Mkuu wa Mkoa wa Arusha Azomewa na Wananchi Karatu

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Azomewa na Wananchi Karatu

Mtu unapoamua kubumba habari unapaswa uwe na uelewa wa mambo mengi hususani jiografìa, la sivyo utaonekana bwege na kuumbuka kiurahisi.

Karatu ni wilaya ambayo sasa hivi iko kwenye mkoa mpya wa Manyara. Zamani mkoa wa Arusha ulijumulisha maeneo hayo. Sasa hivi mkoa wa Arusha unaishia Monduli tu. Sasa Mkuu wa mkoa wa Arusha ataenda Manyara kama nani huko? Yaani mtu uandike kwa mfano Makonda amekwenda kufanya vitu vyake Kibaha, ukiaminisha watu kuwa mkoa wa Dar unafika hadi Kbaha? Uzi huu unapaswa kuwa deleted na aliyeuleta kuchukuliwa hatua kwa kanuni za Jf.
Karatu ipo mkoa wa Arusha ndiyo maana Gambo alikuwa huko.

Umeandika mambo mengi lakini umeandika ujinga mtupu.

JF haiishi vituko.
 
Aliyezomewa ni mbunge wa chadema muache upotoshaji

@MwanahabariHuru
 
Chagadema mmeishiwa hoja....yani sijui Bavichaa mnalipwa shilingi ngapi kwa huu utumbo wenu
 
Mkuu wa mkoa wa Arusha ndg Mrisho Gambo amekutana na hasira ya wananchi katika wilaya ya Karatu.Gambo amezomewa na kuachwa pekee yake mkutanoni kufuatia yeye Gambo kupuuza agizo rasmi la waziri mkuu ambaye aliagiza Pampu za matajiri wachache kuondolewa kwenye vyanzo vya maji,baadhi ya watu wakatoa mashine zao kwa hiari na wale wengine waliokaidi agizo hilo mashine zao zilitolewa kwa Nguvu na mkuu wa Wilaya kutumia jeshi la police na mashine zote zikawa zimetolewa kwenye chanzo

Na baada wiki mbili toka waziri mkuu aondoke wakajitokeza watu wengine na kurudisha mashine zao kwenye chanzo na baada ya wananchi kuona kuwa kuna kundi ambalo limekaidi agizo la waziri mkuu wakaamua kupiga mwano yaani wakapiga YOWE na wakaamua kwenda kutoa mashine zote zilizorudishwa na pia mashine hizo zote zilichomwa moto na wananchi wenye hasira kali hiyo ilikuwa jana tar 27/12/16.

Hivyo baada tukio la jana Mhe Mkuu wa Mkoa wa Arusha ndg Mrisho Gambo akaamua kuja Karatu bonde la Eyasi na wanachi wakaalikwa na wananchi walijitokeza kwa wingi sana

Mkuu wa Mkoa akaja asubuhi ya leo akifuatana na kamati ya ulinzi na usalama mkoa na wakaenda kukagua mashine zote zilizochomwa na wanachi jana lakini ikumbukwe kuwa hata leo asubuhi wananchi waliendelea kuchoma mashine zote zilizowekwa kwenye chanzo,,,


Na mkuu wa Mkoa akaanza kuhutubia akaanza Eyasi hoyeee wananchi kimya,,,,karatu hoyeeeee kimya na baada ya hapo akasema naona ni kama hamnielewi naombeni basi niwakaribishe madiwani wa kata hizi yaani kata ya Baray na Mang'ola aliuliza wapo? Wananchi wakajibu wapo basi akakaribishwa mhe Thomas Darabe diwani kata ya Baray ambaye pia ni mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya hivyo akaeleza jinsi ambavyo waziri mkuu aliagiza mashine zitolewe kwenye chanzo na pampu zote ziwekwe umbali wa mita 500 wanachi wakamshangilia sana na akakaribishwa Diwani wa mangola CCM naye akawa upande wa wanachi akashangiliwa kama mwenzake wa chadema baada ya hapo akakaribishwa mkuu wa Wilaya ya Karatu Mhe Taresia mahongo ndipo pale wanachi waliposimama na kuanza kupiga miluzi na kumzomea sana na mkuu wa Mkoa akaamua kumshusha jukwaani na akasema kuwa sasa yeye ataanza kuongea na akaanza kwa kusema kuwa mashine zote ni marufuku kwenye chanzo badala yake mashine ziwekwe umbali wa mita 60 hapo ndipo wananchi walipoanza kupiga kelele wakidai kuwa waziri mkuu aliagiza mita 500 leo wewe unasema mita 60 haiwezekani,, hapo wananchi waanza kusimama na kuanza kuondoka na kumwacha mkuu wa Mkoa akiwa jukwaani na ikawa ndo mwisho wa mkutano ikabidi ashuke jukwaani,,,

Sababu kubwa ambayo wananchi wanalalamikia ni kitendo cha waziri mkuu kusema Mashine ziwekwe umbali wa mita 500 toka chanzo cha maji na leo mkuu wa Mkoa kusema iwe mita 60 ,, wananchi wanaamini kuwa mkuu huyo wa mkoa anawahujumu wananchi na amepunguza hizo mita kutokea 500 za waziri mkuu hadi 60 kwa sababu ya kumpendelea mkulima mkubwa wa vitunguu ambaye pia ni mnec wa CCM ndg Daniel Awaki

