Mkutano wa CHADEMA ubungo msewe leo

Mkutano wa CHADEMA ubungo msewe leo

10365874_822727394447520_8431772296851909305_n.jpg
 
Maji jamani chonde chonde Mnyika Huku mitaa ya Kinzudi Hali ni mbaya sana utawaonea wananchi wako huruma kabisa jinsi anavyohangaika Usiku kucha.

Katika changamoto kubwa uliyonayo ni maji na kwa hili unakazi ya kujibu, barabara za jimbo la Ubungo ni mbovu sana hakuna cha maana kinachoendelea!

mnyika ni dawasco au tanroad???
 
ubungo msewe kuna kijamaa kimoja cha ccm kinaitwa jafari, kila mara anachukua uongozi wa serikali ya mtaa, jamaa anapenda rushwa ni balaa, muongo! kuna makada wa ccm akina mama hatia ni wachawi! yaani msewe ni balaa!
jafari kafanya kama mtaa wa kwake huu mwaka wa 15 kama sikosei,wamekula mamilioni ya tanki la maji eneo la golani,kajenga tanuri la kuchomea takataka zahanati ya msewe kwa mil 7 wakati ni kama banda la mbwa thamani halisi halifiki hata milioni 1,atoke tu
 
Nenda kalalamikie serekali yako ya magamba inayokusanya kodi ...maana magamba wanazuia maji ubungo ili mnyika aonekane hafai...lakini kwa hilo magamba mmeula wa chuya..maana mnyika amelipigia kelele tatozo la maji ubungo. Ila kwa vile magamba yanalitaka jombo la ubungo yanamkwamisha mnyika.

Mkuu hawa magamba tulishawastukia na safari hii inakula kwao.Mnyika na Boniface wamekuwa wakishirikiana na wananchi kudai maji dawasco mara nyingi tu.Mnyika yupo mioyoni mwa wanaubungo,kama walifikiri kukata maji ndo kumkomoa Mnyika imekula kwao,Mnyika ni mwenzetu analia na sisi na anacheka na sisi
 
..ulitaka Mnyika alete maji kwa pesa ipi?,au ajenge barabara kwa fungu lipi?, au aweke polisi kwa ajili ya ulinzi. Ni vyema kufahamu majukumu ya Mbunge, Mnyika ametekeleza majukumu yake kwa ufasaha kabisa. Jitokeze tar 14.,mimi nafanya mazoezi ya kuwatwanga CCM tar 14.

Mkuu usinipe hasira za bure. Kama alijua hivyo ni kwa nini alikuja kutuahidi maji, barabara na usalama.

Kimara zamani ilikuwa eneo linaloheshimika, lakini sasa ukisema unaishi kimara watu wanatoa macho na kukuonea huruma.

Mkuuu kumbuka miaka ya 90 na kuendelea Kimara ilikuwa eneo linaloheshimika lakini sasa ni eneo la wapika gongo, barabara hazipitiki, maji hakuna, ujambazi kila kukicha. Halafu unaleta dhihaka.
 
Mwongo jana maji yametiririka mpaka usiku,hata hivyo spingi kuwa ubungo hakuna uhaba wa maji.Kete ya maji inawabeba UKAWA Kama huamini waulize wagombea wa CCM.

Hayo maji yametiririka wapi mbona sisi hatujayaona?
 
Maji jimbo la Ubungo yanahujumiwa na serikali ya CCM, na kamwe si Mnyika. Wanaubungo ni lazima mjue mchawi wenu ni CCM.
 
Mnyika yupo ubungo anaendelea kusambaza upendo wale wanafiki wa ccm wako wapi .
 
Picha-Mnyika.JPG


Mkutano wa chadema ubungo msewe sasa hivi,yupo mnyika na Tundu Lissu na Mabere Marando watu wametoroka makazini kwao na biashara zimesimama msewe nzima, ila Mnyika kazi anayo kwani maji hayajatoka wiki ya pili sasa
Haya ndio yamefanya Magufuli atumie polisi kuzuia demokrasia
 
Back
Top Bottom