Mkuu wa Mkoa Dar, Jipime kuhusu Taka zilizorundikana Barabarani

Hii dhana haipo dar peke yake hata arusha nalo ni tatizo hawa wakuu waliitikia wito wa rais bila kujipanga haiwezekan wananchi tumefanya usafi tokea tarehe 09-12 hadi leo uchafu ulipokusanywa upo wala hawaba dalili za kuutoa tumekusanya mafungu ya uchafu ili kuhararisha mlipuko wa kupindupindu? Jiji la arusha angalien hili
 
Tuseme ukweli mkuu wa mkoa wa Dar alilala kwa kazi, hakufanya juhudi zozote za kuhakikisha upatikanaji wa magari ya kuzoa taka, nilitegemea angeomba magari ya polisi siku hiyo yangesaidia kufanyakazi ya kuzoa taka, nilitegemea angeenda kuomba magari ya jeshi nayo yaungane katika zoezi hili, nilitegemea angewaita wamiliki wa mafuso ya mchanga na kokoto nao wangeshiriki zoezi la kubeba taka.

Yapo mafuso yameegeshwa maeneo mbalimbali yakisubiria mizigo ya kwenda mikoani yangeombwa nayo yasaidie kupeleka taka dampo, yapo maroli ya jkt na magereza, sikuona ushirikishwaji wa wafungwa katika zoezi hili la kuzoa taka.

Naamini wadau niliowataja kama wangeshirikishwa sawa sawa basi mji ungekuwa safi zaidi ya hapa tulipo sasa.

Umeongea cha maana sana mkuu
 
Picha haionekani.
hili zoezi liwe endelevu taka bado zipo mkazizoe maana mabulungutu mtayakuta hasa siku itakapotangazwa zinabadilishwa
attachment.php

picha za malundo ya taka zipo nyingi tu Kaka Jambazi
 
sasa kwanini usingejitolea kwenda mamlaka usika ku report wakautoe..? umekuja ku report JF ?
 
Ukistaajabu ya Musa hujayaona ya Firauni, sio huko Dar na Arusha tu jijini kwetu ndiyo usiseme mpaka dakika hii kuna vifusi vya uchafu eti magari ya kuzoa taka ni mabovu. Hivi kumbe hamkuwa na maandalizi?
 

Attachments

  • 1449990529353.jpg
    1449990529353.jpg
    102.3 KB · Views: 310
Ukistaajabu ya Musa hujayaona ya Firauni, sio huko Dar na Arusha tu jijini kwetu ndiyo usiseme mpaka dakika hii kuna vifusi vya uchafu eti magari ya kuzoa taka ni mabovu. Hivi kumbe hamkuwa na maandalizi?
 
Mawaziri husika wameshateuliwa wachukue hatua sasa mm nadhani kwa Dsm naunga mkono hoja
 
Kwa hali hii TUWATUMIE JESHI LETU LA ULINZI MAGARI YAO YAFANYE OPERESHENI UZOAJI WA TAKA.HILI PIA LITAKUWA ONYO KWA WANANCHI WANAOTUPA UCHAFU OVYO OVYO WAKIWAHOFIA WANAJESHI WETU IWE KWA MUDA HUU TU KWANI HALMASHAURI WAMEZIDIWA NA HAO WAKANDARASI UCHWALA WA UZOAJI WA TAKATAKA WALIOLAMBA TENDA TUTAFAKARI TUSILAUMU TU TUTOE PLAN B
 
Tarehe 09.12.2015 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania JPM aliagiza iadhimishwe kwa kufanya usafi wa mazingira ikiwa ni jitihada za kukabiliana na ugonjwa wa kipindupindu.

Mwitikio wa wananchi ulikuwa mkubwa hali iliyoonyesha kuwa huko nyuma hakukuwa na mwamko miongoni mwa viongozi ktk swala zima la kuhamasisha na kusimamia usafi.

Kinachonishangaza ni kuona takataka zilizojusanywa na kulundikwa sehemu moja hadi leo bado hazijazolewa na Mkuu wa Mkoa bado anacheka na watendaji wake.

Kwa mimi mwananchi wa kawaida tafsiri ninayopata kwa kutokuzolewa kwa taka hizo ni kumkwamisha mhedhimiwa Rais ili aonekane juhudi zake ni nguvu ya soda.

