Dalton elijah
JF-Expert Member
- Jul 19, 2022
- 780
- 1,831
Mkuu wa Majeshi wa Uganda, Jenerali Muhoozi Kainerugaba, amemjibu tena Seneta wa Marekani Jim Risch kupitia mtandao wa X siku ya Jumanne, Februari 3, 2026, baada ya kuomba radhi hapo awali.
Mzozo huu wa maneno umeibuka kati ya Uganda na Marekani baada ya Muhoozi kuchapisha na baadaye kufuta baadhi ya taarifa zilizosababisha utata kati ya Muhoozi na seneta huyo wa Marekani.
Hapo awali seneta huyo wa Marekani alimwambia Muhoozi kwamba baadhi ya ‘tweet’ zake zilizofutwa ambazo zilikashifu Ubalozi wa Marekani jijini Kampala zilivuka mstari mwekundu.
Muhoozi alikuwa amelihusisha Ubalozi wa Marekani na siasa za upinzani nchini humo, na hata kupendekeza kusitishwa kwa ushirikiano wa kijeshi kati ya Uganda na Marekani.