Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA Wilfred Lwakatare alazwa Hindu Mandal

Status
Not open for further replies.

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,894
20,375
KWA KIFUPI
  • Mbunge wa Bukoba Wilfred Lwakatare ni Mgonjwa
  • Alilazwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kabla ya kuhamishiwa Hindu Mandal
  • Mama Tibaijuka amefanya jitihada kubwa kuhakikisha Lwakatare anapata matibabu sahihi
  • CHADEMA hawataki taarifa za ugonjwa wake zijulikane kutokana na nafasi yake ndani ya chama
Mbunge wa Bukoba mjini Mh. Wilfred Lwakatare ni mgonjwa ambapo aliwahi kulazwa ICU Hospitali ya Mkoa wa Dodoma na Hindu Mandal.

Mama Tibaijuka alipomtembelea hospitalini Dodoma, ndipo wananchi tukajua kumbe Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA ni mgonjwa. Mama Tibaijuka na wabunge wengine wa mkoa wa Kagera kwa kushirikiana na uongozi wa Bunge walikodi ndege binafsi ya kumpeleka Dar es Salaam ambako amelazwa kwenye hospitali ya Hindu Mandal ambapo alipelekwa moja kwa moja ICU.

Inaelezwa pia kuwa jitihada zinafanyika ili taarifa za Lwakatare ziwe siri. Na watu wake wa karibu wameambiwa wasiiongelee kwenye public hali ya Lwakatare.

Sote tuungane kumuombea Lwakatare ili arejee kwenye hali yake ya kawaida
 
Ujumbe umefika ingawa umeuleta ukiaambatana na kejeli na vicheko kwa mtanzania mwenzako kuugua, pole lwakatare
 
Anyway. ..nimefundishwa kutokukejeli au kufanya siasa kwenye afya za watu...am logging off
 
Tibaijuka alifika hospital,kwani ushirikiano kati ya wabunge wa ukawa na ccm upo si, tulitangaziwa umevunjika na wenye wapenzi waachane by kubenea!
uongozi wa bunge uko chini ya katibu kashililah...yeye hana chama...na wabunge wote lazima wewe treated equally. ..kama hii ishu ni kweli ni kashfa Kubwa kwa bunge na uongozi wake
 
Umeandika kipumbavu kabisa! Kwa jinsi ulivyoandika hata kusoma mtu unashindwa maana umechanganya na hisia zako binafsi, majungu, itikadi za vyama, uchonganishi na fitina za kisiasa wakati hii ni kama kutoa taarifa.

Ujinga kila sehemu!
 
Siasa zetu mbaya sana mtu anafurahia kuumwa kwa mwenzie!!! Mapito ya dunia yanatusahaulisha tupo kama tunaweza kuishi miaka zaid ya 3000 wakat kuikamata 60 ni kazi pevu.
 
Mkuu, hilo nalifahamu kabisa. Hata hivyo, kuna jukumu la familia na taasisi anayofanya kazi. Kwani CHADEMA hamna mkakati wa kuwasaidia wabunge wenu?
Kwani BUNGE lilishaacha jukumu la kutibisha WABUNGE???.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom