Mkutano wa Rais Magufuli Kahama: James Lembeli aungana naye. Je, kurejea CCM?

mafundisho

JF-Expert Member
Sep 26, 2015
388
136
Katika hali inayoshangaza wapenzi na mashabiki wengi wa CHADEMA ni pale aliyekuwa mgombea Ubunge kupitia CHADEMA ameonekana katika mkutano wa CCM unaoendelea hapa mjini Kahama.

Wadadisi wa masuala ya kisiasa hapa Kahama wanadai kiongozi huyo aliyejizolea umashuhuri mkubwa enzi za uongozi wake kwa sasa mambo yake yamekwenda mrama hivyo njia nyepesi ni yeye kutubu na kurejea nyumbani kwao waliko mababu zake

image.jpeg


Lembeli pamoja na kushawishiwa na Magufuli "arejee kundini" hakuonekana kuafiki.

VIDEO:
Magufuli akimshawishi:


Lembeli alipopanda jukwaani:


Habari zaidi zinasema.....

Kahama. Mbunge wa zamani wa jimbo la Kahama, James Lembeli aliyehamia Chadema ameibuka leo katika mkutano wa na Rais John Magufuli uliofanyika mjini Kahama.

Akihutubia wananchi wa Kahama, Rais Magufuli amemkaribisha Lembeli na kumtaka kurudi CCM akisema kwa Tanzania anayoijua yeye hatakuwa amepoteza mkia, kwani huko aliko ndiko mafisadi wamekimbilia.

Hivi karibuni akihutubia mkutano Mkuu wa CCM, Rais Magufuli akizungumzia waliotoka kwenye chama na kurejea tena, alitoa mfano wa ng’ombe aliyekatwa mkia, akisema huwezi kumzuia kurejea zizini lakini wenzake wanamkua kuwa hana mkia.

Akizungumza kwenye mkutano huo, Lembeli amesema amekwenda kwenye mkutano huo kwa kuwa kazi anayoifanya Rais Magufuli ndiyo ambayo alikuwa anapigania wakati akiwa

mbunge kwa kuwa Shinyanga rushwa ilikuwa imekithiri.

Amesema na hawezi kurudi CCM mpaka Rais ambaye pia ni mwenyekiti wa chama hicho akisafishe.

"Kubadilisha msikiti siyo kuacha Uislamu, nyumba itaposafishika nitarudi," amesema Lembeli.

=========

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema serikali yake haitagawa chakula cha bure kwa wananchi wanaopatwa na tatizo la njaa pasipo kuwa na sababu za msingi na badala yake amewataka watanzania wajikite kufanya kazi kwa juhudi na maarifa ikiwa ni pamoja na kuzalisha chakula cha kutosha.

Rais Magufuli amesema hayo leo tarehe 31 Julai, 2016 wakati akihutubia mikutano ya hadhara na kuzungumza na wananchi waliosimamisha msafara wake akiwa njiani kutoka Mkoani Tabora kuelekea Shinyanga na baadaye Geita anakoendelea na ziara yake.

Pamoja na kuwahimiza wananchi kuzalisha chakula cha kutosha ili kuondokana na njaa Rais Magufuli amesema serikali yake itajikita kuhakikisha inashughulikia tatizo la uhaba wa maji, ujenzi wa miundombinu hususani barabara na reli, kuimarisha huduma za matibabu, elimu na kutengeneza ajira.

Akiwa Isaka Mkoani Shinyanga Rais Magufuli amesema serikali haitalipa fidia kwa wananchi waliopatwa na maafa ya mafuriko yaliyobomoa nyumba zao mwezi Machi mwaka 2015 na badala yake itajielekeza kutatua tatizo kubwa la uhaba wa maji katika mji huo ambao una makutano ya reli ya kati ya kutoka Dar es Salaam kwenda nchi za Burundi na Rwanda.

Katika Mji wa Kagongwa Rais Magufuli amepokea kilio cha wananchi dhidi ya vitendo vya ujambazi na ametoa siku tano kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga kuhakikisha watu wanaojihusisha na ujambazi wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Mjini Kahama, Dkt. Magufuli ameiagiza Wizara ya Nishati na Madini kushirikiana na Mbunge wa Kahama Mhe. Jumanne Kishimba kukokotoa mahesabu vizuri na kubaini kodi ambayo Serikali inastahili kulipwa baada ya Mbunge huyo kudai kuna kiasi kikubwa cha kodi hakijakusanywa kama ambavyo sheria inaelekeza.

Aidha, Rais Magufuli amesema serikali itahakikisha wawekezaji wanaochimba madini wanaacha kusafirisha mchanga wenye madini kwa lengo la kwenda kuchakata nje ya nchi na badala yake ametaka uchakataji huo ufanyike hapa hapa nchini.

Dkt. Magufuli amezungumza na wananchi vijiji vya Segese na Bukoli na kuwahakikishia kuwa Barabara ya Kahama, Segese, Kakola hadi Geita yenye urefu wa kilometa 146 itajengwa kwa kiwango cha lami kama alivyoahidi.

Mjini Geita, Rais Magufuli amepokea kilio cha wananchi wanaodai kuwekewa zuio la kutumia mawe yenye mabaki ya madini ya dhahabu (Magwangala) kwa lengo la kusaga na kuchenjua ili kupata dhahabu, na ametoa wiki tatu kwa Wizara ya Nishati na Madini kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kufanya tathimini na kuwaruhusu wachimbaji wadogo kutumia Magwangala.

Rais Magufuli pia ameiagiza Bodi ya Pamba hapa nchini kuhamisha ofisi zake zilizopo Jijini Dar es salaam na kuzileta katika Mikoa ya kanda ya ziwa ambako uzalishaji wa zao la pamba unafanyika.

Dkt. Magufuli amewaonya viongozi na watendaji wa bodi hiyo dhidi ya vitendo vya usambazaji wa mbegu za pamba zisizoota na amesema ikitokea tena watachukuliwa hatua.

Kesho tarehe 01 Agosti, 2016 Rais Magufuli ambaye ameongozana na Mkewe Mama Janeth Magufuli anatarajia kukamilisha ziara yake ya siku nne katika Mikoa ya Singida, Tabora, Shinyanga na Geita.

Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Geita

31 Julai, 2016

44b6446f-855e-49c4-b19f-6a4f21488143.jpg
 
Shida kweli kweli, tulimuonya MBOWE mapema juu ya hili, hao wote tuliowapokea ni wasaka madaraka wakiongozwa na baba yao EL, kama kweli walikuwa na mapenzi ya dhati juu ya mageuzi na ukombozi wa kweli basi wasingesubiri kukatwa tena kipindi cha uchaguzi halafu na bado 90% ya tuliowapokea moja kwa moja walipewa nafasi za kugombea uongozi aka ubunge na urais.. TUNAHITAJI MAGEUZI YA KWELI NA SI SANAA ZA MWENYEKITI NA NDUGU ZAKE..
 
Cha kushangaza na.kujiuliza kwa nini mtu anapo toka ccm anaanguka kimaisha akianguka? ?

Hii ina maana ccm inatumika mabavu kukufanya udhalilike kwa kusimamisha na kuziwekea ngumu njia zako za kuingia pesa
 
Kuna Watu walitumwa kumsindikiza Lowassa kujivua Gamba wamemfikisha Salama inabidi warejee nyumbani. Hata Zanzibar waliomsindikiza Maalim Seif wamesharejea Nyumbani mf. Nalaila Jidawi, Fatma Maghimbi na Hamad Rashid. Huo ndo utamaduni wa CCM ukiondoka lazima usindikizwe
 
Yuda esikarioti wa Namba moja wa chadema ni Mbowe.

Ipo siku hata Mr zero atarejea bila mkia. Hapo ndio saccos itakufa kabisa
 
Back
Top Bottom