Mkurugenzi wa Uendeshaji ACACIA aeleza sababu za kitaalamu kwanini wanasafirisha mchanga wa dhahabu

king Davidson

JF-Expert Member
Feb 9, 2017
252
1,063
Ni kwa jinsi gani na kwa nini tunazalisha mchanga wa dhahabu (Makinikia)?

Siku ya Ijumaa tarehe 3 Machi, Wizara ya Nishati na Madini ilitoa tamko kupitia vyombo vya habari kuzuia uuzwaji wa mchanga wa dhahabu (makinikia) kwa misingi kwamba makampuni lazima yawekeze katika ujengaji wa kinu cha kuchenjulia hapa Tanzania , badala ya kupeleka bidhaa hii nchi nyingine kwa ajili ya uchenjuaji. Agizo hilo limetimiza muda wa wiki mbili sasa na linaathiri migodi miwili ya Bulyanhulu na Buzwagi, ambayo huzalisha makinikia yenye dhahabu, shaba na fedha. North Mara hawaathiriki.

Mkurugenzi Mtendaji wetu, Brad Gordon aliwasili Tanzania wiki iliyopita kuhudhuria mikutano ya mahususi na viongozi wa serikali na kujaribu kueleza athari ambazo hatua hii itapelekea juu ya biashara yetu hata wakati mazungumzo zaidi yanaendelea juu ya njia zinazofaa huko mbeleni katika kufanya uchunguzi wa aina ya kinu cha uchenjuaji kinachoweza kujengwa Tanzania. Mpaka wakati huu ambapo katazo bado linaendelea tunayo matumaini kwamba kutakuwa na habari njema katika siku za usoni ili shughuli za kawaida ziweze kurejeshwa.

Usafirishaji madini mchanga nje ya nchi, au kwa upande wetu uuzwaji wamakinikia shaba ni suala nyeti katika kila nchi yenye madini. Kuna mtazamo kwamba Tanzania inapoteza asilimia kubwa ya mapato kwa kutokuchenjua makinikia hayo nchini, pia kuna mtazamo mwingine kwamba makampuni pia huuibia Tanzania kwa kutokutangaza madini yote yaliyomo katika makinikia. Haya ni masuala mazito, na yenye madhara makubwa kwa mustakabali endelevu na faida ya biashara yetu na sekta ya madini Tanzania. Ili Acacia iwe na mafanikio katika Tanzania, ni lazima kuwa na uwezo wa kushughulikia na kusahihisha hizi dhana potofu. Ili sote tuwe na uelewa, katika migodi yetu, sisi huzalisha mapato yetu kwa:

1. Kuzalisha na kuuza tofali za dhahabu (Doré) ambazo baadae huboreshwa/husafishwa ili kupata dhahabu safi zaidi. Hii ni sawa na asilimia 55% ya mapato yote katika mgodi wa Bulyanhulu, na asilimia 45% ya mapato katika mgodi wa Buzwagi na asilimia 100% ya mapato katika mgodi wa North Mara.
2. Uzalishaji na uuzaji wa makinikia (ambayo huchenjuliwa na kusafishwa ili kutenganisha dhahabu, shaba na fedha - hii ni sawa na asilimia 45% ya mapato yote katika mgodi wa Bulyanhulu, asilimia 55% ya mapato yote katika mgodi wa Buzwagi na asilimia 0% ya mapato katika mgodi wa North Mara.

Mauzo ya dhahabu ni asilimia 95% ya mapato ya jumla, na asilimia 70% ni kutoka mauzo ya tofali za dhahabu na asilimia 25% hutoka kwenye dhahabu iliyomo ndani ya makinikia. Asilimia 5% iliyobaki ya mapato ni kutokana na shaba iliyomo katika makinikia na kiasi kidogo sana cha fedha. Kwa msingi huu, kampuni kwa sasa inapoteza asilimia 30% ya jumla ya mapato, na karibu asilimia 50% ya mapato ya pamoja ya Bulyanhulu na Buzwagi. Kwa katazo hili la kusafirisha makinikia tunapoteza mapato ya zaidi ya $1 milioni kwa siku (na mapato ya ziada yanapotea kutokana na makinikia yaliyopo Dar es Salaam ukisubiri kusafirishwa na ambao umekwisha lipiwa mrahaba ).

