Mkuu wa Kituo Cha Polisi Mwenge anakula Rushwa hadharani, IGP chukua hatua

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,277
8,840
Mamlaka zinazohusika mwangalieni mkuu wa kituo cha polisi cha Mwenge. Huyu mama anakula rushwa haradani, Nitaeleza. Hapo mwenge kuna wamachinga, Ambao kimsingi,,Mkuu wa wilaya kawatengea eneo rasmi la kufanyia biashara zao.

Lakini mkuu wa kituo cha polisi mwenge, Huamasisha baadhi yao wasiende eneo walilotengeawa. Na hivyo anawauzia eneo la barabarani.

Kila meza moja huyu mama anauza kwa laki moja. Hivyo kusababisha kero kwa watu wengine wanaofanya manunuzi yao mwenge pamoja na wafanyabiashara wa eneo hilo.

Niliona jitihada za kuwatoa zimefanyika na halimashauri lakini baada ya masaa kadhaa machinga wakajichanga na kumpa rushwa Mkuu wa kituo na kuwarejesha tena.

IGP watume vijana wako mwenge wapeleleze juu ya hili utapigwa na butwaa. Mbaya zaidi mkuu wa polisi mwenge kutokana na kuwa na maslahi binafsi na machinga hao wachache, Amekuwa anaingilia majukumu ya mtendaji wa kata husika, Na hivyo kuwa na mgogoro wao kwa wao.

Na kwa taarifa ni kuwa mkuu huyu wa kituo cha polisi mwenge anazo meza zake alizopanga barabarani na kuzipangisha kwa machinga,Kazi yake ni kuokota ushuru kinyemela na kuweka mfukoni. mamlaka chukueni hatua za haraka kabla ya mambo kuharibika.

Ni mimi mzalendo mpita njia!
 
Ni taarifa nzr na nzito kidogo ngoja tuone mamlaka zinazohusika kwani umeisukuma taarifa juu sana kwa IGP nadhani tutapata majibu mapema na sisi tunafuwatilia kwa haraka hili tupate tukio.
 
Polis tunawaomba hizi taarifa za mkuu wa kituo mwenge mzifanyie kazi wenyewe mtapata ukweli,pia polisi wasipochukua hatua mapema mwenge yatatokea maafa Kama yale ya afrika ya kusini
Vijana kutwa wanakunywa konyagi wameshinda na Mapanga muda wote maafa yatatokea mwenge,wameapa kuuwa watu ndio waondoke
Tafadhalini jeshi la polisi tuanawaomba mfanyie kazi hizi taarifa
 
Sio Mwenge Tu Magenge Ya Rushwa Ni Vituo Karibu Vyote Dar.
.
Tatizo Ata Bosi Wao Waziri Anachukua Rushwa.

Mkuu huyu mkuu wa kituo cha polisi mwenge nje ya rushwa anakusanya ushuru wa mh rais kama mali yake. anatia hadi aibu jeshi
 
Hofu yangu kubwa ni uhalifu unaoweza kutokea maana hawa vijana hawalali usiku kucha wako pale mwenge wanaweka meza za barabarani kwa kutumia jina la rais vibaya,karikoo mbona wao hawajapanga meza barabarani?
 
Wewe ni mtendaji Kata?
Hofu yangu kubwa ni uhalifu unaoweza kutokea maana hawa vijana hawalali usiku kucha wako pale mwenge wanaweka meza za barabarani kwa kutumia jina la rais vibaya,karikoo mbona wao hawajapanga meza barabarani?
 
Back
Top Bottom