ikipendaroho
JF-Expert Member
- Jul 26, 2015
- 3,903
- 3,850
sasa kwanini usingejitolea kwenda mamlaka usika ku report wakautoe..? umekuja ku report JF ?
Mimi hili suala huwa silipendi hata kidogo. Watu wa mazingira ni kazi yao na wanalipwa sio kusafisha na kuzoa taka tu, bali hata kuvumbua mbinu kupunguza uchafu kusambaa. Wao hawalipwi kukaa ofisini na kusubiri simu tuwaarifu uchafu uko wapi. Ikiwa mimi mkaazi au mpita njia nauona uchafu ama chanzo cha uchafu, inatakiwa yeye awe keshauona na keshautafutia ufumbuzi. Iwe nikitokezea kupiga simu basi jawabu lake liwe tushapata taarifa hiyo na tuko njiani kutatuwa hilo tatizo.
La muhimu kuwe na sheria ya wananchi kuweza kuwashitaki hawa watu kama wanvyotushitaki sisi. Kiweko kitengo maalumu kinachojitegemea katika halmashauri ambapo mwananchi anakwenda kutoa mashitaka yake, na kama hichi kitengo wataona kuna mashiko juu ya haya malalamiko ya wananchi basi hawa mazingira washitakiwe na watoleshwe fine au hata kifungo cha jela. Hapo tunaweza kukaa sawa. Lakini hii ya kwa sasa kuwa wanatushitaki sisi tu, ni uonevu mtupu. There are always two sides of a coin
Kuhusu huyu ku report hapa JF, namuunga mkono, kwani anajuwa habari kwa kupitia JF zitawafika walengwa na mabosi wao kwa haraka zaidi kuliko ku report kwao.