Mkutano wa CHADEMA Kasulu mjini wafanyika, lakini...

Ziara za Dr. Slaa huko Kahama na Kigoma ziliwahishwa sana. Wangesubiri mpaka maamuzi ya hatima ya hao walioambiwa wajieleze...
Kwa kweli hiyo ndo ingekuwa hekima. Hapakuwa na sababu yoyote wakati hatujasikia upande wa watuhumiwa wakijieleza. Mi naona huku ni kujaribu kumfrustrate zzk; uchokozi tu!
 
........mbona hayo mabango yanaonekana kabisa yameandikwa na mtu mmoja na yametoka sehemu moja,angalia UANDISHI WAKE pia angalia AINA YA KARATASI na WINO ULIOTUMIKA vyote vimefanana....inaonyesha ni jinsi gani waliopanga hili jambo hawako makini na wamekurupuka..
 
Habari kama hizi habari hazina uhakika kabisa. Maccm wako kwa gharama yoyote kukwamisha ziara ya Dr Slaa kigoma sijui faida yake Ni nini?? Ila moderators huyu aloleta hii post ya kizushi NA una kizandiki kwanini msimle burn ya milele?
 
kila mtu atavuna alichopanda-SLAA kaanzisha chuki ndani ya chama akisahau ile kanuni ya Newton-ACTION and REACTION are equal but in opposite DIRECTION-sasa ajue na yeye aonje joto la jiwe-afadhali mtoto wa ZZK ni mkubwa, SLAA mtoto wake kwa MSHUMBUSI ndo kwanza anatambaa anataka kutuachia yatima huyu mzee
 
Kwani Chadema wakiandamana huwa wanatumiwa na nani?
Vyovyote itakavyokuwa, kama wewe unamfahamu ambaye huwa anawatuma basi tutajie. Lakini baada ya siku 14 Zitto afukuzwe kabisa uanachama. Nina uhakika kabisa hawa waleta fujo hawana hata kadi ya uanachama wa CHADEMA.
 
mbona mabango yote yameandikwa na mtu mmoja????????????????????????????
 
........mbona hayo mabango yanaonekana kabisa yameandikwa na mtu mmoja na yametoka sehemu moja,angalia UANDISHI WAKE pia angalia AINA YA KARATASI na WINO ULIOTUMIKA vyote vimefanana....inaonyesha ni jinsi gani waliopanga hili jambo hawako makini na wamekurupuka..
 
Good news, baada ya kutekeleza mpango huu, hawana tena nguvu za kuendelea, they are on the run.
Go DR go.
 
Slaa(CHADEMA) ni kioo cha mageuzi na wala siyo shina la mageuzi hivyo kumdhuru hakuondoi moyo(spirit)wa mageuzi
 
Mabasi mawili yalifika kwenye mkutano vijana kama kumi na tano wakashuka na kuanza kurusha mawe kwenye mkutano, Polisi wakaanza kurusha mabomu ya machozi na wamefanikiwa kuwakamata baadhi....
 
Hii ni aibu ya Zitto, kwa hizi vurugu naamini kamati kuu walikua sahihi kumtosa zitto.!!
 
MABANGO YANASOMEKA HIVI
mtei-baba mwenye nyumba.
Mbowe -mtoto wa mwenye nyumba.
Slaa-mpangaji.
Lissu-mchumia tumbo.
Lema-mibangi.

2.bango lingine limeandikwa.
Dr kabur???, zitto kabwe???,chacha wangwe?? Siasa za ubaguzi na ukanda zitakiua chama.
 
Wabeba mabango wana hoja inayostahili kujibiwa...
hoja gani? Labda onyesha tu kwamba upo tofauti kidogo na hao wabeba mabango kwa kututajia hoja inayostahili kujibiwa hapo. Hivi unafikiri watu wote ni wambea kama ninyi?
 
mbona muda wa mkutano kufanika umekwisha tayari au umeendelea mpaka usiku?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…