Mkutano wa CCM Tegeta na uongo wa hadharani dhidi ya CHADEMA

Mkutano wa CCM Tegeta na uongo wa hadharani dhidi ya CHADEMA

yaani anaongea pumba na bado mnamshangilia! Na nyie mliokuwa mkutanoni ni wauongo wala sio wa ukweli, kuanzia waongeaji mpaka wasikilizaji wote sio!
 
Huyu mwigulu sianakaa tegeta-dawasa naalikuwa anawaleta ndugu zake pale boko-basihaya kutibiwa lakini alivyo chaguliwa kwenye sekretalieti ya ccm haji tena kutibiwa kwenye zahanati anatibiwa kwenye hospitali za kifisadi,unajua anaona aibu kukaa kwenye jimbo lililochini ya chadema kawe hivyo haishi kufanya mikutano tegeta lakini atambue vijana kawe tumejipanga siyo rahisi kuwadanganyi watu wa kawe na vipropaganda vyake sisi tunataka umeme,maji na bidhaa hasa vyakula kushuka bei mambo ya slaa sijui kaoa mke wa mtu, sijui padre haituhusu haitupunguzi ugumu wa maisha tunatamajibu wa maswali yaha..
 
Sijaua ulishangaa kitu gani mkuu mtoa mada kana kwamba wewe umezaliwa jana. Hv tangu lini Magamba wameacha kusema uongo mbona tunajua hawa ni waongo na ndio maana kila wanapokwenda wanataka tuendelee kuwasikiliza na kama hutaki kudanganyika basi unaitwa UPINZANI. Nini kilikuponza kwenda kuwasikiliza hawa watu ambao wana ma roho ya kudanganya hata bungeni kwani juzi hukusikia Ngeleja akidanganya kwamba kuna sehemu nguzo zimepelekwa wakati hazipo na akawa bubu kujibu? Unategemea nini wasomi wanapogeuka kuwa watu wa FIX
 
Jamani
Muambieni Mwigulu aache kuendelea kusambaza huo uongo wa kusomesha watu.
wakati wa kampeni alidai anasomesha watoto yatima, wana ilamba sasa wameishachoka
wanatafuta hao yatima ni wepi? na anawasomesha shule ipi? sasa kaja na hili la kusomesha
wanafunzi wa A-Level, anafikiri siasa za kuongea ongea zinalipa sio
 
Wakuu leo nilihudhuria katika mkutano wa CCM uliofanyika Mkoa wa Dar, Wilaya ya Kinondoni, Jimbo la Kawe, hapo Tegeta Sokoni. Mgeni rasmi mwanzoni baadhi yetu tuliambiwa ni W. Mkama (tulidanganywa? Ili kujaza watu?) kumbe alikuwa ni Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha, Mwigulu Lameck Mwichemba. Huyu bwana pia ni mbunge wa Iramba Magharibi nafikiri kama sijakosea. Leo ndo nimesikia kumbe alikuwa mfanyakazi wa Benki Kuu (BoT) (???????), kabla hajaenda kugombea na kuukwaa ubunge na ukatibu huo wa NEC.

Nilikuwa na siku nyingi kidogo, du! Watoto bado wanatumikishwa, wamevalishwa maskini nguo haziwaenei. Kubwa si kubwa, ndogo si ndogo. Wamekalilishwa na kulishwa maneno! Walipomaliza kuimba, jamaa Mwigulu nikaona kampatia mmoja wao, kiongozi sijui, shilingi elfu kumi kadhaa hivi mkononi, akiwa amezifunga funga! Posho ya siku kwa kukaa juani masaa kadhaa! Maneno kama wakereketwa sijayasikia kitambo, leo nikayasikia. Nisiwachoshe, msinichoshe pia!

Katika upupu aliomwaga huyo jamaa, (maana yeye na Shigela walitumia sana nafasi hiyo kuwananga wapinzani, hasa CHADEMA, Mbunge Halima Mdee, Dkt. W.P Slaa na Freeman Mbowe) huu ulivuka mipaka ya vijembe vya kisiasa bali ulikuwa ni uongo uliokubuhu. Halafu jamaa hata aibu hana kabisa. Hoja za Jamaa na Shigela zinasema hivi;

1. Dkt. Slaa alifukuzwa upadri kwa sababu alimpatia mimba sister mmoja. Hana analojua, maana ni Dokta wa Sheria za Kanisa, akisisitiza neno Padri, kwa makusudi wanayoyajua wao Chama Cha Magamba. Hata kazi hiyo aliyoisomea na kupata udaktari wa sheria za kanisa bado hakuweza kufanya kazi muda mrefu, maana alifukuzwa punde tu alipoanza kufanya kazi! Wakuu du!

2.Juzi wakati akichangia bungeni Freeman Mbowe atakuwa alikuwa amepandwa na Malaria, maana alisema kuwa ukosefu wa maji uliosababisha ukosefu wa umeme si janga la asili. Kwa hiyo si kiongozi wa kuaminika wala kusikilizwa maana uelewa wke ni mdogo hata hajui kuwa kukosekana kwa mvua/ maji ni janga linalotokana na asili, nje ya uwezo wa binaamu.

