibu wa Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Namba 5 ya mwaka 2015 pamoja na kanuni zake. Sheria hii inaruhusu uteketezaji wa dawa hizi kufanyika kabla, wakati, au baada ya shauri kumalizika mahakamani," alieleza Kamishna Lyimo.

Kamishna alifafanua kuwa uteketezaji huo unafanywa kwa njia zinazozingatia usalama wa afya ya watu na utunzaji wa mazingira, huku ukisimamiwa na wadau mbalimbali waliotajwa kisheria.

Aidha, Kamishna Lyimo alibainisha kuwa katika mwezi huu wa Desemba pekee, mamlaka imefanikiwa kuteketeza ekari 12 za mashamba ya bangi katika mkoa wa Tabora, pamoja na kilogramu 398.105 za dawa mbalimbali mkoani Mtwara. Pia, mamlaka inatarajia kuteketeza kilo 126.21 za mirungi mkoani Arusha katika siku chache zijazo.

Kamishna aliwapongeza wadau wote waliofanikisha uteketezaji wa dawa hizo na kuendelea kushirikiana na mamlaka katika juhudi za kupambana na biashara haramu ya dawa za kulevya. Alihitimisha kwa kusema kuwa zoezi la uteketezaji litaendelea nchi nzima, kadri mahakama zitakavyoendelea kutoa amri.

"Tunaendelea kushirikiana na wadau kuhakikisha kuwa dawa hizi haramu zinadhibitiwa kwa ustawi wa jamii yetu," aliongeza.
View attachment 3179997View attachment 3179998View attachment 3179999View attachment 3180000View attachment 3180001View attachment 3180002View attachment 3180003View attachment 3180004
Ndio maana leo nilikua nimedata sana kimbe chanzo kupita pale wazo
 
Back
Top Bottom