Mkurugenzi wa Uendeshaji ACACIA aeleza sababu za kitaalamu kwanini wanasafirisha mchanga wa dhahabu

Huo utafiti wao ni uongo mtupu, tatizo tuna macho lakini tunajifanya hatuoni, tuna masikio tunajifanya hatusikii, mchawi wa mtanzania ni mtanzania mwenyewe
 
Suluhu ni kwa serikali yenyewe kuwekeza kwenye ujenzi na uendeshaji wa hizo smelters..
Mengine yote tumeyataka wenyewe.. Tusiwalaumu wawekezaji!
mkuu hiyo biashara ndogo sana hata akina Reginard Mengi wanaiweza wao watangaze tenda waone kama hawatajengewa fasta tena wa kisasa wakaachana na huo wa wachina. Tumejenga bomba la gesi kwa us$8billioni tushindwe chekecheo la mil 500.
 
Nasubiri muda wa kujua..kwa sasa nabaki hapa hapa..usilete mambo ya kusadikika..

Nyie ndo mnaleta mambo ya kusadikika mnoasema mchanga una 90% Madini...hiyo kauli alitakiwa aitoe mtoto wa darasa la tano si mtu unajiita muandisi unaongea ugoro kama huo.
 
Lakini haya mamichanga si waliwapa wenyewe,kama wanayachukua waachieni michanga yao...
Ahsante kwa maelezo mazuri naona process nzima ya uchimbaji wa dhahabu na kuchenjua. kimsingi hao ACACIA wako sahihi na wanaendana na makubaliano tuliyoafikiana kimkataba. Jambo linguine nililoliona kumbe kwa kila hatua kuna wakaguzi au observers wa serikali TMAA, TRA, Ministry of Minerals etc mashaka yangu ni weledi wa hao wakaguzi yawezekana wapo tu lakini uelewa wao ni mdogo kujua process kama zilivyoainishwa kitaalamu hapo juu, vile vile yawezekana kuna harufu ya rushwa hapo kwenye ukaguzi na usimamizi maana watoza ushuru na TMAA wanaweza kupokea kitu kidogo na kutoa takwimu ambazo sio sahihi za usafirishaji mchanga huo wenye dhahabu, fedha, Shaba na chuma unaoenda nje ya TZ kuchenjuliwa. ACACIA wao wana biashara hapo lazima hutumia mbinu kubwa ili wapate faida kubwa hiyo ni pamoja na kupitia udhaifu wetu wa kitaalam na uaminifu wa watendaji kazi wetu. linguine la kitaalam imeonekana kuna process mbili, kwanza wanapata dhahabu ghafi (Tofali) huku huku TZ na mabaki ambayo ndio mchanga pia huuzia makampuni mengine yaende kufanya hizo stage za smelting au oxidation kulingana na technologies walizo nazo. imeonekana kujenga viwanda vya uchenjuaji ni ghali kwetu huku hasa kutokana na kiwango kidogo cha upatikaji wa madini yanayotakiwa kuchenjuliwa. Chile wameweza kujenga kwa kuwa wao wanazalisha hadi tani 850,000 sie ni tani 30,000 tu hapo wawekezaji wanasita kuwekeza mtambo wa kuchenjua kutokana na production yetu ni ndogo.......mie nimeelewa hivyo
 
Kuna pesa migodi inatoa kwa ajili ya kufukia hayo mashimo baada ya uchimbaji kumalizika...kama hayajafukiwa hiyo pesa imeliwa hapo hapo almashauri ya nzega..
katika mikataba ya madini ya kimataifa waliolichimba ndio wanapaswa walifukie na kurudishia ardhi kama walivyoikuta hatakama waliwakuta vyura walipaswa wawatunze hadi wakimaliza kuchimba wawarudishe, kumbuka sakata la vyura wa kihansi wale wajenzi waliwatunza vyura hadi leo wanawatunza kwa kuharibu mazingira yao.
 
mkuu hiyo biashara ndogo sana hata akina Reginard Mengi wanaiweza wao watangaze tenda waone kama hawatajengewa fasta tena wa kisasa wakaachana na huo wa wachina. Tumejenga bomba la gesi kwa us$8billioni tushindwe chekecheo la mil 500.

