Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Jakaya Kikwete, atembelea chuo hicho

TataMadiba

JF-Expert Member
Feb 7, 2014
9,866
5,742
1.jpg

MKUU mpya wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ambaye ni Rais mstaafu Jakaya Kikwete, ametembelea chuo hicho kujifunza na kujionea hali halisi ilivyo, kabla ya kukabidhiwa rasmi wadhifa huo.

Kikwete aliyekuwa Rais wa Awamu ya Nne, ameteuliwa hivi karibuni na Rais John Magufuli kushika wadhifa huo, baada ya kufariki kwa Balozi Fulgence Kazaura mwaka 2013.

Akiwa chuoni hapo majira ya mchana, Kikwete alitembelea Chuo cha Uhandisi, Jengo jipya la Sayansi, kumbi za mihadhara za Yombo na eneo ambalo itajengwa maktaba mpya ya kisasa.

Akiwa katika Ukumbi wa Yombo, aliwaambia wanafunzi kuwa Rais John Magufuli amempa kazi ya kuwa mkuu wa chuo, hivyo amefika hapo kujionea hali halisi kabla ya kukaa na viongozi kutengeneza chuo hicho kiwe bora zaidi.

Akiondoka katika eneo la ukumbi huo, baadhi ya wanafunzi walimfuata na kumweleza kuwa zaidi ya miezi miwili hawajapewa fedha za kujikimu, hivyo aliwaahidi kuwasaidia kwa kulisemea sehemu husika.

Baada ya ziara hiyo, Kikwete alikutana na watendaji mbalimbali wa chuo hicho na kuwaeleza kuwa ujio huo umempa kukifahamu chuo hicho kwa sehemu. “Nimefurahi fursa hii ya kutembea leo (jana) kabla ya siku rasmi ya kukabidhiwa uongozi wa chuo.

"Bado natamani Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kiwe bora kuliko vyote nchini. Sina maana vingine vitakuwa duni, hapana. Ila kiwe ni chuo kinachotoa viongozi. Mtu akitaka kiongozi aanzie kumtafuta kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, akikosa ndio aende chuo kingine.

"Na hivyo vyuo vingine watafute maeneo ambayo watayakomalia ili nao wafuatwe,” alisema Kikwete ambaye alisoma hapo katika miaka ya 1970.

Alisema amesikia kilio cha wanafunzi hao baada ya kumwambia hali ni tete kwa kuwa hawajapata fedha, hivyo japo hajakabidhiwa rasmi nafasi hiyo, ataanza na hilo ili vijana wasome vizuri.

Aliahidi kurudi kabla ya mwezi huu kuisha ili akutane na viongozi mbalimbali, lengo ni kukielewa vizuri kabla ya kukabidhiwa rasmi
 
teheetehetehee!!eti kukitengeneza kiwe bora zaidi Jk huyu huyu ndo wakutengeneza UDSM kiwe bora zaidi?.Alafu mimi ninavyofahamu,mkuu wa chuo ni ceremonial lakini naona mkulu wa zamani yeye amefanya ni ofisi ya kwenda kufungua saa mbili asubuhi hadi saa kumi na moja jioni.
 
Jiongeze ndugu utakuwaje ceremonia leader kwenye taasisi ambayo huijui? Naamini hii ni mara yake ya kwanza kufika chuoni hapo tangu ateuliwe kukiongoza.
 
1.jpg

MKUU mpya wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ambaye ni Rais mstaafu Jakaya Kikwete, ametembelea chuo hicho kujifunza na kujionea hali halisi ilivyo, kabla ya kukabidhiwa rasmi wadhifa huo.

Kikwete aliyekuwa Rais wa Awamu ya Nne, ameteuliwa hivi karibuni na Rais John Magufuli kushika wadhifa huo, baada ya kufariki kwa Balozi Fulgence Kazaura mwaka 2013.

Akiwa chuoni hapo majira ya mchana, Kikwete alitembelea Chuo cha Uhandisi, Jengo jipya la Sayansi, kumbi za mihadhara za Yombo na eneo ambalo itajengwa maktaba mpya ya kisasa.

Akiwa katika Ukumbi wa Yombo, aliwaambia wanafunzi kuwa Rais John Magufuli amempa kazi ya kuwa mkuu wa chuo, hivyo amefika hapo kujionea hali halisi kabla ya kukaa na viongozi kutengeneza chuo hicho kiwe bora zaidi.

Akiondoka katika eneo la ukumbi huo, baadhi ya wanafunzi walimfuata na kumweleza kuwa zaidi ya miezi miwili hawajapewa fedha za kujikimu, hivyo aliwaahidi kuwasaidia kwa kulisemea sehemu husika.

Baada ya ziara hiyo, Kikwete alikutana na watendaji mbalimbali wa chuo hicho na kuwaeleza kuwa ujio huo umempa kukifahamu chuo hicho kwa sehemu. “Nimefurahi fursa hii ya kutembea leo (jana) kabla ya siku rasmi ya kukabidhiwa uongozi wa chuo.

"Bado natamani Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kiwe bora kuliko vyote nchini. Sina maana vingine vitakuwa duni, hapana. Ila kiwe ni chuo kinachotoa viongozi. Mtu akitaka kiongozi aanzie kumtafuta kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, akikosa ndio aende chuo kingine.

"Na hivyo vyuo vingine watafute maeneo ambayo watayakomalia ili nao wafuatwe,” alisema Kikwete ambaye alisoma hapo katika miaka ya 1970.

Alisema amesikia kilio cha wanafunzi hao baada ya kumwambia hali ni tete kwa kuwa hawajapata fedha, hivyo japo hajakabidhiwa rasmi nafasi hiyo, ataanza na hilo ili vijana wasome vizuri.

