Mkurugenzi wa vipindi Clouds, Ruge Mutahaba alaani RC Makonda kuvamia ofisi zao

I am awarding honorary PhD in Critical Thinking and Argumentation to Ruge mwana wa Mutahaba.

VERY SMART, HUMBLE, ANALYTICAL and ARGUMENTATIVE.
....exactly....in this fiasco Ruge came out big....and now we wait for the judgement day....where bashite bin kolomije has to be punished by his boss ngosha....If this won't happen then judgement will be carried by the mass media itself...only a matter of time....
 
Kama kuna jambo anajuta Bashite ni hili la kumtaja Gwajima kwenye madawa!
Wengine wote aliowataja wako kimya (ukiacha Mbowe aliyefungua kesi), lakini Gwajima amekula naye sahani moja (ameweka miguu kwenye kinu cha kusaga unga! atageuka sembe!).
Ninakumbuka siku anataja majina alisita sana kumtaja! mwanzo alipotaka kumtaja akapotezea lakini mwishoni akajitia nguvu akamtaja! Kwa hali aliyofikia hata mbeleko ya shaba itabidi ichemshe!
 
si mlikua mnajipendekeza sana wacha mkatwe mitama na walinzi wa bashite kama namwona sudy akivuliwa li soxy lake usoni na bashite
 
Ninapoitafakari hii issue ya Makonda au Bashite kama watu wanavyomuita sasa na CLOUDS Media napata maswali kadhaa:
1. Hivi ni kweli Makonda anaweza kwenda CLOUDS Media bila kuwasiliana na RUGE na wamiliki wengine?
2. Hivi urafiki wa Makonda na CLOUDS Media umeanza kuwa wa mashaka?
3. Je, hii sio movie ya kuficha au kuyeyusha jambo fulani linaloendelea kurindima kwenye social media na vyombo vya habari vingine?

I was trying to think loudly.
 
Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds Media amezungumza leo kupitia kipindi cha Clouds 360 kuhusu suala la uvamizi uliofanyika ofisini kwao ijumaa usiku.

======

Ruge: Niliwambia SHILAWADU siku ya Alhamisi mchana kuwa wasiirushe 'Story' bila kuongea na upande wa pili (wa Gwajima)

Ruge: Niliwambia Vijana wa SHILAWADU kuwa 'Story' kama ndo anayoisubiri RC basi ajue haitaenda hewani hata kwny Social Media

Ruge: Ijumaa niliwasisitiza SHILAWADU kuwa kipindi kile kisirushwe kwakuwa 'Story' haiko balanced

Ruge: Ijumaa saa 5 kasoro usiku nilipigiwa simu kuwa RC Makonda alikuwa kaja ofisini akiwa na maaskari wakiwa na silaha

Ruge: Nilimpigia simu RC Makonda kumhoji kwanini aje ofisini na maaskari wenye silaha? Akauliza kwanini nimezuia kipindi kuruka!?

Ruge: RC Makonda alikata simu, lkn nilipaniki nikiwazia hizo silaha walizokuja nazo ofisini. Makonda alikichukua kipindi kwny flash

Ruge: RC Makonda alisema "Bahati yenu" baada ya kujua kuwa waliokataa vijana wa SHILAWADU sio waliozuia kipindi isipokuwa mimi

Ruge: Nilimwambia Mkurugenzi wa Clouds(Kusaga) kuwa RC alitukosea heshima; kulikuwa na haja gani aje na silaha na ni rafiki yetu?

Ruge: Ukweli hakuna aliyepigwa ila kulijengwa hofu kubwa kwa wafanyakazi wa Clouds Media. Si jambo dogo hili!

Ruge: Tusikwepe ukweli kuwa sisi Clouds Media kama chombo cha habari tuna wajibu wa ku-balance story. Sijawahi kulazimishwa story...

Ruge: Kuacha shughuli za kazi, Makonda amekuwa akija hapa Clouds kama rafiki. Ila kitendo cha kuja na walinzi kiliwashtua walinzi

Ruge: Kama watanzania, hatutaki kuiona bunduki mitaani. Hili limetokea kutufungua macho kujua ma-RC na ma-DC wanavyofanya kazi yao...

Ruge: Sisi tuhukumiwe kama taasisi, wafanyakazi wetu wasitiwe hofu. Mimi sikuwekwa ndani, nilienda Polisi kuripoti suala hili

Ruge: Mtu akikosea kabla hatujaangalia cheo chake, tuangalie makosa yake. Si kudai eti wanaomkosoa wanapingana Vita ya [HASHTAG]#DawaZaKulevya[/HASHTAG]

Ruge: Mtu kuwa na nafasi ya Uongozi flani si sababu ya 'kuwapanda' watu . All we want is RESPECT!

Ruge: Video clips za CCTV zinazozunguka mtandaoni kweli ni za hapa Clouds Media. Sisi tulidhani Makonda angeomba radhi kwa kadhia hii

Ruge: Siujutii ukaribu wangu na Makonda. Hata akirudi akaomba radhi bado nitamfikiria! Tunataka kuendelea kumpa ushirikiano

Ruge: Niseme, urafiki na BUNDUKI siutaki. Wanaodai Makonda alikuja hapa Clouds akiwa rafiki wanapotosha! Ametumia vibaya madaraka

Ruge: Clouds inalaani kilichotokea, na inaomba Vyombo vya Habari vitoe ushirikiano ktk kukemea hili. Hatutaki kugombana na Serikali

poleni sana hapa kuna maswali mengi kuliko majibu alikuja na gari ya serikali au binafsi na alikuwa na mualiko wa kuja studio na utaratibu wenu wa kurusha matukio ukoje ,hauna mapungufu ya kuyafanyia kazi ni lazima niwepo studio ili tukio lirushwe .its very sad tuwaache wahusika wafanye kazi zao watupatie majibu stahiki. poleni poleni sana.
 
