Mkurugenzi wa Richmond apandishwa kizimbani!

Mohamed Gire alikuwa mshika mpini tu. Tunalitaka jembe la Richmond!!!! Gire ndo Mbuzi wa kafara au!!!!???

Aliyefikishwa mahakamani ni Naeem Adam Gire na si Mohamed Gire
 
Hivi jamaa bado alikuwa Dar? Mimi nilifikiri alishakimbilia USA kwao muda mrefu.

Je aliyefikishwa ni Mohamed Gire mwenyewe au hao wadogo zake. Kama ni yeye mwenyewe nafikiri ni mhusika mkubwa sana ukiondoa hao wanasiasa.

Watu inabidi kujifunza, wanatumiwa na wanasiasa, majanga yakija, wao wanaishia Keko huku wanasiasa wanapeta.

Aliyefikishwa mahakamani ni Naeem Gire

i216_CriminalCase.jpg
 
Uchunguzi bado unaendelea!!!

Huu huwa ni msemo wa kimahakama? Swala hili limeundiwa tume, limekaa zaidi ya mwaka, hivi ni kweli uchunguzi bado kukamilika!

Bila shaka EL, NK na IM watafuata kwa matumizi mabaya ya madaraka.


Hapo ndio bongo huwa inanichosha kabisa!!!!!
 
Kama ni kweli basi nitamwaminia JK na nitaamini kuwa hata Kagoda hawaponi.Pia vema sheria ifuatwe na si mwizi kuruhusiwa kujiwekea mdhamana na mali anazotuhumiwa kuiba.Wana JF wenye ukweli wa suala hivi mtujulishe.
 
Du! Haya kweli kuongoza nchi unahitajika kuwa mvumilivu sana... kama kuna vitu ambavyo JK alikuwa under-rated ni issue ya ku-deal na ufisadi na dhuluma... lakini hadi leo aliyofanya yanaonyesha mambo tofauti sana.

Pamoja na hayo... lazima niseme yapo mengi sana ambayo JK na serikali yake could do better kama angeweza kutumia opportunity ya kushinda uchaguzi mkuu by 80% mwaka 2005... ambayo hiyo opportunity will never come twice.
 
Kigogo Richmond kizimbani
Neema Mgonja
Daily News; Tuesday,January 13, 2009 @20:02​

RICHMOND3.JPG

MKURUGENZI wa Kampuni ya kuzalisha umeme ya Richmond Tanzania, Naeem Gire, amefikishwa mahakamani akidaiwa kuilaghai Serikali

MKURUGENZI wa Kampuni ya kuzalisha umeme ya Richmond Tanzania, Naeem Gire, amefikishwa mahakamani akidaiwa kuilaghai Serikali kuwa kampuni yake ina uwezo wa kuzalisha umeme wa megawati 100.

Gire, ambaye anadaiwa kuwashawishi maofisa wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Serikali, anakabiliwa na mashitaka matano likiwamo la kughushi, kulaghai, kusema uongo na kuwasilisha nyaraka bandia.

Mshitakiwa alisomewa mashtaka hayo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, na Mwendesha Mashitaka Boniface Stanslaus, mbele ya Hakimu Mkazi Wariarwandwe Lema.

Mtuhumiwa huyo ambaye alipandishwa kizimbani alasiri, anadaiwa kutenda makosa hayo kwa nyakati tofauti ambapo katika mashitaka ya kwanza anadaiwa kuwa Machi 13, 2006 akiwa na nia ya kudanganya, alighushi hati ya Mwanasheria akionyesha kwamba Mohamed Gire ambaye ni mmiliki wa kampuni hiyo ya Richmond ya Texas, Marekani, alimruhusu kuendesha biashara ya kampuni hiyo Tanzania.

Katika mashitaka ya pili ya kutoa hati za uongo, mshitakiwa anadaiwa kuwa Machi 20, 2006 alitoa hati hiyo ikionyesha kwamba Machi 13 mwaka huo, Mohamed Gire, alisaini hati ikionyesha kuwa mshitakiwa ameruhusiwa kuendesha kampuni hiyo Tanzania.

Akisoma mashtaka ya tatu ambayo ni ya kutoa taarifa za uongo kwa watumishi wa umma, Stanslaus alidai kuwa mshitakiwa huyo Machi 20, 2006 maeneo ya Ubungo alitoa taarifa za uongo kwa ujumbe wa Bodi ya TANESCO akidai kuwa Richmond ina uwezo wa kuzalisha umeme wa megawati 100, na kuwashawishi waipendekeze kampuni hiyo kuanza kazi.

Katika mashtaka ya nne, mshitakiwa anadaiwa kutoa taarifa za uongo Juni, 2006 kwa wajumbe wa timu ya majadiliano ya Serikali na kudai kwamba kampuni ya Richmond ina uwezo wa kuzalisha umeme wa megawati 100 na kuwafanya wafanyakazi hao wa Serikali kuamini hivyo.

Akisoma mashitaka ya tano, Stanslaus alidai kuwa Juni 2006 mshitakiwa alitoa hati za uongo zikionyesha kuwa Mohamed Gire alimwidhinisha kufanya biashara za kampuni ya Richmond Tanzania. Baada ya kusomewa mashitaka hayo, mshitakiwa alikana kuhusika nayo na upande wa mashitaka kudai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.

