Elections 2010 Mkutano Wa Hadhara Wa Wana-JF [Online]

Mchungaji na WoS mnatoka nje ya mada. Sasa mmenichanganya . . . Aisee, nilifikia wapi tena?

Weka hii Chungaji! Nataka mabadiliko ya Katiba, tuliyo nayo raisi ni kama Mungu Mtu! Madaraka iko mingi sana kwake na kwanini asishitakiwe hebu angalia EPA....
 
sasa nataka kuongea , nanyosha kidole mwenyekiti hunichagui

Kijana wangu Nguvumali ni kweli umenyoosha mkono muda mrefu. Hii yote ni kwa sababu ya WoS na Mchungaji walikuwa wanatumia lugha isiyo ya kistaarabu kwa kwenda nje ya mada.

Sasa ongea tafadhali . . .
 
Weka hii Chungaji! Nataka mabadiliko ya Katiba, tuliyo nayo raisi ni kama Mungu Mtu! Madaraka iko mingi sana kwake na kwanini asishitakiwe hebu angalia EPA....

Very Good. Point taken.

Sasa nakupa kazi . . . watafute wale jinsia nyingine wote waje hapa. Mfumo dume naona umefubaa.
 
Agenda Nyingine, ambayo ni muhimu sana, nikuvifanya vyombo vya Umma, kuwa vya Umma kweli, si mali ya CCM , KIMWENENDO NA KIMTAZAMO.hapa nikuiondoa sekta ya UMMA katika soko la biashara , maana wanapokea kodi zetu, haiwezekani wapigania soko moja na vyombo vya habari binafsi.pia Mkurugenzi wa TBC ateuliwe na Rais ila athibitishwe na chombo huru.
 
Napendekeza:
" AHADI ZA WAGOMBEA: NI KWA VIPI TUTAPIMA UTEKELEZAJI WAKE UKIZINGATIA TUNAPEWA AHADI MPYA KILA SIKU ILHALI ZA ZAMANI HATA HAZIKUMBUKWI?"

( Inanikumbusha wakati nachumbiwa...ahadi kibaooo! ukishaingia ndani...utakoma kuringa!)

WoS mbona zijaona huo mchango wako? Au wa "Kujiandikisha Kupiga Kura"?

Mwenyekiti.... nadhani umeiona hapo juu sasa.Nilipokuwa nachangia ulikuwa unatuma sms!
 
Agenda Nyingine, ambayo ni muhimu sana, nikuvifanya vyombo vya Umma, kuwa vya Umma kweli, si mali ya CCM , KIMWENENDO NA KIMTAZAMO.hapa nikuiondoa sekta ya UMMA katika soko la biashara , maana wanapokea kodi zetu, haiwezekani wapigania soko moja na vyombo vya habari binafsi.pia Mkurugenzi wa TBC ateuliwe na Rais ila athibitishwe na chombo huru.

Nimekupata kijana wangu. Kwa hiyo hoja ni kuwa "Rasilimali za Taifa Zimilikiwe na Umma na Wananchi Wote Wazifaidi"

Pia Uteuzi wa Wakuu wa Mashirika Wathibitishwe na Chombo Huru? Naona hili ni la kikatiba zaidi.
 
Nimekusoma lakini bado sijakupata WoS. Sasa hiyo agenda wataitekeleza vipi kama wataingia madarakani?

Inabidi kuwepo na utaratibu wa kuorodhesha ahadi zote kisha wagombea walioahidi waweke sahihi zao. Kisha tuje tuwabane watakapoingia madarakani! ( Breakthrough thinking lol!)
 
Inabidi kuwepo na utaratibu wa kuorodhesha ahadi zote kisha wagombea walioahidi waweke sahihi zao. Kisha tuje tuwabane watakapoingia madarakani! ( Breakthrough thinking lol!)

Nimekusoma sasa . . . ngoja niiboreshe pointi yako. Unachosema ni kuwa:

"Kuwepo na Chombo Huru Cha Ku-monitor ahadi zote na utekelezaji"? Is that correct?

Wasipotekeleza je?
 
Nimekusoma sasa . . . ngoja niiboreshe pointi yako. Unachosema ni kuwa:

"Kuwepo na Chombo Huru Cha Ku-monitor ahadi zote na utekelezaji"? Is that correct?

Wasipotekeleza je?
Thats correct!
Wasipotekeleza ndio sababu ya kuwaambia wananchi wasiwachague tena.Utaratibu wa sasa usiokuwa na M& E ndio unafanya watu kudanganywa tu bila kuwa na point of reference. Mtu anakuja na khanga na t-shirt na ahadi mpya outrageous..anazingua watu na kujipatia kura kiulani.
 
Back
Top Bottom