MtuHabari
JF-Expert Member
- Oct 16, 2020
- 321
- 1,019
Nikiri kuwa Mimi ni mwanachama wa moja ya Press Club za mkoa ulio mashariki mwa nchi hii lakini pia miaka ya nyuma nilikuwa pia mwanachama wa Mwanza Press Club hadi miaka ya karibuni nilipohamia kwenye chombo cha habari chenye makao makuu yake huku Mikoa ya Pwani.
Hizi Press Clubs ni vyama muhimu sana kwa maslahi ya moja kwa moja kwa waandishi ambao ndio mwanachama wake.
Clubs hizi ziliunda (au kiukweli waliundiwa) chombo wakakiita mwamvuli wao nacho ni UTPC (Union of Tanzania Press Clubs) na ndio hapo misaada na ufadhili mbalimbali toka kwa wahisani inakopitia na kuratibiwa kabla haijafika kwenye Clubs au kwa waandishi wanachama moja kwa moja.
Sasa mwezi huu huko Morogoro utafanyika uchaguzi wa Rais mpya wa UTPC na wajumbe wa bodi ya wakurugenzi.
Je, wajumbe wa mkutano mkuu huo kutoka kila Press club ambao ni Mwenyekiti, Katibu mkuu na Mweka hazina wanaelewa wanakwenda kufanya nini na umuhimu wa jambo hilo?
Je, wajumbe hao wanafahamu kuwa kwenye nafasi ya Urais kuna waliojipanga kugombea kwa mbinu Kali ya kujinufaisha na tayari wanajinadi kuwa mambo yote sawasawa?
Nini kifanyike kuinusuru UTPC isiingie mikononi mwa matapeli ambao wana historia ya ujanja ujanja na wanaotaka kuhakikisha mambo yote ya UTPC yananufaisha hao walioko huko makao makuu ambako ni Mwanza?