Mwekezaji atakayejenga copper concentrate smelter Tanzania kwa sasa atakuwa siyo tu mwendawazimu Bali ni mwehu Kabisa.

Mwambie rais wako awashawishi wajenge sasa uone kama watakubali.
 
katika mikataba ya madini ya kimataifa waliolichimba ndio wanapaswa walifukie na kurudishia ardhi kama walivyoikuta hatakama waliwakuta vyura walipaswa wawatunze hadi wakimaliza kuchimba wawarudishe, kumbuka sakata la vyura wa kihansi wale wajenzi waliwatunza vyura hadi leo wanawatunza kwa kuharibu mazingira yao.

Nakubaliana na wewe ila mkuu wangu hii ni Tanzania ujue..
 
Kumbe TRA na TMAA huwa wapo kila hatua?Sasa swali je yale makontena 200 yalikamatwa au yalizuiwa?
Mkuu hizo ni siasa tu!! Ila yale yamefika pale kihalali kabisa. Na utaniambia mwisho wa yote hutaambiwa sakata hili limeishia wapi
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Migodi ipo miaka yote na hayo yote huwa yanafanyika kama taratibu zilivyo, TMMA na TRA wapo migodini miaka yote, je walikuwa hawajui kinachofanyika? siasa za kutafuta umaarufu ndiyo zinazotumika sana Tanzania, Jiulize nani anaweza kujenga kiwanda kwenye nchi inayoweza kuzalisha Tani 25-30.000 kwa mwaka, hata kama kitajengwa je ni majirani wangapi wa Tanzania wanaozalisha mchanga wenye madini kuweza kuzalisha jumla ya Tani 800-900.000 kwa mwaka ili kiwanda kiwe busy na kazi, Tunawaza kujenga kiwanda tu, je kiwanda kitafanya kazi kama kawaida na kuingiza mapato. kuna viwanda vingapi vimebaki magofu Tanzania- nini kilitokea katika katika kiwanda cha nyama pale kawe
 
Mwekezaji atakayejenga copper concentrate smelter Tanzania kwa sasa atakuwa siyo tu mwendawazimu Bali ni mwehu Kabisa.

Mwambie rais wako awashawishi wajenge sasa uone kama watakubali.
serikali itangaze tenda wakikosa mjenzi ndio tuseme haiwezekani, tuliwahi ambiwa hatuwezi kuwa na kituo cha television eti ni gharama sana kukiendesha viko ulaya tu, leo hata akina Millard Ayo wanavyo mnaanza kutuletea story hizohizo waambieni watoto wa shule waliozaliwa 2009.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
wacha mawazo ya kishamba, hao walioua hivyo viwanda akina lowasa sumaye hawako tena serikalini, acacia/MEM/stamico watangaze tenda ya mwekezaji uone kama akina Dangote hawajaruka na Jet zao na kubanana Mlangoni mwa JPM, juzi tu walitaka kupiga us$ 4b kiulaini isingelikuwa JPM kulibumburua.
Unataka atangaze nani? Kwenye mazungumzo siku za awali 2011, ilikuwa serikali ijenge. Kama ndivyo serikali itangaze ili tusubiri kuona wafanyabiashara watakaokuwa tayari kujenga plant ya kuchenjua tani 30,000 za concentrate!

Wafanyabiashara siyo wapumbavu kiasi hicho. Hawawezi kuwekeza $800m kwenye kitu ambacho wanajua dhahiri hakitarudisha pesa yao pamoja na faida. Concentrates zinazalishwa mataifa mengi, hujiulizi kwa nini wafanyabiashara wengi au nchi nyingi hazijengi? Dangote u Bakhresa usifikiri amefika pale kwa pupa. Anawekeza baada ya kujiridhisha kuna faida.

