Mkuu wa Magereza Mwanza Matatani! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkuu wa Magereza Mwanza Matatani!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mongoiwe, Apr 25, 2009.

 1. Mongoiwe

  Mongoiwe JF-Expert Member

  #1
  Apr 25, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 521
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  Mkuu wa Magereza Mwanza matatani

  Na Mwandishi Wetu
  MKUU wa Magereza Mkoa wa Mwanza Kamishna Msaidizi Mwandamizi Ahmed Kopwe, amejikuta katika wakati mgumu baada ya kumdanganya Kamishna Mkuu wa Magereza nchini Augustino Nanyaro, kuhusiana na gharama za ujenzi wa nyumba za maafisa wa gereza kuu la Butimba.
  Katika hali isiyotarajiwa, Kopwe alijikuta akidanganya juu ya gharama halisi za ununuzi wa matofali yanayotumika kujenga nyumba tano za maafisa hao, ambao ujenzi wake uko katika hatua ya lenta.
  Tukio hilo lilitokea wakati Kamishna wa Magereza nchini akikagua ujenzi wa nyumba hizo, alipofanya ziara ya siku mbili Mkoani Mwanza ambapo alimuuliza Kopwe kuhsu gharama zilizotumika kununulia matofali hayo.
  Kopwe alijibu kuwa tofali moja la kuchoma walinunua kwa shilingi 600/= , baada ya kauli hiyo wajumbe wa kamati ya ulinzi ya Mkoa waliofuatana na Nanyaro katika ziara hiyo waliguna kuashiria kwamba gharama hizo si za kweli, huku Kamishna huyo akitikisa kichwa.
  Baada ya Kutamkwa bei hiyo, mmoja wa maofisa walifuatana na Kamishna kutoka makao makuu ya Magereza Kamishna Msaidizi Mwandamizi ambaye ni Mkuu wa utawala na fedha wa jeshi hilo alihoji tfali la kuchomwa linalouzwa Morogoro shilingi 150/- liuzwe Mwanza kwa shilingi 600/-.
  Swali ambalo hata hivyo RPO Kopwe hakulijibu, baada ya hali hiyo gazeti hili liliambiwa na mmoja wa maafisa wa Gereza la Butimba kuwa matofali hayo yalifyatuliw ana kuchomwa na wafungwa wa gereza hilo na kwamba hata kama yangenunuliwa bei isingezidi shilingi 200/-.
  Kamishana Nanyaro ambaye kitaaluma ni Mhandisi wa Ujenzi, alishtukia maelezo hayo na kumwagiza Kopwe kuandaa mchanganuo wa gharama za ujenzi wa nyumba hizo kwa kuthaminisha nguvu za wafungwa ili kupata gharama halisi.
  “Hata kama mnawatumia wafungwa katika ujenzi huu lazima mthaminishe nguvu kazi zao kujua gharama halisi maana hizo ndizo zinaitwa nguvu za wananchi”alisema Nanyaro na kuendelea na ukaguzi.
  Awali akitoa maelezo ya ujenzi wa nyumba hizo kwa Mkuu wa magereza nchini, Rpo Kopwe alisema kwamba ujenzi wa nyumba hizo tano ambao hakutaja gharama zake na lini ulianza, unalenga kupunguza tatizo la makazi linalowakabiri maofisa wa gereza hilo.
  Kopwe alisema kuwa alishindwa kubainisha gharama halisi za ujenzi huo kutokana na kutofanya tathmini na kuahidi kurekebisha kasoro hizo.
  Wakati wa ziara yake katika gereza hilo, Nanyaro alitunuku Nishani kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete kwa askari na maofisa 41 wa Magereza katika mikoa ya kanda ya ziwa ambazo ni Nishani ya Utumishi uliotukuka Tanzania na Utumishi wa muda mrefu na tabia njema Tanzania.

  Source: Gazeti la Matukio Daima (Gazeti la kanda ya Ziwa)
   
 2. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #2
  Apr 25, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  hehehe
  hehehe
  haya hata saluti nazo zinadanganya eeeh!
   
 3. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #3
  Apr 25, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  ujenzi wa nyumba za wafanyakazi wa magereza ni jambo jema sana. Kama huyu afande kakosa basi wampe adhabu ya ujenzi wa nyumba zingine tano bila bajeti ama nusu bajeti
   
 4. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #4
  Apr 25, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,434
  Likes Received: 5,691
  Trophy Points: 280
  Mod badilisha kichwa cha habari weka
  mkuu wa magereza akumbwa na uufisadi...hii mnampendelea sana mshenzi wa tabia
   
 5. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #5
  Apr 25, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Jamaa hajui hata kujipanga??hata aibu hana??jamani tumuogopeni Mungu.....du aibu sana
   
 6. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #6
  Apr 26, 2009
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,276
  Likes Received: 4,260
  Trophy Points: 280
  Kama ni ufisadi nafikiri huko magereza umekithiri kazi/miradi mingi wanayofanya wanatumia wafungwa kama ni matofali ya kuchoma sidhani kama kuna gharama yeyote waliyotumia kwani mchanga utachimbwa na wafungwa ,watachoma matofali na ujenzi wote kazi inafanywa na wafungwa but jamaa wakiandika bajeti wanasema eti wamenunua
   
 7. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #7
  Apr 26, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  ufisadi kila kona
   
 8. M

  Mtamu Member

  #8
  Apr 26, 2009
  Joined: Apr 21, 2009
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  take the important message only.
   
Loading...