Kushughulikia suala la uaminifu

Kuna mtazamo kuwa hatutangazi wazi kila kitu kilichomo kwenye makinikia. Hii siyo kweli.
Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) wapo katika kila mgodi wetu na pia wanayo makufuli na mihuri kwenye maeneo mbalimbali ya vifaa vya ndani ya chumba cha dhahabu kiasi kwamba hatuwezi kufanya kazi bila TMAA kuwepo ili kuthibitisha kila kitu tunachofanya. Kila tofali la dhahabu na kila kontena la makinikia linalosafirishwa linatolewa sampuli ili kujua kiasi cha dhahabu, shaba na fedha iliyomo. Sampuli nne huchukuliwa: moja kwa Acacia, moja kwa TMAA, moja kwa kinu cha uchenjuaji cha nchi tunayopeleka na sampuli moja huwekwa kama akiba iwapo kutatokea mgogoro wa aina yoyote au tofauti kati ya sampuli nyingine zilizochukuliwa

Zaidi ya uwepo wa maafisa wa TMAA mgodini, inapofikia wakati wa kusafirisha matofali ya dhahabu au makinikia , maafisa kutoka Mamlaka ya Mapato (TRA) pia wanakuwepo kusimamia mchakato. Kabla makontena ya makinikia hayajapakiwa kwenye malori, ni lazima kujua thamani ya dhahabu, shaba na fedha iliopo katika makinikia kupitia sampuli zilizochukuliwa, na kulipa mrahaba kwa serikali. Wakati mrahaba unapokelewa katika akaunti ya benki ya serikali, makontena yanawekewa mihuri na TMAA na TRA na kisha usafirishaji unaweza kuanza


Mchanga wa dhahabu ni nini na kwa nini tunauzalisha?


Jinsi tunavyochenjua madini inatokana na jinsi madini yalivyoumbika katika miamba mamia ya mamilioni au mabilioni ya miaka iliyopita. Uwanja wa sayansi ya jiolojia, uhandisi madini na madini (usindikaji madini) ni wa ajabu/kuvutia na unahitaji kuwa na uelewa wa njia bora ya kugundua, kuchimba na kuchenjua madini yanayouzika.

Kwa ujumla, wakati dhahabu ndio madini pekee yanayoweza kuuzika (yaani> 98-99% ya thamani), tunaweza kufanya mchakato wa uchenjuaji mgodini na kutoa matofali ya dhahabu. Katika migodi ya North Mara na Geita, dhahabu inachenjuliwa kwa kutumia mbinu mvuto, na baadae sianidi inatumika kuyeyusha dhahabu ambayo iko katika chembechembe ndogo zaidi. Matofali ya dhahabu huzalishwa katika migodi yote hii miwili.

Bulyanhulu na Buzwagi zina utaratibu tofauti kidogo, kutokana na aina ya mwamba katika migodi hiyo ambao una dhahabu zaidi (95% ya thamani) na metali nyingine zenye thamani kama vile shaba na fedha (5% ya thamani iliyobaki). Migodi yote hiyo bado inauwezo wa kuchenjua karibia nusu ya dhahabu yao kwa kutumia mbinu mvuto na mbinu sianidi Leach. Hata hivyo tunahitaji kutumia mbinu zaidi ili kuvunja miamba ya sulphide ili dhahabu nyingine, shaba na fedha ziweze kupatikana.

Kwa bahati nzuri, tunaweza kutumia mchakato uitwao 'flotation' ambapo kemikali zinaongezwa kulainisha mawe na kusababisha madini kuelea na hivyo kuachanisha na miamba fifi (waste rock). mchakato wa flotation ni mzuri sana na hufanya dhahabu, shaba na fedha kujilimbikiza pamoja na kuwa na thamani zaidi na kuwa na umbo dogo sana kuliko la awali wakati wa kuchimbwa:

 Mgodi wa Bulyanhulu unaweza kuchenjua tani milioni 1.0 ya madini ya chini ya ardhi kwa mwaka na, kupitia mchakato flotation, huondoa zaidi ya miamba fifi(waste rock) na huchanganya madini katika tani takriban 25,850 ya mchanga wenye dhahabu na shaba. Hiyo ni karibu na kupunguza mara 40 katika ujazo ambayo hufanya mchanganyiko unaopatikana kuwa na thamani ya kutosha kwa ajili ya kuuza.

 Mgodi wa Buzwagi unaweza kuchenjua tani milioni 4.4 ya madini katika shimo la wazi kwa mwaka ambayo ni ya chini sana kidaraja na, kwa njia ya flotation, huondoa zaidi ya miamba fifi (waste rock) na kuchanganya madini kuwa katika tani takriban 25,750 za mchanga wenye dhahabu na shaba. Hiyo ni karibu kupunguza mara 200 katika ujazo na kufanya mchanga huo kuwa na thamani ya kutosha kwa ajili ya kuuza.

Hatuwezi kuchenjua asilimia 100% ya dhahabu, fedha na shaba kutoka katika madini yetu. Kwa Bulyanhulu, mfumo wetu wa gravity, sianidi Leach na flotation ni mchakato unaowezesha kupata dhahabu bora na wakati huo huo tunaweza kupata shaba ya kutosha yenye thamani inayoweza kununuliwa kutoka kwetu na vinu vya uchenjuaji vya nje.

Nina imani kwamba kwa maelezo haya mafupi watu wataelewa , kwamba ni kutokana na aina ya miamba ndio inayopelekea kutumia njia fulani ya uchenjuaji. Kwa njia nyingine , North Mara na Geita wana bahati kwa sababu wao wana uwezo wa kufanya uchenjuaji wao wote mgodini na kuzalisha matofali ya dhahabu. Kwa makinikia ya Bulyanhulu na Buzwagi , dhahabu inayopatikana ndio bidhaa muhimu wakati shaba na fedha ni asilimia 10-15% tu ya thamani ya makinikia hayo.

Uchenjuaji yakinifu

Inaonekana kwamba moja ya maswala makuu yaliyosababisha kupigwa marufuku uuzaji wa mchanga wetu nje ni kwamba tunapaswa kufanya uchenjuaji wetu wote nchini Tanzania kwa sababu vinginevyo nchi inakosa faida kamili kutokana na madini yake. Ni muhimu kutambua kuwa mchanga wetu wa dhahabu / shaba / na fedha ni bidhaa ambayo inasindikwa kwa ustadi na umakini mkubwa.

Wakati kampuni za uchenjuaji wa makinikia nje ya nchi (smelters) zinatutoza fedha kwa ajili ya kuchenjua mchanga wetu, kwa wastani kutokana na masharti ya mkataba tuliokubaliana nao, tunapokea asilimia 97% ya jumla ya thamani ya dhahabu, fedha na shaba. Hiyo ni kwa sababu kwa kampuni yoyote ya uchenjuaji wa mchanga wa dhahabu au uchenjuaji wowote unaotumia kemikali, kupata asilimia 100% ya bidhaa haiwezekani na masharti haya yanafanya kampuni za uchenjuaji mchanga za nje kuhakikisha kwamba wanapata juu zaidi ya viwango (au sivyo watapoteza fedha).

Nchini Tanzania (kama kinu cha uchenjuaji mchanga wa dhahabu kitajengwa), muendeshaji wa kiwanda hicho itabidi aweke masharti ya ushindani, si tu kwa bei lakini pia kutokana na recovery au marudio ya metali mbalimbali, kwa hiyo faida yao itategemea gharama zao za uchenjuaji na ufanisi.

