Mungi
JF Gold Member
- Sep 23, 2010
- 16,975
- 9,580
Wakuu,
Mkutano wa kampeni wa chadema sombetini ndiyo umefunguliwa rasmi na Mwenyekiti wa Kata ya Sombetini Kamanda Madava ndiyo amefungua rasmi, lakini amegusia suala la utulivu, kwamba tunaombe tuwe watulivu kwa kipindi hiki cha kampeni, tuwe wapole, wavumilivu, lakini tusiwe wanyonge. Amesema tusimguse wala kumchokoza mtu, lakini tukiguswa tusimwache....
Diwani wa Ngarenaro Doita anawasalimia wananchi, anasema maendeleo yanayoonekana Arusha ni kwasababu ya chadema, wakati hatupo hawakuthubutu, lakini tulipoingia tukikohoa wanafanya..... chezea chadema.
More Updates::
.........................................................................................................................................................................

Mwenyekiti wa Wilaya Diwani wa Levolosi Kamanda Ephata Nanyaro anasema hatuendi kumtafutia Bananga ulaji, na sisi kama chadema siyo waheshimiwa, bali watumishi wa wananchi, na safari hii tumejiandaa kwa namna yoyote na kama ni noma na iwe noma, titahakikisha tunalindana wenyewe...... wamezoea kupiga mabomu kwenye mikutano yetu, wamezoea kuua watu wetu, awamu hii tumejiandaa
Nanyaro anasema tutahakikisha kikao cha bajeti kwenye baraza la halmashauri kabla ya uchaguzi wa sombetini. baada ya bananga kuingia kwenye baraza la madiwani chadema wataongoza kamati zote na maendeleo lazima yaje kwa kasi
Kamanda Alfonce Mawazo anasema ukiitwa mheshimiwa ni title kubwa sana, manake kila kitu chake, na kuanzia leo amemwachia Bananga uheshimiwa. cha pili nimemwachia posho, mimi siyo mheshimiwa tena....... na uheshimiwa huu una maana ya kuwatumikia wananchi wa sombetini, siyo uheshimiwa wa kujiona mkubwa kuliko wengine. jambo la muhimu nakuachia mpenzi wangu wa kweli na wa pekee duniani ambaye ni kata ya Sombetini, na nakuomba umlee vizuri
Mawazo;
pamoja na matatizo yote niliyowahi kupata, nakiri kuwa kama kuna wakati naona kuna raha ni wakati huu wa kupigania ukombozi wa watu maskini.......
Mawazo;
Anaomba msamaha kwa wale waliokwazika kwa yeye kuondoka udiwani, kwamba alipokuwa diwani nilisema mtoto yeyote atakayefukuzwa shule asiende kwa wazazi wake, aje ofisini kwangu, watoto wakawa wanakuja ofisini kwangu, lakini baada ya kuondoka watoto walipofukuzwa walikuta kufuli ofisini kwangu. Anasema kama kuna wakati aliishi maisha magumu ni wakati alipokuwa ccm.... anasema alichukiwa na mpaka mfagiaji wa ccm kwa kusema ukweli....
Mawazo;
Kanda ya ziwa nimeivuruga ccm kote, nimefanya mikutano 400 kwa mwaka katika majimbo 38, na hatafuti utukufu bali kukomboa watu maskini kama mimi ambao wameteswa mateso mengi.....
Katibu wa Kanda ya Kaskazini Kamanda Amani Golugwa anazungumza sana, anasema umati mkubwa namna hii unanipa faraja, kwamba ccm hawana lao tena Sombetini.
Anamwambia Bananga kwamba umati huu hapa unatuambia kwamba Sombetini kumenuka, ccm hali tete....
Golugwa,
CCM walikuwa hawataki sombetini uchaguzi usifanyike, wakati wa uchaguzi wa kata nne Lema alinijia akaniambia tugome kuingia kwenye uchaguzi hadi Sombetini ijumuishwe, wakazingua lakini sasa wameachia na hatimaye wanasombetini wanakwenda kuchagua haki dhidi ya dhuluma........ sombetini ccm wakitoka na kura 10 watafanya sherehe
Golugwa:
Haka kakijana kalikosimamishwa na ccm alikuwa reject kwetu, bahati mbaya kwake amekimbilia tena kwenye nuksi, chadema tunakwenda kushinda siyo kwa ajili ya kutafuta heshima, bali kwenda kusimamia miradi ya wananchi na kuwatumikia kwa haki na ukweli
Godbless Lema,
Anasema wakati anamshawishi Mawazo aje chadema tulikuwa njiro complex, nikamwambia Mawazo uwezo wako ni mkubwa wa kwenda kuwakomboa watu wa kanda ya ziwa. Nikamwambia Mawazo ajivue udiwani, nikirudishiwa ubunge ada ya chuo kikuu nitakumalizia.
Lema,
Bananga anafanya kazi nzuri kwenye chama, amekisaidia chama lindi na mtwara, leo tuna wenyeviti wa serikali za mitaa kule yote ni kwasababu ya kazi ya Bananga.
Lema;
Uchaguzi wa Sombetini, akipigwa moja wetu, tunaacha kampeni, tunakwenda kumsaidia mwenzetu. Hatuwezi kuvumilia upumbavu wowote na hili polisi na usalama wa taifa wasikie
Lema;
Maslahi ya mtu kuwa diwani wa chadema ni kupigania utu wa mtu kwanza.
Polisi wasikie, kwamba kama nitachomwa kisu nikafa, na sababu ya kifo hicho ni kwasababu ya kuwatetea akina mama wanaoteswa na kunyanyaswa, hicho kifo nakitaka sasahivi.
CCM hamtatufanya wajinga tena, wametutesa, wametupuuza sana, na wakileta uhuni, na polisi wakishindwa kuwashughulikia tutawashughulikia wenyewe
Lema,
Nilipokuwa bungeni majuzi nilimwambia Ole Medeye kuwa Kikwete akikurudisha uwaziri utakuwa chizi.
Tumesikia jamaa amempiga chini.
Ole Medeye anahubiri ukabila wakati ameoa mchaga mpuuzi kweli
Lema,
Kesho kutwa tunaanza operations nchi nzima, helcopter tano kwa siku kumi, agenda kuu ni rasimu ya katiba na kupanda kwa gharama za umeme na gesi. Kazi ya sombetini tunawaachia BAVICHA wakapambane na hawa ndondocha
Bananga,
Anampandisha mama yake jukwaani, anamfananisha na wamama wengine wa sombetini waliochoka. Nawaahidi watu wangu wa Sombetini kama familia moja, na wazee wangu wa Sombetini ni wazee wangu wote.
Anamwahidi Mawazo kuwa mpenzi wake nimempenda, na nitamlea kwa dhati, na kwamba mimi siyo boya, na wala siyo faala, kwa ishu ya maji nitalala kwenye ofisi ya mbunge mpaka nipate maji
Nassary;
Kama mnavyotuona hatujavaa suti kwasababu chadema hatugawi vyeo.
Mkoa wa Arusha umekuwa icon ya mabadiliko kwenye taifa la Tanzania. CCM wamemsimamisha mtoto wa kiongozi hapa kuwa mgombea, na kule Arumeru mnakumbuka ccm walimsimamisha mtoto wa kigogo aliyeoa mtoto wa kigogo, watu wa Arumeru wakawaambia ccm kuwa utawala wa kifalme hauna nafasi kwetu. Ndugu zangu nawaambia ccm wakipata kura 30% Sombetini na Bananga kashinda kwa 70% itakuwa ni aibu kubwa sana..... Ndugu zangu mnapomchagua diwani wa chadema maana yake ni mmechoka kunyanyaswa na ccm, mmechoka na utawala mbovu wa ccm.