Ugomvi wa marafiki ukiingilia unaweza ukahamia kwako- ngoja nisubiri mwisho wake niujuwe
 
Kanywe maji ya betri km unaumia sana lakini huyo mumeo,basha wako au mchepuko wako lazima aondoke tuu
Ninapata uhakika pasi na shaka huyu ni mke wa makonda.
Nitakuthibitishia kwa machache;

Tumepata kusikia mwanamke yule ana asili ya Rwanda right.
Tazama andika yake. Utakubaliana na mimi hajui kiswahili vizuri.

cocochanel prove me wrong kwa kuandika hata paragraph moja kwa kiswahili kilichonyooka.

Niwasihi ndugu zangu msijisumbue na mtu huyu
 
Koti lile lilimbana ameamua kulivua. Wakati Mwingine ni lazima kujitoa na kuthubutu. Urafiki umeyumba umebaki unafki. Bashite hana pa kuruka kila kona yeye tu.
 
Mbona hawarushi clip ya hayo yanayosemwa? Tumeona tu anamlinzi na inatakiwa. Mkurugenzi hajasema kuwa atachunguza.

Hajavamia akiingia na bunduki ni analindwa.

Eti Nape nae amebeba njugu anamsaka Makonda tangu aanze ya madawa

Sinema inaendelea

Makonda oyeeeee
Ila we mrundi una moyo
 
Ruge ni snitch
anaongea hivyo baada ya kuona makonda kakalia kuti bovu
lakini aliweza kumlinda toka siku ya kwanza ya tukio
 
Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds Media amezungumza leo kupitia kipindi cha Clouds 360 kuhusu suala la uvamizi uliofanyika ofisini kwao ijumaa usiku.

======

Ruge: Niliwambia SHILAWADU siku ya Alhamisi mchana kuwa wasiirushe 'Story' bila kuongea na upande wa pili (wa Gwajima)

Ruge: Niliwambia Vijana wa SHILAWADU kuwa 'Story' kama ndo anayoisubiri RC basi ajue haitaenda hewani hata kwny Social Media

Ruge: Ijumaa niliwasisitiza SHILAWADU kuwa kipindi kile kisirushwe kwakuwa 'Story' haiko balanced

Ruge: Ijumaa saa 5 kasoro usiku nilipigiwa simu kuwa RC Makonda alikuwa kaja ofisini akiwa na maaskari wakiwa na silaha

Ruge: Nilimpigia simu RC Makonda kumhoji kwanini aje ofisini na maaskari wenye silaha? Akauliza kwanini nimezuia kipindi kuruka!?

Ruge: RC Makonda alikata simu, lkn nilipaniki nikiwazia hizo silaha walizokuja nazo ofisini. Makonda alikichukua kipindi kwny flash

Ruge: RC Makonda alisema "Bahati yenu" baada ya kujua kuwa waliokataa vijana wa SHILAWADU sio waliozuia kipindi isipokuwa mimi

Ruge: Nilimwambia Mkurugenzi wa Clouds(Kusaga) kuwa RC alitukosea heshima; kulikuwa na haja gani aje na silaha na ni rafiki yetu?

Ruge: Ukweli hakuna aliyepigwa ila kulijengwa hofu kubwa kwa wafanyakazi wa Clouds Media. Si jambo dogo hili!

Ruge: Tusikwepe ukweli kuwa sisi Clouds Media kama chombo cha habari tuna wajibu wa ku-balance story. Sijawahi kulazimishwa story...

Ruge: Kuacha shughuli za kazi, Makonda amekuwa akija hapa Clouds kama rafiki. Ila kitendo cha kuja na walinzi kiliwashtua walinzi

Ruge: Kama watanzania, hatutaki kuiona bunduki mitaani. Hili limetokea kutufungua macho kujua ma-RC na ma-DC wanavyofanya kazi yao...

Ruge: Sisi tuhukumiwe kama taasisi, wafanyakazi wetu wasitiwe hofu. Mimi sikuwekwa ndani, nilienda Polisi kuripoti suala hili

Ruge: Mtu akikosea kabla hatujaangalia cheo chake, tuangalie makosa yake. Si kudai eti wanaomkosoa wanapingana Vita ya [HASHTAG]#DawaZaKulevya[/HASHTAG]

Ruge: Mtu kuwa na nafasi ya Uongozi flani si sababu ya 'kuwapanda' watu . All we want is RESPECT!

Ruge: Video clips za CCTV zinazozunguka mtandaoni kweli ni za hapa Clouds Media. Sisi tulidhani Makonda angeomba radhi kwa kadhia hii

Ruge: Siujutii ukaribu wangu na Makonda. Hata akirudi akaomba radhi bado nitamfikiria! Tunataka kuendelea kumpa ushirikiano

Ruge: Niseme, urafiki na BUNDUKI siutaki. Wanaodai Makonda alikuja hapa Clouds akiwa rafiki wanapotosha! Ametumia vibaya madaraka

Ruge: Clouds inalaani kilichotokea, na inaomba Vyombo vya Habari vitoe ushirikiano ktk kukemea hili. Hatutaki kugombana na Serikali

Kwa kiasi fulani haya Malipo yanawastaili Clouds wasilalamike chochote unless ni kamchezo fulani kamekuwastaged kwao. Nimemsikia Ruge akisema Makonda ni rafiki yake japo ni mdogo kwake hivyo inabidi awe na heshima. Namshangaa Ruge kwani hiyo heshima ni kwake Ruge tu? Kipindi Clouds wakizunguka na Makonda akiita wafanyakazi vichaa hawakumsoma hadi yawakute wao? Tafakari
 
Back
Top Bottom