MTAANI KWENU HAKUNA MTU ANAYEJENGA "GUEST" TUMUITE RC AJE KUZINDUA??
Kuna watu hawailewi CHADEMA inaposema vyeo vya Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya vifutwe katika Katiba. Ukweli ni kwamba DC na RC wanafilisi tu nchi hii kwa kula mishahara mikubwa, magari ya kifahari, posho na marupurupu mengine bila kufanya kazi yoyote ya maana.
Kazi zote za kiutendaji zinafanywa na wakurugenzi wa halmashauri au makatibu tawala. So DC na RC hawana kazi wafanyayo.
Labda hujanielewa ni hivi DC na RC hata wao wenyewe hawajui kazi yao ni ipi. Ndio maana wanaishia kufanya kazi kama hizi.
Eti RC mzima anaenda kufungua GUEST ya mtu. Very shameful. Yani jamaa kajenga Guest yake, halafu akatafuta mtu wa kuzindua. Kwa dharau akamualika RC. Na RC nae bila aibu akaenda kuzindua Guest ya mtu.
Kazi ya kuzindua Guest haipaswi kufanywa hata na mjumbe wa nyumba kumi achilia mbali RC. Lakini kwa kuwa RC hana kazi unamuita tu, unamwambia nizindulie Guest yangu, nae anakuja kuzindua.! Aibu sana hii.
Mi nilidhani Guest huwa inazinduliwa na wageni waliokosa makazi, plus wale jamaa wa kuvunja amri ya sita, kumbe hata Mkuu wa mkoa anaweza kuzindua.?? Vp mtaani kwenu hakuna mtu anajenga GUEST tumuite RC aje kuzindua??