Watu wanadhani dhahabu inapatikana Tanzania tu! Tanzania haimo hata katika top 15 countries. Hata zile top 15 gold producing countries, siyo zote zina plants za kuchakata concentrates. Tusidanganyike kuwa na kiwanda cha kuchakata ndiyo kupata faida zaidi kutokana na madini. Ni hesabu za kibiashara na kiuchumi ndiyo zitatusaidia. Kuna wakati unapata faida kubwa zaidi kwa kujenga jengo lako mwenyewe ili uweke biashara yako, kuna wakati unapata faida zaidi kwa kukodi.
 
Unaweza ukawa mnufaikaji namba moja hata Deo Mwanyika wa ACACIA ni mbongo mwenzetu lakini ukiigusa anakuwa mkali vibaya..kuna tetesi kuwa anakula mill 30 kwa mwezi kama mshahara.
Anakula milioni 75 mkuu jamaa yuko njema sana yule
 
Hapana hayajakamatwa. Yamezuiliwa kwa sababu ya agizo la Rais.

Hayo makontena yote yamekutwa na seal ya TRA, inamaanisha TRA washakagua na kupokea chao.

Tunafanya mambo kwa hisia na mtu akielezea tofauti anaitwa mpiga dili au si mzalendo. Hakuna mtu anaweza kujaza kontena la gold na kulilaza bandarini. Wengine hata hawajui gramu moja ya gold ni kiasi gani.
Magazet yaliripot YAMEKAMATWA
 
serikali itangaze tenda wakikosa mjenzi ndio tuseme haiwezekani, tuliwahi ambiwa hatuwezi kuwa na kituo cha television eti ni gharama sana kukiendesha viko ulaya tu, leo hata akina Millard Ayo wanavyo mnaanza kutuletea story hizohizo waambieni watoto wa shule waliozaliwa 2009.

Anayetakiwa kutangaza tenda ni serikali sio Acacia...acacia wao wanapata faida hata wakisafirisha mchanga kwenda nje.

Sasa kwa vile magufuli ni mzee wa maamuzi na hafuati hata bajeti yeye anajichukulia hela tu. Ajenge sasa hyo smelter kama haijaishia kuwa nyumba ya popo.
 
Kipindi cha kupigania uhuru Afrika Kusini nilishangaa sana ngozi nyeusi kugeukana wao kwa wao, kuna weusi waliokuwa wameajiriwa polisi, walikuwa wanawaamrisha mbwa kuwang'ata watu weusi wenzao.
Hii ndio inajionesha kwa hawa akina Mwanyika wa Acacia, Kafumu Dalali, Zitto Kabwe n.k wanatetea matumbo yao. na ya mabwana zao.
Tatizo vile vitabu vya zamani vya historia ya nchi yetu, Adili na nduguze, kibanga ampinga mkoloni, chifu mangungo, KULI n.k serikali imevipiga marufuku na havionekaniki, watoto wangejifunza uzalendo kuanzia shule ya msingi. lakini blah blah nyingi.
 
Naona katoa sababu za kitaalamu za kutuibia. Mwambieni hatuyibiwi tena tumeshashtuka...tumeamka
 
Hata serikali yenyewe mpaka sasa imekwishajua na imejiridhisha uwezekano wa kujenga hiyo smelter hapa haupo. Kinachoendelea kwa sasa ni kuona kama kunaweza kuwa na uwezekano wa kupata mapato zaidi kutokana na uuzwaji wa concentrates, siyo kujenga smelter.

serikali itangaze tenda wakikosa mjenzi ndio tuseme haiwezekani, tuliwahi ambiwa hatuwezi kuwa na kituo cha television eti ni gharama sana kukiendesha viko ulaya tu, leo hata akina Millard Ayo wanavyo mnaanza kutuletea story hizohizo waambieni watoto wa shule waliozaliwa 2009.
 
Uzalendo hauonekani kwenye kushikilia ujinga bali uonekane kwa mambo yenye manufaa kwa Taifa letu. Kwa fikra zako akitokea mwehu mmoja leo hii akasema kuanzia leo, kuagiza magari toka nje ni marufuku, tununue magari tuliyoyatengeneza wenyewe, atakuwa mzalendo?

Back
Top Bottom