Mkusanyiko wa matukio ambayo yameshawahi nitokea

Mkusanyiko wa matukio ambayo yameshawahi nitokea

20PROFF

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2013
Posts
8,217
Reaction score
7,255
Habari wanajamvi,

Natumai ni wazima kabisa. Wale wanaofunga nawapa pole na hongera, makobe badilikeni lakini nyote tumieni mfungo na kipindi kufanya yaliomema na acting ziishe. Leo nimeona niwaletee mkusanyiko wa matukio kadhaa yalioyowahi nitokea, kushuhudia au kusimuliwa na wahusika hii ni sehmu ya fasihi tu, so maudhui ya fasihi nadhani yanatambulika. Ngoja nianze kama ifuatavyo.

Nusura jumba bovu liniangukie: Nakumbuka ilikuwa usiku kama saa tano kuelekea saa sita. Tulikuwa tunapiga pindi na washkaji zangu wa chuo kipindi hiko. Geto letu lilikuwa karibu na Jeshini kabisa, so mpaka uliotenganisha jeshi na uraini ilikuwa ni miti iliyopandwa kama ishara ya mipaka.

Tulisikia kilio cha maumivu makali ambacho kilitupa tasfira kuwa kinatoka kwa binti. Alikuwa akilia kwa uchungu sana na uomba msaada kwa yeyote anayeweza muokoa, kwa haraka haraka nikajua labda anabakwa ama kukabwa na wahuni (maana wahuni hutegaga mara kadhaa kuvizia hapo na wengi wao ni watoto wa kota).

Nilishtua washkaji zangu tonde tukaone yanayojiri. Kutoka nje na kufika eneo la tukio maana kulikuwa hakuna umbali ni hatua kadhaa tu. Nakuta watu wamezunguka kiasi wakiangalia bila kutoa msaada kuhofia kugeuziwa kibao. Kumbe walikuwa wajeda wawili wakitembeza kichapo kwa dada mmoja.

Nilikuta amelala hawezi kusimama, anagalagala kutaka kujitoa katika katika mikono ya wale askari wenye hasira sana, mithiri ya simba alieporwa watoto wake. Kipigo kiliendelea bila wao kuhofu polisi kuja au watu kuingilia maana walimzusha kwewnye ule mpaka wa jeshi (hakuna fensi) na mpaka kufika kwenye geti la jeshi ambapo ndipo walinzi hukaa kuna ka umbali. Huyu dada alipigwa nikaanza kuona akotoka damu puani, pia naye alikuwa hakitamka mbavu zinamuua na mengine mengi. Wajeda walikuwa kimya sana na mara moja moja walikuwa wakiongea kuwa leo tutakua wewe.

Hasira, huruma zote zilinifika kuona hata mmoja wa watu katika kundi lile kashndwa kumpa msaada yule dada, maana hata kama kosa liwe la namna hakushtahili kwa kweli. Nikiwa na washkaji tumekaa karibu na kuangalia nikasema guys Tumsaidie huyu binti, wote walijitoa aisee. Nikasema its oky, let me try to get her out of there ( kipindi hiko nikiwa nimekulia na kuishi kota za jeshi muda mrefu sana so ikabida nitumie akili niijuayo kumsaidia huyu dada ).

Nina mwili na apearnce ya askari kama ukiwa hunifahamu. Kwa haraka haraka nikajua fika kuwa wale lazima watakuwa ni private tu, hakuna ataye zidi SGT. Ikabidi nivae ujasiri na kutoa kauli ya mari kwa wale askari, " nikasema private stand down". Wale jamaa mmoja wao ikibidi ageuke uangalia ni nani anaongea, mwenzie akiwa hajasikia neo kutokana na jazba. Nikarudia wewe kokapu husikiii amri yangu? Jamaa nilichogundua walikuwa maji pia ingawa hawayumbi yumbi, vinywa vyao vilikuwa na harufu ya pombe. Nikaanza zungumza nao na kuuliza nani kawapa kibali cha kupiga raia.

