Mkutano wa CHADEMA Kasulu mjini wafanyika, lakini...

Mkutano wa CHADEMA Kasulu mjini wafanyika, lakini...

Mm nawambia hv mtu si maarufu maarufu ni chama huyo kama mnampenda mwambie anzishe chama na mukamuunge mkono huko
 
viongozi mbalimbali wa CHADEMA wakiwamo Shaban Mambo Mwenyekiti wa chadema Kanda ya magharibi na Rajabu Bujoro Mwenyekiti wa Kasulu wamefungua mkutano hali ikiwa shwari watu wa Kasulu wakionesha ustaarabu wa hali ya juu. Lakini kufumba na kufumbua alipopanda jukwaani Dr Slaa Katibu mkuu wa CHADEMA Taifa kikundi cha watu kiliibuka na mabango mbalimbali huku wakitamka kwa jazba maneno mbalimbali ya kumtaka Zitto na kukejeli upngozi wa juu wa CHADEMA.

Katibu Mkuu ameonesha ustaarabu na demokrasia iliyokomaa alipo ruhusu mabango yasogezwe mbele na kuwataka askari polisi wasiwachukulie hatua wenye mabango. Pia aliwauliza wanakasulu ni wangapi wanataka mkutano uendelee wengi wamenyoosha mikono kutaka mkutano uendelee. Hali si salama sana na nimeacha mpaka naingia mitamboni polisi wanatafuta mbinu mbadala za kuimarisha ulinzi na kuongeza kikosi.

======================
Habari Zaidi
======================



===========================
Kwa Mujibu wa Kurugenzi ya Habari
==========================
Baada ya cc ya cdm kumuhukumu zitto kwa kumzushia fitna kama baraza la wazee wa kiyahudi walivyo mkatia yesu hukumu ya kifo kwa fitna mnategemea nini kutoka kigoma.
 
kp05122013.jpg
 
Nadhani hao vijana hawajui wanachokifanya. Wanamtumikia nani? kwa faida gani? Je, Ujira wa siku moja tu?
 
Nimeangalia taswira ya mkutano kabla ya kund la wahuni kuvamia mkutano

wananch,walikuwa tayar kwa ajil ya mkutano

hizi vurugu haztarudsha harakat nyuma
 
Badala ya kupambana na changamoto za matatizo ya wananchi kwa sasa wanapambana na ubinafsi wao kwa wao.

Wanataka kutoana macho kwa sababu ya ruzuku na posho mbali mbali za kibunge mpaka wameanza kuangaliana kwa ukabila, ukanda na udini.

Hivi vyama vya siasa vya upinzani ni hasara kubwa na mzigo mkubwa kwa wananchi masikini walipa kodi.
 
NAYE KIHEREHERE KAMA WALE VIJANA ALIOWATAJA MKUU. Hutakiwi unalazimisha penzi?
 
Ujumbe umemfikia Dr.slaa. Huu ni uchochezi kabisa, alitaka aaatuaminiahe kwamba Zitto is no body kule kigoma. sasa umeelewa who is Zitto!

Fanyieni kazi ujumbe huo wa mawe kwa maslahi mapana ya chama na wananchi na sio wanauchu
 
Kigoma subirini ZZK hafukuzwe uanachama kabisa then mmhamie Burundi na Kongo kwa wenye fujo wenzenu

Yale yanayotokea Arusha mara kwa mara mpaka hata mnavamia vituo vya Polisi sio fujo? nyani haoni ku..... huona la mwenzake!!!
 
Badala ya kupambana na changamoto za matatizo ya wananchi kwa sasa wanapambana na ubinafsi wao kwa wao.

Wanataka kutoana macho kwa sababu ya ruzuku na posho mbali mbali za kibunge mpaka wameanza kuangaliana kwa ukabila, ukanda na udini.


Hivi vyama vya siasa vya upinzani ni hasara kubwa na mzigo mkubwa kwa wananchi masikini walipa kodi.

Sio chama cha Wananchi!!!
 