Kwa ujumla kuna aina mbili tofauti za uchenjuaji ili kutoa dhahabu, shaba na fedha kutoka kwenye mchanga wa dhahabu: Uchenjuaji wa mchanga wa dhahabu (smelting) na oxidation. Kuna aina tatu za uchenjuaji wa oxidation: roasting, pressure oxidation na bio-oxidation. Aina ya uchenjuaji unaotumika utategemea maswala kadhaa ikiwa ni pamoja na aina ya madini , ukubwa wa kituo na upatikanaji wa umeme nafuu.

1) Uchenjuaji wa mchanga wa dhahabu (Smelting): inahusisha kuuchoma mchanga huo kufikia nyuzi joto 1,200 ° C ili kuyeyusha vyuma vyenye thamani (dhahabu, shaba na fedha)

2) Roasting: kimsingi 'kupika' mchanga wa dhahabu katika nyuzi joto 750 °C na kutenga dhahabu, shaba na fedha kwa kubadilisha sulphur iliyo katika madini ya sulphide kuwa gesi ya sulphur dioxide (ambayo inazalisha kiasi kikubwa cha asidi ya sulfuriki)

3) Pressure oxidation: autoclave (tanuri kubwa ) inayofanya kazi katika nyuzi joto ya 190 - 225 °C na pressure kubwa ya kiwango cha 1.9-3.2 MPa (vipengele vingi vimeundwa kutokana na titanium kutokana na hali yake)

4) Bio-oxidation: kutumia bakteria katika umajimaji ulio katika nyuzi joto 42 °C, ambao kiuhalisi ‘wanakula' sulphide iliomo kwenye dhahabu, shaba na fedha.

Kuna maelezo mengi ambayo yanaweza kutolewa ya kina kuelezea hizo mbinu mbalimbali za uchenjuaji, ingawa katika hali zote kiasi cha shaba kwanza hutengwa na dhahabu na fedha na hizi huchujwa tofauti ya kupata bidhaa ya mwisho ya chuma.

Kama migodi yetu ingeweza kujenga kiwanda cha kuchenjua mchanga wa dhahabu kingekuwa kidogo ikilinganishwa na viwanda vikubwa vya kibiashara. Zaidi ya hayo, gharama za umeme nchini Tanzania ni kubwa ikilinganishwa na ilivyo katika nchi nyingine zilizoendelea katika sekta ya uchenjuaji wa mchanga wa dhahabu. Wakati migodi ilipokuwa inajengwa (Bulyanhulu katika miaka ya 1999-2000 na Buzwagi katika miaka ya 2007-2008), tafiti zilionyesha kuwa ni nafuu zaidi kuuza mchanga wa dhahabu kwa kampuni kubwa za uchenjuaji kibiashara ambazo wanapata umeme kwa bei nafuu badala ya kujenga chetu wenyewe. Kwa sasa tunauza mchanga wetu wa dhahabu kwenye viwanda vya uchenjuaji vilivyopo Ujerumani, China na Japan.

Kulingana na mpango wa sasa wa mgodi, Buzwagi una muda wa miezi 18 ya kuzalisha mchanga wa dhahabu, na baada ya muda huo, wakati wa usindikaji wa grade ndogo ya mchanga wa dhahabu, haitahitajika kuchuja shaba yoyote na dhahabu yote itachenjuliwa kwa kutumia mfumo wa gravity na sianidi Leach. Hii utaufanya Bulyanhulu kuwa mgodi pekee mkubwa Tanzania ambao unazalisha mchanga wa dhahabu.

Je unafikiria nini?

Kama wafanyakazi wa Acacia, au makandarasi wanaofanya kazi katika migodi ya Acacia, au familia na marafiki, bila shaka unaweza ukashangaa kwa nini hakuna kiwanda cha kuchenjulia mchanga wa dhahabu yetu, shaba na fedha nchini Tanzania.