Ikumbukwe kuwa hicho chanzo cha maji inategemewa na wananchi zaidi ya 20 Elfu(20,000) kwa huduma za kawaida kama kunywesha Ng'ombe na matumizi ya maji ya kawaida hivyo kitendo cha watu kuweka pampu kwenye chanzo kinawafanya wao kukosa maji

Na baada ya wananchi kumwacha mkuu wa Mkoa jukwaani ikabidi ashuke na akaagiza Madiwani wa kata ya Baray na mang'ola wakamatwe na tumejitahidi kutafuta mdhamana lakini imeshindikana police wanasema ni kwa order ya RC hivyo wanasubiri RC Gambo atoe maelekezo mengine.


Taarifa za uhakika kutoka Mangola Karatu zinasema kuwa wafanyabiashara wenye Ukwasi mkubwa wa fedha wamempa Mkuu wa mkoa fedha nyingi ili awasaidie.Rc Gambo ni miongoni mwa the most corrupt leaders in Arusha.Itakumbukwa kuwa alipewa fedha kule Loliondo,sasa Karatu.
Tabia yake hii ni aibu na fedheha kwa mteule wake yaani Mh Rais wa nchi ambaye amejipambanua kupambana na rushwa na ufisadi
Nakubalina na wewe serikali ya Magufuli imemuweka Gambo Arusha as a corrupt leader anagalia alichofanya ngorongoro magazeti yanasema amekula hela za wafanya biashara anadanganya waziri mkuu ambaye naye anaweza kubariki corruption kwa kumwita GAMBO eti JEMBEEEEEEEEEEEEEEEEE, unayaona sasa haya ya kupokea hongo kwa mlimaji wa vitunguu anayekausha vyanzo vya maji serikali haina nidhamu waziri mkuu anasema mita mia tano yeye anasema 60 halafu anakamata Diwani na nyie waarusha kwa nini munamuangalia tuu corrupt leader mume kula maharage ya wapi nyie
 
Haya tujikumbushe jana ilivyokuwa Mkuu wa Mkoa akizungumza na Wananchi mbona sioni alipozomewa! Acheni ushabiki maandazi nyie kila kitu mnapotosha tu!
Na mwisho wenyewe ndio hapa Mh Gambo akihitubia na wananchi wakimsikiliza kwa makini....ushahidi wa aliyezomewa nshautoa juu

haya Macho yatawatoka Kodo aliyezomewa Vs Aliyeskilizwa na Wananchi Vs Uzi Wenu wa Fekale
 
Wananchi wamechoshwa na maigizo
Unanikumbusha na ishu ya wafanyabiashara wadogo na wakubwa waliokuwa wakimiliki frame stand ndogo nilishangaa jamaa huyu alipoamua kuwa upande wa wafanyabiashara wakubwa na kuamua kuwamilikisha frame ambazo ni mali ya halmashauri
 
Unanikumbusha na ishu ya wafanyabiashara wadogo na wakubwa waliokuwa wakimiliki frame stand ndogo nilishangaa jamaa huyu alipoamua kuwa upande wa wafanyabiashara wakubwa na kuamua kuwamilikisha frame ambazo ni mali ya halmashauri
Sasa hapo akiitwa corrupt leader hawataki yaani awaache wahitaji akawaongeze wenye nacho kwa sababu kashikishwa mkono no wonder laana inapiga nchi hii matetemeko ukame mauaji ya watu kwenye visandarusi
 
Haya tujikumbushe jana ilivyokuwa Mkuu wa Mkoa akizungumza na Wananchi mbona sioni alipozomewa! Acheni ushabiki maandazi nyie kila kitu mnapotosha tu!

haya Macho yatawatoka Kodo aliyezomewa Vs Aliyeskilizwa na Wananchi Vs Uzi Wenu wa Fekale
ha ha kwa nini umeedit wakati tumeletewa ile aliyozomewaa na la mwisho nakuachwa akishangaa maana alidhani kijogoo wakupindisha taratibu ili mradi kapewa rushwa kwa minajili ya mtoa habari
 
View attachment 451630kwahiyo hii ndio habari? Kweli upumbavu ni hasara sana

Kwanza hiyo miradi ya maji Dr Slaa aliwapigania sana watu wa karatu halafu sasa hivi inahujumiwa na vijana wa juzi tena mi nawaita wapumbavu tu maana hata elimu yao ni ya kuunga na kubebwa na chama cha magamba.

Nonsense
Mimi na changia hoja ya hiyo picha,kweli anahitaji maombi.
 
Na mwisho wenyewe ndio hapa Mh Gambo akihitubia na wananchi wakimsikiliza kwa makini....ushahidi wa aliyezomewa nshautoa juu

kama kuna mtu anayetumiwa inamaanisha alikuwa anazimewa, naona anapiga bit
 
Mwingine kasema akipita Arusha watu wanafunga pua wanamtema mate yaani ananuka kwa rushwa chuki uongo uzandiki hawamtaki kabisa
 
Back
Top Bottom