Wakataka nijitamburishe nami nilifanya hivyo, wakijua mimi ni Luteni (ilikuwa usiku, kucheki muonekano wa mwili wangu, na ujasiri na ukali ikabida wajifocre kutulia). Ikabidi waanze kunieleza kwanini wanampiga yule dada, huku yule dada akaanza kuningangania nimuokoe baada ya kuona jamaa wameweza tulia kwa kauli yangu. wakasema makosa ya yule dada kama yafuatayo Jamaa mmoja wapo alianza uhusiano na yule dada, baadae alienda likizo fupi kwao, yule binti aliachiwa pesa na alikuwa anatumiwa pesa na jamaaa kila atakapo au mshahara kutoka.

Pia jamaa alisema yeye ndie alimpangishia chumba na kumnunulia vitu vyote vya ndani. Lakini huyubinti nimerudi huku, nakuta chumba kina mpangaji mwingine nayeye kasema alipata matatizo ikabidi vitu vichukuliwe na kuuzwa alikuwa na madeni so akaamua kurudi kwao. Jamaa kwao hapajui wamekutana mjini, ila anawajua baadhi ya wadada wa huyu binti. Kumbe binti anamzingua jamaa, kapata bwana mwingine lakini mshikaji anapewa kalenda na kujibiwa hovyo sometimes.

Jamaa akasema alimpenda sanmsichana akasamehe yote hayo. Msichana akachana na yule mchepuko karudi kwa jamaa mapenzi yakaendelea, sasa huyu jamaa wa pili yeye ni rafiki wa karibu na huyu mwenzie, alikuwa kikosi kingine na alikutana na huyu binti akiwa na wenzake hapa hapa Dar. Jamaa naye akaingiza chiombezo msicha akalipokea sio wote wawili wakawa wanahudumia, msichana anachanganya wanaume.

Siku imetokea jamaa wakatembeleana kukumbushana mabo yao ya zamani na story za wasichana wa depo, ndipo likaja swala la kunyweshana pumziko lao jipya. Picha zikatolewa kwa simu kutambiana ndipo hapo ikagundulika wanashare, maana wote wakatoa picha zao punde walizopiga na msichana.

Hapo ndipo wakaamua kuweka mtego wamnasebinti, Jamaa akampigia simu msichana aje wanywe na kula nyama jioni, achukue usafiri atalipa, binti alifanya hivyo huku akitoa taarifa za uongo kwa huyu mwingine. Wakaenda bar za uraiani Baada ya vinywaji na maogezi ya hapa na hapa na pale huku mwingine akisubiri sms ya njoo tumalize mchezo akiwa anachoramchezo nzima kwa mbali. Ndipo hapo akatiwa nguvuni na kwenda kuchapiwa hapo mpakani. Wakati hayo maongezi yakifanyika binti alikuwa anasota miguuni mwangu na kulia nimuokoe.

Nilichowambia kuwa hapa kuna haja ya kuumuuliza binti, nikimuuliza jibu ni moja tu napewa, kaka naomba niokoe. Nikajua fika huyu binti ni mkosaji, ila inabidi nimsaidie maana uhai wa mtu ni ghali sana. Nikasema sasa yatosha, mmempiga vya kutosha mwacheni aende la sivyo nitawachukulia sheria, sawa! Wakajibu sawa afande. Hilo jibu lilinipa ujasiri kuwa hawa wameamini mimi ni mkuu wao.

Jamaa mmoja akasema basi naomba nimpeleke kwa dada zake napajua, huyu hawezi kufika mwenyewe. Nikasema huwezi nizidi akili, kumpiga kule kote sasa hivi hasira zimeisha? Au mwataka kwenda kumuua? Ooh huyu hana hela kaangusha pochi huko kwenye mtaro, nikasema pesa mtatoa nyie ya bajaji. Nikawataka wasaidiane kuchanag wenyewe wakatoa pesa, nikaomba baadhi ya watu wasaidie kuita bajaji ikaitwa.

