Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,814
- 34,196
Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’.
MKURUGENZI wa Kituo cha Kusaidia Waathirika wa Dawa Za Kulevya, Sober House, kilichopo Bagamoyo, Pwani, Karim Banji, amekanusha taarifa zinazosambaa kuwa mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ amepelekwa katika kituo hicho.
Akizungumza Jumamosi na mtandao huu uliofunga safari mpaka kituoni hapo, Karim alisema kuwa ni kweli siku ya jana (Ijumaa) alipokea taarifa kutoka kwa watu wa karibu wa mwanamuziki huyo kuwa wangempeleka kituoni hapo leo (Jumamosi), lakini hadi majira ya saa tisa leo mchana hakuwa amepelekwa.
“Jana nilipokea taarifa kwa njia ya simu kutoka kwa mtu aliyejitambulisha kuwa ni mtu wa karibu wa Ray C (hakumtaja jina) kuwa watamleta leo, hapa unaponiona nimefunga safari kutoka Dar kuja bagamoyo kwa ajili ya suala hilo lakini mpaka sasa hajafika, kama ni kweli watamleta, basi nitawajulisha,” alisema Karim.
Baada ya kupokea maelezo hayo kutoka kwa mkurugenzi huyo, mtandao huu uliacha mawasiliano yake kituoni hapo na kung’oa nanga kusubiri taarifa zaidi.
Wakati Mkurugenzi huyo akitoa taarifa hiyo, tayari kuna taarifa kwenye vyombo vingine vya habari, ikiwemo mitandao ya kijamii ikisema kuwa Ray C amepelekwa Sober House Bagamoyo na kumkariri Karim kuwa amethibitisha taarifa hiyo.
Ray C amerejea tena kwenye vyombo vya habari mwishoni mwa wiki hii baada ya juzi Ijumaa kuonekana kwa kipande cha video yake ikimuonesha kama mtu aliyechanganyikiwa kwa kusema maneno hovyo baada ya kudaiwa kubwia kiasi kingi cha madawa ya kulevya, tuhuma ambazo amekuwa nazo kwa muda mrefu sasa licha ya yeye kujaribu kukanusha na kuuhadaa umma kuwa anasingiziwa. chanzo.Mkurungenzi Sober House Akanusha Ray C Kupelekwa Kituoni Hapo