Emmanuel J. Buyamba
JF-Expert Member
- May 24, 2013
- 1,167
- 651
Ndg wana JF na watanzania kwa ujumla, leo kutakuwa na mkutano mkubwa sana wa hadhara wa Chadema hapa kahama maeneo ya CDT. Mbunge wa Arusha mjini kamanda mpambanaji Godbless Lema atakuwepo kuwajaza ujasiri watu wa huku. Pia ataambatana na m/kt wa Bavicha taifa kamanda Patrobass K.Paschal.
Kama ilivyoada ya JF iliyojaa wawakilishi kila kona ,itakuwa nawe moja kwa moja toka eneo la mkutano.
Ungana nami Sir. E.J.Buyamba, m/kt wa vijana jimbo la Msalala mkoani Shinyanga nikiwa na makamanda wengine kibao ktk kuhakikisha hakiharibiki kitu.
Karibuni sana!!.
Dodoma lini tunawaitaji na huku mtujaze ujasiri
Shamrashamra zimeanza hapa mkutanoni. Ameanza kuweka sawa watu hapa kamanda Leonard Mayala, diwani wa kata ya Nyasubi.
Anasema serikali yetu ina mawaziri wengi sana wakati uwezo wa kujigharamia ni mdogo. Anatolea mfano wa mtu mwenye duka la laki 6 halafu aweke wauzaji saba kwa wakati mmoja.
Analalamikia pia uwepo wa sikukuu nyingi za kitaifa. Ktk mwaka wenye siku 365,kuna jumla ya siku za wikiendi zaidi ya mia. Ukijumlisha na hizi za may mosi n.k zinafikia karibu mia mbili.
Picha tutawaletea muda si mrefu. Pia wageni rasmi nao wako karibu kufika.