Kama ingeleta maana kiuchumi kufanya hivyo - kwa ajili ya nchi na kwa ajili ya kampuni – basi kiwanda hicho kingejengwa. Kusini mwa DRC na kaskazini mwa Zambia (zote ni sehemu ya ukanda wa shaba, ambapo shaba ni bidhaa ya msingi), kuna migodi ya kutosha kuzalisha mchanga wa shaba kuleta umuhimu wa ujenzi wa kiwanda kikubwa cha kuchenjulia na vituo vya kusafishia katika nchi hizo ambavyo vingeweza kutumika na migodi kadhaa kwa kuchangia gharama. Katika Marekani ya Kusini, baadhi ya migodi ya shaba - kama vile Chuquicamata huko Chile - ni mikubwa kiasi kwamba hufanya uchenjuaji wao wenyewe (wana uwezo wa kuzalisha tani 855,000 kila mwaka, ikilinganishwa na Bulyanhulu wa tani 25-30,000 tu kwa mwaka).

TMAA ilifanya utafiti kuhusu ujenzi wa kiwanda hicho cha kuchenjulia mchanga wa shaba na dhahabu nchini Tanzania ambao ulikamilika mapema mwaka 2011 na ambao ulihitimisha kwamba hakuna faida katika kufanya hivyo. Acacia amejitolea kutoa mchango kwa Serikali ili kufanya mrejesho (update) ya utafiti huu (ingawa hatutashiriki katika utafiti yenyewe), ili kuona kama hali imebadilika.

Ni muhimu kwamba sisi sote tunaelewa zaidi kuhusu zuio hili kwa makini ili wakati wa kujadiliwa katika duru mbalimbali, tuweze kuwa na maoni na majadiliano ya kina. Suala hili kwa kweli linatuathiri sote. Tafadhali toa maoni yako ili tuweze kusaidia kufanya jambo hili kuwa rahisi kuelewa, kujenga uaminifu na kuelezea. Kwa muelekeo wa sasa, tunaamini tunafanya vizuri zaidi kwa Tanzania na Acacia, kwa kusindika dhahabu yetu na madini ya shaba yaliomo katika mchanga wa dhahabu katika migodi ya Tanzania na kisha kuuza bidhaa hiyo kwenye kampuni za uchenjuaji wa mchanga huo (smelters) zilizopo katika nchi nyingine.

Asante Sana

Mark Morcombe
Chief Operating Officer
 
Jana PM ameenda migodini,najiuliza tu miaka yote hii haya mambo yalifanywa kimagendo?
kama wakiendelea na misimamo hii hii migodi itafungwa kwani unaona asilimia 55 (55%) ya mapato yao pia hutokana na usafirishaji wa migodi
 
Kuna mtazamo kuwa hatutangazi wazi kila kitu kilichomo kwenye makinikia. Hii siyo kweli.
Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) wapo katika kila mgodi wetu na pia wanayo makufuli na mihuri kwenye maeneo mbalimbali ya vifaa vya ndani ya chumba cha dhahabu kiasi kwamba hatuwezi kufanya kazi bila TMAA kuwepo ili kuthibitisha kila kitu tunachofanya.
Wakuu, hivi hawa TMAA kimajukumu Vs kiutendaji wanatofautiana na BASATA!?
 
Unaweza ukawa mnufaikaji namba moja hata Mnyika wa ACACIA ni mbongo mwenzetu lakini ukiigusa anakuwa mkali vibaya..kuna tetesi kuwa anakula mill 30 kwa mwezi kama mshahara.
tuache siasa nyepesi hili swala linaenda kugusa taifa kwenye maswala ya uchumi
 
Lakini haya mamichanga si waliwapa wenyewe,kama wanayachukua waachieni michanga yao...
 
Back
Top Bottom