Mkutano wa CCM Tegeta na uongo wa hadharani dhidi ya CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkutano wa CCM Tegeta na uongo wa hadharani dhidi ya CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Chief Isike, Jul 17, 2011.

 1. Chief Isike

  Chief Isike JF-Expert Member

  #1
  Jul 17, 2011
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 445
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wakuu leo nilihudhuria katika mkutano wa CCM uliofanyika Mkoa wa Dar, Wilaya ya Kinondoni, Jimbo la Kawe, hapo Tegeta Sokoni. Mgeni rasmi mwanzoni baadhi yetu tuliambiwa ni W. Mkama (tulidanganywa? Ili kujaza watu?) kumbe alikuwa ni Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha, Mwigulu Lameck Mwichemba. Huyu bwana pia ni mbunge wa Iramba Magharibi nafikiri kama sijakosea. Leo ndo nimesikia kumbe alikuwa mfanyakazi wa Benki Kuu (BoT) (???????), kabla hajaenda kugombea na kuukwaa ubunge na ukatibu huo wa NEC.

  Nilikuwa na siku nyingi kidogo, du! Watoto bado wanatumikishwa, wamevalishwa maskini nguo haziwaenei. Kubwa si kubwa, ndogo si ndogo. Wamekalilishwa na kulishwa maneno! Walipomaliza kuimba, jamaa Mwigulu nikaona kampatia mmoja wao, kiongozi sijui, shilingi elfu kumi kadhaa hivi mkononi, akiwa amezifunga funga! Posho ya siku kwa kukaa juani masaa kadhaa! Maneno kama wakereketwa sijayasikia kitambo, leo nikayasikia. Nisiwachoshe, msinichoshe pia!

  Katika upupu aliomwaga huyo jamaa, (maana yeye na Shigela walitumia sana nafasi hiyo kuwananga wapinzani, hasa CHADEMA, Mbunge Halima Mdee, Dkt. W.P Slaa na Freeman Mbowe) huu ulivuka mipaka ya vijembe vya kisiasa bali ulikuwa ni uongo uliokubuhu. Halafu jamaa hata aibu hana kabisa. Hoja za Jamaa na Shigela zinasema hivi;

  1. Dkt. Slaa alifukuzwa upadri kwa sababu alimpatia mimba sister mmoja. Hana analojua, maana ni Dokta wa Sheria za Kanisa, akisisitiza neno Padri, kwa makusudi wanayoyajua wao Chama Cha Magamba. Hata kazi hiyo aliyoisomea na kupata udaktari wa sheria za kanisa bado hakuweza kufanya kazi muda mrefu, maana alifukuzwa punde tu alipoanza kufanya kazi! Wakuu du!

  2.Juzi wakati akichangia bungeni Freeman Mbowe atakuwa alikuwa amepandwa na Malaria, maana alisema kuwa ukosefu wa maji uliosababisha ukosefu wa umeme si janga la asili. Kwa hiyo si kiongozi wa kuaminika wala kusikilizwa maana uelewa wke ni mdogo hata hajui kuwa kukosekana kwa mvua/ maji ni janga linalotokana na asili, nje ya uwezo wa binaamu.

  (Jamani kwa wale tuliomsikiliza kwa makini juzi Mkuu wa Kambi yetu rasmi ya Upinzani bungeni alipiga nondo za uhakika. Mbowe alisema serikali isiseme wala kusingizia kuwa matatizo ya umeme ni janga (si maji, aki-refer kauli ya Ngeleja kuwa umeme ni janga la taifa sasa), kwa sababu majanga husababishwa na natural calamities, nje ya uwezo wa binadamu, lakini matatizo ya umeme nchini yamesababishwa na binadamu ambayo ni matokeo ya uongozi mbovu), jamaa bila aibu akabadili, du! Nikaona watu wenye mavazi ya kijani na weusi wakishangilia. Wakaitikia sema baba ukweli! Nikasikitika.

  3. Halima Mdee hana muda na wananchi wake, kwa sababu muda wote yuko katika maandamano. Hawezi kuwaletea maendeleo, wala kuwanunulia hata pipi. Hana uwezo wa kujenga hata uchochoro kwa sababu inabidi akaombe msaada serikali ya CCM.

  4. CDM hawafanyi maandamano 'kwao', ndiyo maana huwezi kusikia maandamano Karatu wala Kilimanjaro kwa akina Mbowe kwa sababu wenzenu hawataki hata kuona risasi zikigusa migomba na kahawa zao, wanaletea ninyi huku, mnapigwa tu risasi.

  5. CDM wanafuja fedha za wananchi kufanya maandamano. Akina Lema na Mdee na wengine badala ya kupeleka maendeleo, kucha wanazungumza mambo yasiyokuwa na maana hata bungeni. 'Nimewauliza Arusha kama wameletewa hata pipi, hakuna, wakati kwangu mimi Iramba nimepeleka mifuko ya sementi, nimesomesha wanafunzi wote waliokwenda form five, nimelpia ada wanafunzi na nimepeleka madawati, ninyi hapa mmepata nini, huko sasa wananiiita Baba wa Taifa wa Iramba.'.

  Zilikuwepo hoja nyingi za uongo wa wazi na vijembe vya hovyo kbs kufanywa na mwanasiasa wa level ya washikaji kama Shigela na Mwigulu. Nitazidi kuziweka kadri mjadala utakavyokwenda!
   
 2. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #2
  Jul 17, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,784
  Likes Received: 2,393
  Trophy Points: 280
  hakuna wilaya masikini tanzania kimaendeleo kama iramba,kule bado wananchi wanaishi ktk nyumba za udongo juu na chini-tembe nani anabisha?aeleze pia hizo risasi zinatoka wapi?
   
 3. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #3
  Jul 17, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Hayo ni makelele ya mavuvuzela hayaizuii CDM kufunga magoli! Peopleeeeee's Poweeeeeer!
   
 4. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #4
  Jul 17, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Madai hayo yaa hao jamaa hata MS anaweza kuwa point kuliko wao .Hakika hao majamaa nij majuha wanaweza kweli kusimama na kudai hayo mbele ya wananchi dhidi ya Slaa ? Kweli Slaa moto mkali nimeamini sasa .Haya waache tuone .
   
 5. s

  sem2708 JF-Expert Member

  #5
  Jul 17, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 3,093
  Likes Received: 505
  Trophy Points: 280
  Huyu mwigulu mbona anapenda sana tegeta? Ths isnt the first time kwenda kudhihirisha upeo wake hapo tegeta.kaka nenda kwako iramba..I thought you are a 'substance' but i was wrong or else you are in the wrong venue,siamini kuwa kile kichwa nkijuacho toka ilboru hadi udsm ndo kimetema hizo pumba,naamini umepotea njia.i am disappointed!
   
 6. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #6
  Jul 17, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Mpuuzi tu huyu
   
 7. chipanga

  chipanga JF-Expert Member

  #7
  Jul 17, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 661
  Likes Received: 141
  Trophy Points: 60
  Yule Chambili na yule mbunge wa Tarime ...yule mwenye genge la kuuza wali pale bandarini... siku ile pale clouds si walisema mbunge akitaka kwenda kwenye jimbo la mwanzake inabidi amuombe ruhusa kwanza mwenye jimbo lake, sasa yeye vipi, alimuomba Mdee ruhusa?
   
 8. G

  Giddy Mangi JF-Expert Member

  #8
  Jul 17, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 833
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ana bahati sana nilichelewa kufika Tegeta kwa sababu ya Foleni angenikoma Mse§§§§ mkubwa huyu ajui tumechosha na maneno yao kwani nchi imewashinda.
   
 9. m

  mndeme JF-Expert Member

  #9
  Jul 17, 2011
  Joined: Sep 2, 2008
  Messages: 322
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  mwigulu hafikirii kitu kingine zaid ya siasa chafu, amekalia kuvaa skafu za ccm hana hoja huyu
   
 10. z

  zamlock JF-Expert Member

  #10
  Jul 17, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  huyu bwana nimemsikia leo na uongo wake wa wazi wazi na amefanya makosa sana kuzungumzia maswala ya mtu binafsi na imani yake ila nampa pole sana kwa sababu ajajua watanzania wanataka nini mpaka saizi na kingine ambacho kimewakqaza wanamagamba wenzake ni mgao wa pikipiki kwa waislamu pekee kitu ambacho watu wengi wamehoji kwa nini hizo pikipiki ziende kwa waislamu pekee yao kwani akuna qakristo ambao ni vijana pia nawanapaswa kugawiwa hizo pikipiki? Kwa kweli wameni
   
 11. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #11
  Jul 17, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,875
  Likes Received: 1,561
  Trophy Points: 280
  ndugu unashangaa nn? Ukshakuwa sisiemu tu lazma akili zako ziwe "left hand" it doesn't umesoma ilboru, udsm au Havardg.
   
 12. c

  chief m Member

  #12
  Jul 17, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyo bwana sio wa kupuuza, nilikwepo pale, anauwezo wa kujenga hoja, atakayesema nimzaha hatendei haki jf na mwishoni nilibaki kwenye vikundi watu walikuwa wanashabikia maneno yake, niliwasikia wakisema laiti huyu angekuwa mbunge wetu, na mwingine alisema kumbe ccm bado inaviongozi wanaojali watu, na mwingine alisema huyu jamaa amenigusa sana. Mimi nadhani cdm tufuatilie na ikiwezekana viongoz wakasafishe
   
 13. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #13
  Jul 17, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,971
  Likes Received: 6,601
  Trophy Points: 280
  kumbe leo wapinzani walikuwa katka jimbo la kawe! sikujua.naona upinzani wameuanza mapema kabla ya 2015
   
 14. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #14
  Jul 18, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Pole sana Mkuu 2MINE; umekosea kitu kimoja tu! Huyo Bwana siyo Mbunge na wala hakugombea ubunge, kwahiyo kama hiyo pia ni taarifa mliyopewa hapo basi kila habari ilikuwa ya uongo kuanzia mgeni wenu Mkama, maneno juu ya Slaa na hata wasifu wa huyo Bwana.

  By the way CCM inapambana na Slaa au CDM?!
   
 15. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #15
  Jul 18, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Hakuna hoja hapo
   
 16. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #16
  Jul 18, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Lakini hii ni dhasna mbovu inayoendeshwa na serikali yetu. Inaonyesha miradi ya maendeleo haitapelekwa kwenye majimbo yenye wapinzani ili kuwarubuni wananchi kuwa wabunge waliowachagua hawafanyi kazi. Nilimshangaa Mh. Anna Kilango (Same Mashariki) na Mh. Ally Mohamed (Nkasi) walipomjia juu Bungeni waziri Ngeleja kuwa miradi ya Umeme ameirundika kwao Sengerema na kwa Mawaziri marafiki zake. Hii inaonyesha pia, viongozi wa serikali wanatumia miradi kuvutia kwao kama mtaji wa kuwarudisha tena kwenye POSHO. Tulitegemea BUNGE lijadili na kutetea mahitaji ya wananchi wote kwa usawa. Wananchi tumeanza kuliona pungufu hili kubwa na litaongeza chuki na serikali hii kwa makusudi haya wanayoyafanya. Nafikiri suluhu hapa ni kudai KATIBA ya wananchi itakayo ondoa mapungufu yote haya na kuleta usawa kwa wananchi wote. Bila KATIBA mpya, bado tutakuwa na mapungufu hayahaya tupende tusipende.
   
 17. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #17
  Jul 18, 2011
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Huyu kilaza anachekesha na kusikitisha sana. Dr Slaa awe amesomea sheria za kanisa, za msikiti, za sokoni hilo si muhimu kwa watanzania.
  Tanzania na Watanzania tunachotaka ni kuona na kusikia yale yatakayoweza kulitoa taifa letu katika uchafu na uozo ambao umesababishwa na CCM.

  Dr Slaa ameibua kashfa nyingi na nzito kama vile EPA, MEREMETA, DEEP GREEN, RICHMOND nk ambazo serikali iliyopo madarakani ilijaribu kukataa na kufunika kwa lengo la kuficha uchafu huo. Sidhani kama Dr Slaa alitumia degree yake ya sheria za kanisa katika kufichua uchafu huo, bali alitumia uzalendo wake kwa Taifa.

  Mwalimu Nyerere, hatukumpima kwa degree yake aliyosemea. Tulimpima kwa uzalendo wake aliokuwa nao kwa Taifa, hii ikiwa ni pamoja na marehemu Edward Moringe Sokoine.


  Kwa mtu yeyote mwenye akili timamu na uzalendo wa kweli kwa Taifa letu ataona na atakubali kwamba Chadema wana lengo na nia madhubuti kabisa la kutaka kuikomboa Tanzania toka mikononi mwa wakoloni weusi (CCM). CCM wametufikisha pabaya.
   
 18. c

  chief m Member

  #18
  Jul 18, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi niliyeshudia huyo mtu sio kilaza na anao uwezo wa kusema kwa hisia na mpaka kuwafanya watu wapokee hotuba kwa hisia kali, hayo maneno ulioordhesha aliyoyasema yamepokelewa kwa hisia kali kuliko ulivyoyaelezea hapo, watanzania wengine nadhani unawafaham, mpaka anamaliza hotuba walikuwa wanamwambia endelea, na kuna maeneo mengine walikuwa wanamwambia kwa furaha rudia kusema hilo. Mtu akipata muda afike tegeta atapata feel. Huyu jamaa hata Arusha, hata mpanda, sumbawanga, jimboni kwake na hata wakati anasoma huwa ananmna ya kuhutubia ambayo huwafanya watu wahamasike. Wananchi wetu bana?
   
 19. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #19
  Jul 18, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  swala la umeme, maji na mfumuko wa bei hakugusa kabisa? hahaha watanzania bwana yahani watu kila kukicha CCM inawapotosha mbona hawapendi kuzungumzia matatizo badala yake kuwakashfu wapinzani tu.
   
 20. Tuyuku

  Tuyuku JF-Expert Member

  #20
  Jul 18, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 3,149
  Likes Received: 1,406
  Trophy Points: 280
  Pole sana. Hivi kweli na wewe ukapoteza muda wako kuwasikiliza hao wanaofikiri kwa kutumia matumbo yao? Lkn bora umeweza kutushirikisha umbunye wao.
   
Loading...