Mkuu wa Mkoa kama kiongozi uliyekabidhiwa rungu tunakutaka ujipime ktk nafasi uliyonayo iwapo unatosha kuendelea kuvaa viatu vya nafasi hiyo huku ukishindwa kuwawajibisha wa chini yako.

Hivi Mkuu wa Mkoa unashindwa nini kuwaandikia Wakurugenzi wa Halmashauri zote tatu kutaka wakupe maelezo kwa nini taka hazizolewi.

Mbona Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni angalau anajitutumua na kuwaweka watendaji wake ndani kwa utovu wa nidhamu.
Kwenye nyekundu: Unaonyesha ulivyo na akili finyu ya kimanamba! Jaribu kufikiria tena na kwa kina!
 
Kwa hali hii TUWATUMIE JESHI LETU LA ULINZI MAGARI YAO YAFANYE OPERESHENI UZOAJI WA TAKA.HILI PIA LITAKUWA ONYO KWA WANANCHI WANAOTUPA UCHAFU OVYO OVYO WAKIWAHOFIA WANAJESHI WETU IWE KWA MUDA HUU TU KWANI HALMASHAURI WAMEZIDIWA NA HAO WAKANDARASI UCHWALA WA UZOAJI WA TAKATAKA WALIOLAMBA TENDA TUTAFAKARI TUSILAUMU TU TUTOE PLAN B

Nchi hii haihitaji kibabe na kuwatisha wananchi, kutumia jeshi ni sawa ila serikali iweke vifaa vya kuweka taka kila mita 100

Hapo ndio unaweza kumlaumu mwanachi kama watatuoa taka ovyo.

Mm naamini Watz ni wasikivu sana na mifano tunaiona kwenye muitikio huu wa uzoaji taka.
 
Hili halina mana ya kuwatisha raia ila basi uchafu huo ukiachwa muda mrefu ni mlipuko wa maradhi.na hili la maradhi ni vita mimi binafsi siuoni ubaya wo wote magari ya jeshi yakawamobilized kusaidia jambo hili ni sawa tu na mafuriko yanapotokea.tusianze kulaumu ooh serikali haikujipanga!la muhimu hapa ni vipi uchafu huu utaondolewa wakosoaji kwa maslahi yao hawakosi leta wazo tusilaumu
 
ndo maana wananchi wamewapa ukawa nao wajaribu angalau watakuja na mbinu nyingine japo tayari kuna malalamiko watendaji wa ukawa wanaomba pesa watu wanaokwenda kupata huduma pasipo kutoa risiti.

Kwani huki ulikojaa uchafu si pengine serikali za mitaa ni ukawa ama wao wanahisi ni sawa ?
 
Hili zoezi lilikuwa na malengo mazuri na wote tulipenda lifanikiwe na liwe endelevu lakini inaonekana liliendeshwa pasipo mikakati na malengo maalumu.Labda kama kulikuwa na malengo ya PR ya kisiasa.Kwa nini wasingetenga mafungu kiasi toka pesa zilizo okolewa kutoka gharama za sherehe za uhuru kwa ajili ya kukodi agari ya kuzoa hizo taka?Kwa jinsi mambo yanavyoenda napata mashaka makubwa muda ukifika mipango ya kutoa elimu bure itakuwa na kasheshe la aina yake,only time will tell.


Kuna makampuni yaliyoshinda zabuni ya kufanya usafi wa mji wanalipwa mabilioni ya pesa. Cha kujiuliza ni kuwa, ikiwa wananchi wamewasaidia kazi ya usafi na kuwakusanyia uchafu wao waokote tu wakatupe na wameshindwa, wataweza kweli kufanya usafi wa jiji? Na baya zaidi, mpaka taasisi nyengine kama JWTZ zinasaidia katika hili zoezi la kuokota huu uchafu.

Kinachonishangaza mimi ni kwa nini viongozi husika hawalisimamii hili agizo la Mh Raisi mpaka likagikia lengo. Labda wanasubiri Mh Raisi afanye ziara ya kushtukizia tena aone huo uchafu. Nafikiri kuipa jina la uchafu wa Magufuli itasaidia zoezi likamilike haraka, kwa sababu wataogopa jina lisitapakae mpaka mwenyewe akalisikia. It's not fair on him, officials let him down big time!
 
Back
Top Bottom