Maccm akili imewaishia kweli nyie ndo wale ambao nyerere alisema mkiona hawa muwakatae
Mmeishiwa sera hadi mnafanya vituko hivyo?
Hata kama mnamuhitaji zitto wenu kwa nini msimchukue kwa amani badala ya shari?
mafisadi nyie wauza unga migodi mnabadilishana na vyandarua na suti
Tz tusipokubali ukweli tutakuwa maskini wa kutupwa
Wakenya wameshajitambua wanyaruanda n.k
Sisi tumebakia hoe hai
ivi mtu kwa nini usijiulize maswali mazuri tuu
Kwa nini umwone mtanzania mwenzako anapata shida kunyanyasika na wewe unafurahia?
Wewe unapewa book 7 kwa sababu ya kuisifia ccm ila wenzako wanakufa watz wenzako wanakatishwa maisha kwa sababu ya kukosa huduma muhimu

Post yako inachosa kusomaaaaaa,tunataka min KABANG tu hapa,
 
Sio chama cha Wananchi!!!
Ujumbe wako sina budi kuukubali kwa sababu migogoro inayotokea chanzo chake ni pesa.

Mungu aliwaangazia wananchi 2010 na kuwaambia wasiwape nchi hawa mbwa mwitu walikuwa wanavaa ngozi ya kondoo wakati wakiomba kura.

Thanks God kwa kulipenda Taifa letu na sisi hatutachoka kuwaelimisha wale waliolaghaika na wafanyabiashara kupitia siasa.

Tuwaache wafu wazikane!
 
viongozi mbalimbali wa CHADEMA wakiwamo Shaban Mambo Mwenyekiti wa chadema Kanda ya magharibi na Rajabu Bujoro Mwenyekiti wa Kasulu wamefungua mkutano hali ikiwa shwari watu wa Kasulu wakionesha ustaarabu wa hali ya juu. Lakini kufumba na kufumbua alipopanda jukwaani Dr Slaa Katibu mkuu wa CHADEMA Taifa kikundi cha watu kiliibuka na mabango mbalimbali huku wakitamka kwa jazba maneno mbalimbali ya kumtaka Zitto na kukejeli upngozi wa juu wa CHADEMA.

Katibu Mkuu ameonesha ustaarabu na demokrasia iliyokomaa alipo ruhusu mabango yasogezwe mbele na kuwataka askari polisi wasiwachukulie hatua wenye mabango. Pia aliwauliza wanakasulu ni wangapi wanataka mkutano uendelee wengi wamenyoosha mikono kutaka mkutano uendelee. Hali si salama sana na nimeacha mpaka naingia mitamboni polisi wanatafuta mbinu mbadala za kuimarisha ulinzi na kuongeza kikosi.

======================
Habari Zaidi
======================



===========================
Kwa Mujibu wa Kurugenzi ya Habari
==========================

chama changu cha CHADEMA kimefanya makosa kufanya ziara kigoma,,,kilitakiwa kwanza kiwape muda uongozi wa mkoa kutoa elimu kwa wanaCHAMA juu ya ukuu wa katiba wa chama.


Kiukweli chama chetu kina mashabiki wa watu kuliko hata wanaCHAMA, ukitaka kuligundua hilo humu JF kuna watu wanapinga kila kitu juu ya ZITTO hata kama hicho kitu kina faida kwa chama,,,kwakuwa hao watu si mashabiki wa Zitto ndio maana wanapinga kila kitu cha Zitto.


Pia kuna watu wanaunga mkono kila kitu juu ya Dr.Slaa hata kama hicho kitu Dr anakosea. Kwa mfano kuna watu walikuwa wanaunga mkono na kutetea kitendo cha Dr kusema katiba ya CHADEMA haikuwahi kuwa na kipengere cha ukomo ili hali hicho kipengere kiliwahi kuwepo kwenye katiba yetu. Ushabiki watu juu ya Dr. Wakajikuta wanatetea tu bila kuzingatia kosa la Dr.