Aliahidi kurudi kabla ya mwezi huu kuisha ili akutane na viongozi mbalimbali, lengo ni kukielewa vizuri kabla ya kukabidhiwa rasmi

Wanasaisa wote Duniani huwa wanafanana ona sasa Raisi Kikwete anaahidi mambo ambayo miezi Mitatu iliyopita alikuwa Raisi wa nchi na angeweza kuyafanya leo hana madaraka atayafanya vipi? Wanafunzi hawajalipwa alikuwa na uwezo wa kulitatua hili tatizo mara moja lkn hakufanya leo yuko nje wakati hawezi hata kumtuma mtu chai, anaahidi Mbingu!

Inanikumbusha Raisi wa Marekani Bill Clinton alikutana na wanafunzi wa Waafrika akaanza kuwaambia stori ndeefu ya jinsi alivyodhamiria kusadia kupunguza umaskini Afrika, Mwanafunzi mmoja akamuuliza mbona wakati uko Raisi haukilifanya hilo kwa maana ndiyo ulikuwa na uwezo zaidi iweje umeshatoka leo ndiyo unasema unataka kusaidia Afrika wakati uwezo wako wa ushawishi umepungua ? Akaaanza kujiuma uma akakokosa jibu!

Hata Raisi Obama suburini mtaona muda wake ukiisha ndiyo ataanza kushughulika na Afrika mikutano kibao NGO za kila aina, ndio ataanza kwenda mageto wa Wamarekani weusi yeye na Mke wake na kuwaambia amekuja kuwasaidia ili wasome college na kupata ajira wakati yuko Raisi sasa hivi hana habari, tena ndiyo kwanza anawapiga mabomu Afrika, akitoka Uraisi utamuona yeye ndiyo anageuka kuwa mshauri wa Nigeria kupambana dhidi ya Boko Haramu au Kenya na Al Shabab!
 
"Bado natamani Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kiwe bora kuliko vyote nchini. Sina maana vingine vitakuwa duni, hapana. Ila kiwe ni chuo kinachotoa viongozi. Mtu akitaka kiongozi aanzie kumtafuta kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, akikosa ndio aende chuo kingine.

Haya bana Pro JK!
Unawaza uongozi tu! Kweli ndiyo maana uliwahi kunukuliwa kuwa hujui kwanini Nchi yako TZ ni Maskini!
Mlimani si kiwanda cha kutenegeneza Viongozi bali iwe chuo ambacho wenye kuwaza watatupa jibu kwanini sisi siyo maskini na siyo kwa maneno bali kwa vitendo!

Raia Mwema - Kimfaacho JK ni asasi za hisani, si urais!

Jamii Forums on Twitter: "TUJIKUMBUSHE: Kikwete - Sijui kwani
 
Kama kuna mtu anayewatesa CHADEMA hadi leo hii basi ni JK! Wanachuki ya ajabu sana juu ya huyu mzee, na mzee ndo anazidi kukubalika nationally and internationally, wao kapi lao lipo tu limefulia na halina issue!

Wewe ni kati ya wale 46?
 
1.jpg

MKUU mpya wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ambaye ni Rais mstaafu Jakaya Kikwete, ametembelea chuo hicho kujifunza na kujionea hali halisi ilivyo, kabla ya kukabidhiwa rasmi wadhifa huo.

Kikwete aliyekuwa Rais wa Awamu ya Nne, ameteuliwa hivi karibuni na Rais John Magufuli kushika wadhifa huo, baada ya kufariki kwa Balozi Fulgence Kazaura mwaka 2013.

Akiwa chuoni hapo majira ya mchana, Kikwete alitembelea Chuo cha Uhandisi, Jengo jipya la Sayansi, kumbi za mihadhara za Yombo na eneo ambalo itajengwa maktaba mpya ya kisasa.

Akiwa katika Ukumbi wa Yombo, aliwaambia wanafunzi kuwa Rais John Magufuli amempa kazi ya kuwa mkuu wa chuo, hivyo amefika hapo kujionea hali halisi kabla ya kukaa na viongozi kutengeneza chuo hicho kiwe bora zaidi.

Akiondoka katika eneo la ukumbi huo, baadhi ya wanafunzi walimfuata na kumweleza kuwa zaidi ya miezi miwili hawajapewa fedha za kujikimu, hivyo aliwaahidi kuwasaidia kwa kulisemea sehemu husika.

Baada ya ziara hiyo, Kikwete alikutana na watendaji mbalimbali wa chuo hicho na kuwaeleza kuwa ujio huo umempa kukifahamu chuo hicho kwa sehemu. “Nimefurahi fursa hii ya kutembea leo (jana) kabla ya siku rasmi ya kukabidhiwa uongozi wa chuo.

"Bado natamani Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kiwe bora kuliko vyote nchini. Sina maana vingine vitakuwa duni, hapana. Ila kiwe ni chuo kinachotoa viongozi. Mtu akitaka kiongozi aanzie kumtafuta kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, akikosa ndio aende chuo kingine.

"Na hivyo vyuo vingine watafute maeneo ambayo watayakomalia ili nao wafuatwe,” alisema Kikwete ambaye alisoma hapo katika miaka ya 1970.

Alisema amesikia kilio cha wanafunzi hao baada ya kumwambia hali ni tete kwa kuwa hawajapata fedha, hivyo japo hajakabidhiwa rasmi nafasi hiyo, ataanza na hilo ili vijana wasome vizuri.

Aliahidi kurudi kabla ya mwezi huu kuisha ili akutane na viongozi mbalimbali, lengo ni kukielewa vizuri kabla ya kukabidhiwa rasmi
disco limeingia masai tena na rungu na sime.
 
Back
Top Bottom