(Jamani kwa wale tuliomsikiliza kwa makini juzi Mkuu wa Kambi yetu rasmi ya Upinzani bungeni alipiga nondo za uhakika. Mbowe alisema serikali isiseme wala kusingizia kuwa matatizo ya umeme ni janga (si maji, aki-refer kauli ya Ngeleja kuwa umeme ni janga la taifa sasa), kwa sababu majanga husababishwa na natural calamities, nje ya uwezo wa binadamu, lakini matatizo ya umeme nchini yamesababishwa na binadamu ambayo ni matokeo ya uongozi mbovu), jamaa bila aibu akabadili, du! Nikaona watu wenye mavazi ya kijani na weusi wakishangilia. Wakaitikia sema baba ukweli! Nikasikitika.

3. Halima Mdee hana muda na wananchi wake, kwa sababu muda wote yuko katika maandamano. Hawezi kuwaletea maendeleo, wala kuwanunulia hata pipi. Hana uwezo wa kujenga hata uchochoro kwa sababu inabidi akaombe msaada serikali ya CCM.

4. CDM hawafanyi maandamano 'kwao', ndiyo maana huwezi kusikia maandamano Karatu wala Kilimanjaro kwa akina Mbowe kwa sababu wenzenu hawataki hata kuona risasi zikigusa migomba na kahawa zao, wanaletea ninyi huku, mnapigwa tu risasi.

5. CDM wanafuja fedha za wananchi kufanya maandamano. Akina Lema na Mdee na wengine badala ya kupeleka maendeleo, kucha wanazungumza mambo yasiyokuwa na maana hata bungeni. 'Nimewauliza Arusha kama wameletewa hata pipi, hakuna, wakati kwangu mimi Iramba nimepeleka mifuko ya sementi, nimesomesha wanafunzi wote waliokwenda form five, nimelpia ada wanafunzi na nimepeleka madawati, ninyi hapa mmepata nini, huko sasa wananiiita Baba wa Taifa wa Iramba.'.

Zilikuwepo hoja nyingi za uongo wa wazi na vijembe vya hovyo kbs kufanywa na mwanasiasa wa level ya washikaji kama Shigela na Mwigulu. Nitazidi kuziweka kadri mjadala utakavyokwenda!
Turudishieni hela mlizokwapua EPA(BOT), turudishieni hela mlizokwapua kupitia RICHMOND na DOWANS wake, MEREMETA, RADAR
Wanyama mlioiba hai jana kutoka mbugani mwetu.
Hivi jamani waliulizeni swali hili "maana ya kuvua gamba nini?" Ni kukimbia na hela ulizokwapua uraiani au ni kushtakiwa na kurudisha zote baada ya kufungwa" Kuvua gamba ni falsafa iliyobuniwa na mafisadi kukimbia na haki zetu walizopora! baada ya kuwashtukia. HATUKUBALI
Waambieni hatutaki matusi tunataka haki zetu zilizoibwa kwa namna mbalimbali.
 
Kabla kusoma habari hii. naona ni google jina hili nione wasifu wake Mwigulu Lameck Mwichemba. kama ni kweli kama ilivyobainishwa na mtoa habari.
 
Nadhani hao watu wa Arusha aliowahoji walimjibu vizuri! Ni kweli kabisa kwamba mbunge wetu hajatuletea pipi. Na hii ni kwasababu hatukumchagua ili akatuletee pipi. Tulimchagua atuletee maendeleo. Kama watu wa iramba walimchagua awapelekee pipi huku Arusha ni tofauti kabisa. Na mbunge wetu akituletea pipi tutampiga mawe!
 
Nadhani hao watu wa Arusha aliowahoji walimjibu vizuri! Ni kweli kabisa kwamba mbunge wetu hajatuletea pipi. Na hii ni kwasababu hatukumchagua ili akatuletee pipi. Tulimchagua atuletee maendeleo. Kama watu wa iramba walimchagua awapelekee pipi huku Arusha ni tofauti kabisa. Na mbunge wetu akituletea pipi tutampiga mawe!
Thank you for this useful post.
 
kweli ukijiunga na chama cha magamba unabadilika na kuwa kilaza! huyu jamaa( MWIGULU) tulipokuwa mazengo sec alikuwa nondo vibaya.amekuwa kilaza kabisaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Magamba wapo kwenye koma, sio rahisi kutambua uwezo wa wananchi wa kufikiri, kuchambua na kuchuja mambo ndio maana wao magamba bado wako kwenye siasa za uongo na majungu ambayo kwa hakika hayamsaidii mwananchi wa kawaida.

Namshukuru Mungu kwa magamba kuwa katika hiyo hali, inarahisisha safari ya ukombozi wa kweli
 
Back
Top Bottom