Binti unapakumbuka kwao? Ndio unaweza mulekeza bajaji akafika ndio? Nikasema sawa, bajaji mpeleke chukua namba zangu hzi ukimfikisha kwao nibipu nuiongee na wenyeji wa pale. Binti alifka salama hadi leo hii huwa anasalimia sana na kujiluina hali.Nikasema wangejua mimi sio mjeda ningepotea


Nitaendelea na tukio jingine.......
 
Duu mkuu umejitengenezea chance.... Ukitaka..... Unamwita tu hana kipingamizi... Tena gharama kwake.... Hahahahaha.

Lkn mkuu uwe na kumbukumbu maana hata hiyo isha ntokea kuna baadh ya watu hata askar wakiniona wanajua mimi n mwenzao lumbe hataguu pande sijui.... So take care
 
matukio yanaendelea kama ifuatavyo............................

HURUMA YAGEUKA HASIRA KALI
Kuna kipindi kulikuwa na mvua kubwa sana zinanyesha DAR, ilikuwa ni msimu wa mvua. Kama mnavyojua kuwa misimu ya mvua watu huingia ndani mapema sana, kuogopa kuloa na kujikinga na baridi. Kipindi hiki ndipo baadhi ya watu huona nafasi ya fursa kutaka kupata kitu kutoka katika nyumba za watu kwa njia za wizi. Sasa hapa jirani na maeneo mengi kulikuwa na watu wanaolalamika kuibiwa vitu vyao kama vyombo vya ndani vilivyo nje ikiwemo masufuria, kukatwa nyavu na simu kuibiwa, na hata kuanua nguo na mashuka zilizo anikwa nje (maji yachuruzike zingizwe ndani).

Miongoni waliolalamika kuna vijana wamepanga hapo jirani, wengine wakiwa wapiga NONDO (GYM) wamepanga. Mwingine alikuwa akifanya michezo ya boxing zamani. Baba mwenye wao alikuwa ni askari mstaafu. Majamaa walikuwa wakipanga kuwa wakikamata mwizi watamalizana nae kimya kimya na ndicho kilichotokea.

Za mwizi ni arobaini, siku hiyo jamaa mmoja na mwenzie waliibiwa mashuka. Kwa hesabu za haraka harak jamaa anasema tukio hili ni dk 10 tu, maana nimeenda kuoga naingia ndani mashuka yapo, sasa hivi hayapo. Itakuwa huyu mwizi yupo around hapa anatuchora na kula timing ili aibe. Yule mwizi alikuja na mwenzie mgeni kwenye kazi hii, walikuwa peku peku. Nahisi labda kwa ajili ya urahisi wa kukimbia. Yule mgeni alitangulizwa aende apeleke zile, aliebaki kujibanza atamalizia zile na kukutana chimbo lao. Bahati mbaya au nzuri, katika pita pita yule mpiga Boxa akamtilia mashaka mtu aliekaa gizani akaenda kumhoji, wew nani..? unafanya nini hapa? kwa nini unangalia sana huku kwetu? mbona huna viatu? Yale maswali yote yalikosa majibu , ndipo jamaa akapata wazo huyu anawalakini. Kampa ngumi na mtama ili asikimbie na kuita wenziie, NIME MDAKA HUKU.

Jumla ya watu waliotoka ni kama 4, wakati kipigo kikiendelea kimya kimya, vijana wa baba mwenye nyumba wakatoka kufanya idadi ikiwa 6 na mzee akajiunga akawa wa 7. Jamaa alichapika kimya kimya ndipo alipata upenyo kuangia mtarani kukimbia mtarano hadi kutokea karibu na kwetu, hapo kelele zilikuwa zikiitwa KAMATA HUYOO, NENO MWIZI HALIKUSIKIKA HATA.

Wakati huo nikiwa room kwangu napiga zangu msuli, iko mbali kidgo na geti. dogo akiwa sebuleni alisikia mtu ameingia getini, hadi ndani kumcheki ni mtu mgeni, kavimba vimba akiomba amsadie kuna watu wanampiga wanamsingizia ni mwizi. Ikbidi dogo amwambie tulia kwanza, aende kuangalia hao ni wakina nani, kutoka nje anawakuta washkaji ikabidi dogo akaushe kwanza asikie nini kinaendelea.

walikuwa wakisikika wanasema ameingia humu huy, tumemwona. Dogo anauliza tu, mmemwona kweli ? kafanya nini huyo mtu..? muda huo, nikawa natoka niende kuoga. Natoka kwenye korido, namkuta mtu, Khaa. wew nani, unafanya nini hapa? akili za fasta zikaja huyu ni mwizi nikatupa taulo nimkabili. Akarudia maneno yale yale aliyo mwambia dogo.

Mama alikuwa yupo ndani kwake, baba hayupo ametoka. Hatunaga desturi ya kuweka mlinzi (wakurya sisi, mshua anasema wanaume wote nyie mlindwe na mwanaume mwenzenu haha). Nami ikabidi niende nje, nikaon dog kazidiwa maneno, nikasema haya ingieni ndani kwenye maua muangalia labda kajificha. Lengo langu likiwa wakimkosa, nimfate yule mzee kimya, kimya tumchukue huyu kijana tumhoji na kumpeleka polisi. Zogo likawa kubwa mama akasikia, jamaa baada kusikia mlango unafunguliwa wa chumba kingine akajificha bafuni, mama akatoa go ahead watu wamtafute ndani, nikasema sawa, maana ningepinga wangekuwa na shaka namimi.

Jamaa alifanya makosa haya, kilichofanya akaonekana.
1.Kaingia bafuni kafunga mlango kwa ndani, angeacha malango wazi ingekuwa na nafasi ndogo watu kuhisi kuwa yupo mule, maana hata kuingia ndani hawakuwa na hakika.
2. Mule bafuni hakuwasha taa, angewasha taa na kufungua maji watu wangehisi ni mtu wa ndani kwetu ndio yupo, mwizi hawezi jificha then afungulie maji bafuni. MTU WA NDANI HAWEZI KUINGIA BAFUNI GIZA HALAFU AJIFUNGIE NDANI, HILO LILITOA WALAKINI MLANGO UKAFUNGULIWA JAMAA KATOLEWA.
Neno nililosema ni moja tu, mkimpigia ndani na mkachafua rangi kwa damu, mtalipia hasara itayotokea.

Jamaa atolewa nje na hapo ndipo hasira zilinipata, baada ya kuwa akilopoka kuwa mdogo wangu na mimi tulikuwa tunamficha ndani. Hasira ziliwaka ghafla, katika kuonyesha sikuwa na katika huo mpango, ikabidi teke la kidevu na gumi kadhaa kutoka kwangu zimfike alikuwa amesimama.

Nashukuru kuwa hakutolewa uhai nje kwetu pale, bali yule mzee nilimshauri tu, aache vijana wampige bila dhana yeyote wapunguze hasira halafu ahojiwe alikopeleka nguo, hilo lilifanyika na nguo kupatikana baada ya kuwa tumempiga sana.
Kuna kipindi tunaweza pata majanga, hasara hata maafa pale tunapojaribu kusaidia watu, just imagine kauli hile ya kuwa tumemficha ingesikika kwa watu wasiotufahamu.........

Itaendelea ingine
 
Duu mkuu umejitengenezea chance.... Ukitaka..... Unamwita tu hana kipingamizi... Tena gharama kwake.... Hahahahaha.

Lkn mkuu uwe na kumbukumbu maana hata hiyo isha ntokea kuna baadh ya watu hata askar wakiniona wanajua mimi n mwenzao lumbe hataguu pande sijui.... So take care

haha, kwa sasa. Sina la kuogopa hata nikikutana nao
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom