Mongoiwe
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 524
- 270
Mkuu wa Magereza Mwanza matatani
Na Mwandishi Wetu
MKUU wa Magereza Mkoa wa Mwanza Kamishna Msaidizi Mwandamizi Ahmed Kopwe, amejikuta katika wakati mgumu baada ya kumdanganya Kamishna Mkuu wa Magereza nchini Augustino Nanyaro, kuhusiana na gharama za ujenzi wa nyumba za maafisa wa gereza kuu la Butimba.
Katika hali isiyotarajiwa, Kopwe alijikuta akidanganya juu ya gharama halisi za ununuzi wa matofali yanayotumika kujenga nyumba tano za maafisa hao, ambao ujenzi wake uko katika hatua ya lenta.
Tukio hilo lilitokea wakati Kamishna wa Magereza nchini akikagua ujenzi wa nyumba hizo, alipofanya ziara ya siku mbili Mkoani Mwanza ambapo alimuuliza Kopwe kuhsu gharama zilizotumika kununulia matofali hayo.
Kopwe alijibu kuwa tofali moja la kuchoma walinunua kwa shilingi 600/= , baada ya kauli hiyo wajumbe wa kamati ya ulinzi ya Mkoa waliofuatana na Nanyaro katika ziara hiyo waliguna kuashiria kwamba gharama hizo si za kweli, huku Kamishna huyo akitikisa kichwa.
Baada ya Kutamkwa bei hiyo, mmoja wa maofisa walifuatana na Kamishna kutoka makao makuu ya Magereza Kamishna Msaidizi Mwandamizi ambaye ni Mkuu wa utawala na fedha wa jeshi hilo alihoji tfali la kuchomwa linalouzwa Morogoro shilingi 150/- liuzwe Mwanza kwa shilingi 600/-.
Swali ambalo hata hivyo RPO Kopwe hakulijibu, baada ya hali hiyo gazeti hili liliambiwa na mmoja wa maafisa wa Gereza la Butimba kuwa matofali hayo yalifyatuliw ana kuchomwa na wafungwa wa gereza hilo na kwamba hata kama yangenunuliwa bei isingezidi shilingi 200/-.
Kamishana Nanyaro ambaye kitaaluma ni Mhandisi wa Ujenzi, alishtukia maelezo hayo na kumwagiza Kopwe kuandaa mchanganuo wa gharama za ujenzi wa nyumba hizo kwa kuthaminisha nguvu za wafungwa ili kupata gharama halisi.
Hata kama mnawatumia wafungwa katika ujenzi huu lazima mthaminishe nguvu kazi zao kujua gharama halisi maana hizo ndizo zinaitwa nguvu za wananchialisema Nanyaro na kuendelea na ukaguzi.
Awali akitoa maelezo ya ujenzi wa nyumba hizo kwa Mkuu wa magereza nchini, Rpo Kopwe alisema kwamba ujenzi wa nyumba hizo tano ambao hakutaja gharama zake na lini ulianza, unalenga kupunguza tatizo la makazi linalowakabiri maofisa wa gereza hilo.
Kopwe alisema kuwa alishindwa kubainisha gharama halisi za ujenzi huo kutokana na kutofanya tathmini na kuahidi kurekebisha kasoro hizo.
Wakati wa ziara yake katika gereza hilo, Nanyaro alitunuku Nishani kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete kwa askari na maofisa 41 wa Magereza katika mikoa ya kanda ya ziwa ambazo ni Nishani ya Utumishi uliotukuka Tanzania na Utumishi wa muda mrefu na tabia njema Tanzania.
Source: Gazeti la Matukio Daima (Gazeti la kanda ya Ziwa)