Kwahivyo hata kwa viongozi wa makao makuu ni watu wa kuabudu watu badala ya misingi ya chama, je tutegemee nini kwa ngazi za chini kabisa?? Niliwahi kusema midhali uongoz wa mkoa umeona shaka ni vema upewe muda wa kuwafunda wanachama wake, lakini kwa ubishi wa makao makuu imekuwa dhahiri sasa haikuwa ziara ya chama bali ilikuwa ni ziara ya kuvunja kambi ya Zitto, kama ilikuwa ziara ya chama kulikuwa hakuna haja ya kufanya ziara hiyo ikiwa kuna taarifa hali si shwari. Njia nzuri ya kuvunja hiyo kambi ilikuwa ni kwa Dr. Slaa kufanya mikutano ya ndani kwa ngazi ya kila jimbo,,kisha angewaachia kazi viongoz wa jimbo kusema na wanachama wao. Hii ingekuwa njia nzuri na wanachama wangeelewa tu kwasababu wangekuwa wanafundishwa na watu wa kwao ambao kimsingi wasingetaraji kuhujumiwa toka kwao.


Njano5.
 
Hawa watu sio wapenzi wa Zitto. Ni vijana wa CCM, basi. Kwani mimi nikienda sehemu yoyote nikachora mabango yanayofanana, mwandiko na kila kitu, na nikawapa watu elfu tano, unadhani ntakosa watu wa kubeba? Kama Zitto alinunuliwa, itakuwaje wafuasi wake?
Mtaji wa CCM ni umaskini wa watu na ujinga. Ndo maana wanatafuta div 5 hili watu waendelee kuwa watumwa kwenye taifa lao.
Watanzania, keep pushing until we get the results we deserve. Hawa matapeli, watoa rushwa, wala rushwa, wezi, wauaji hawaitakii mema nchi yetu. Hatuwezi tena miaka 50 ya giza.

Mugo"The Great";8038449 said:
Kalinzi acha kudanganya watu, mimi mwenyewe ni mkazi wa Matyazo na nilibahatika kutembelea Nyarubanda, Mkongoro, Kalinzi sokoni na maeneo mengine, Watu wapo tayari kusikiliza hoja za pande zote mbili. Na muda mfupi nimeongea na ndugu yangu aliyepo Mwiranvya Kasulu na amenihakikishia kuwa watu walikuja kwa wingi kumsikiliza Dr. Slaa isipokuwa kuna watu wachache walioletwa na magari ndio walileta fujo. Hii inaonyesha kuwa kuna mtu ambaye ame-organize fujo hizi. Ni kweli Zitto alianza vizuri sana lakini baada ya Buzwagi, mafisadi walifanikiwa kumpata baada ya Zitto kumeza ndoano. Taabu kubwa ninayoipata ni wewe kuwaaminisha watu kuwa wana-Kigoma wanawapiga vita wachaga, huo ni Uongo na Ukabila.Vilevile si kweli kuwa Zitto ndiyo kila kitu. Kigoma tunao vijana wengi sana ambao wata-take over from Zitto. Tulimkabidhi kijiti aongoze mbio za kujikomboa, kijiti hicho ameamua kuwakibidhi CCM. CCM wanajaribu kuigawanya nchi vipande vipaned through ukabila na udini ili waendelee kutawala, lakini Watanzania siyo wadanganyika tena hivyo wameshtuka. Bulocha mwenewachu.
 
Ujumbe wako sina budi kuukubali kwa sababu migogoro inayotokea chanzo chake ni pesa.

Mungu aliwaangazia wananchi 2010 na kuwaambia wasiwape nchi hawa mbwa mwitu walikuwa wanavaa ngozi ya kondoo wakati wakiomba kura.

Thanks God kwa kulipenda Taifa letu na sisi hatutachoka kuwaelimisha wale waliolaghaika na wafanyabiashara kupitia siasa.

Tuwaache wafu wazikane!

ebu tumia ubongo kufikiri! kwani rushwa inayotembezwa majimboni kuhadaa watu ndo kufunuliwa na Mungu?
 
Nimeamini sasa, mtaju wa ccm ni umaskini! hasa wa kipato na fikra,
kwenda na mabango kwenye mikutano ni jambo la kawaida, wangesikiliza agenda/hoja za mikutano then wakatafakari na kuzichambua! sasa vurugu ni za nini?
 
Back
Top Bottom