Upande wa utetezi wa mshitakiwa uliokuwa na wakili Kato Zake uliiomba Mahakama kutoa masharti mepesi ya dhamana kwa mteja wake, hasa ikizingatiwa kwamba ana matatizo ya kiafya na kuwa taratibu za kwenda kutibiwa nje ya nchi zinaendelea.

Zake aliongeza kuwa mteja wake alikuwa akitoa ushirikiano mzuri kwa Polisi, wakati wa upelelezi na kwamba hati ya nyumba na hati ya kusafiria vinashikiliwa na Polisi. Uamuzi wa dhamana kwa mshtakiwa utatolewa leo mahakamani hapo, na alirudishwa rumande.

Wakati huo huo, Neema Mgonja anaripoti kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imekataa ombi la aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Gray Mgonja, aliyewasilisha barua ya maombi ya ruhusa ya kutoka nje ya Makoa wa Dar es Salaam.

Katika barua hiyo, Mgonja ambaye anakabiliwa na tuhuma za kutumia vibaya madaraka aliyokuwa nayo na kusababishia Serikali hasara, aliwasilisha barua ya maombi ya ruhusa ya kwenda kuwaona wazazi wake Kilimanjaro na Arusha ambapo Mahakama ilisema barua haikuandikwa siku anazoomba.

Hakimu mkazi wa mahakama hiyo Hezron Mwankenja, ambaye ndiye anayesikiliza kesi hiyo alisema kuwa maombi hayo yamekataliwa kwa sababu mshtakiwa hakuwa ameandika katika barua hiyo ya maombi kuwa anaomba ruhusa ya siku ngapi, hivyo Mahakama haitoweza kujua itatoa kibali cha siku ngapi. Kuomba kibali cha kutoka nje ya mkoa ni moja ya masharti anayotakiwa kutimiza mshtakiwa pindi anapohitaji kufanya hivyo.

Mgonja, ambaye ni Katibu Mkuu mstaafu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, alifikishwa katika mahakama hiyo kwa tuhuma za kutumia vibaya madaraka aliyokuwa nayo na kusababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh bilioni 11.

Hadi sasa mahakama hiyo imeshatoa vibali vya kutoka nje ya mkoa wa Dar es Salaam kwa washtakiwa wengine wawili katika kesi hiyo ya matumizi mabaya ya madaraka, ambao ni mawaziri wa zamani Basil Mramba na Daniel Yona.

Wakati huo huo, kesi inayowakabili washitakiwa Ajay Somani na Jai Somani ya wizi wa mabilioni ya fedha za Benki Kuu ya Tanzania (BoT) katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), iliahirishwa baada ya upelelezi kutokamilika.

Kesi hiyo ilikuja mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa mbele ya Hakimu Mkazi Victoria Nogwa na iliahirishwa mpaka Januari 22, mwaka huu. Washtakiwa hao ambao ni ndugu wanashtakiwa kwa wizi wa zaidi ya Sh bilioni 2.
 
Mohamed Gire alikuwa mshika mpini tu. Tunalitaka jembe la Richmond!!!! Gire ndo Mbuzi wa kafara au!!!!???

Gire masikiniii!! ni "BANGUSILO TU" lakini utajuaje?? huenda huyo Gire ndo aliyeawapa macho hao vigogo jinsi ya kuiba. Waache watatajana hukohuko, aliyekula nyama au ngozi shauri yao. Damu ya wananchi imemwagika sanaaa kwa ufasadi huu
 
halafu watu wawe makini.. kama inavyosema kuwa "the devil is in the details". Hivi mmejiuliza huyo jamaa ameshitakiwa kwa makosa gani? So, la maana ni kujiuliza "hakushtakiwa kwa makosa gani"... ..

Hii inanikumbusha kesi ya Saileth Vithlani ambaye naye alishtakiwa kwa 'kusema uongo'..
 
Du! Haya kweli kuongoza nchi unahitajika kuwa mvumilivu sana... kama kuna vitu ambavyo JK alikuwa under-rated ni issue ya ku-deal na ufisadi na dhuluma... lakini hadi leo aliyofanya yanaonyesha mambo tofauti sana.

Pamoja na hayo... lazima niseme yapo mengi sana ambayo JK na serikali yake could do better kama angeweza kutumia opportunity ya kushinda uchaguzi mkuu by 80% mwaka 2005... ambayo hiyo opportunity will never come twice.


Kijana mzee wa ikulu yaaminika ni mwoga balaa.
Tusubiri maana tunayasikia mambo yakisema kila kesi inayomtuingiza EL hatiani inakwepeshwa ili tu asisimame kwenye mbao!

Ndani zaidi yasemekana ni maagizo ya JK wa leo. EL asiguswe!
 
Hao waliokuwa wakilishi wa serikali walikuwa wapi hadi walaghaiwe kiasi hicho, ni akina nani?

Yale mabilioni ambayo Richmond walikuwa wakilipwa yalikuwa yaenda kwenye akaunti ya nani?
 
- Ni lazima kutoa credit inapokuwa due, hapa ninampa rais Kikwete heshima kubwa sana. Hapa JF ndipo ukweli wa ufisadi wa Richimonduli ulipoanzia kufichuliwa rasmi, na kuna tuliolala macho kulifanyia kazi taifa letu, sasa matokeo ndio haya yameanza kuonekana,

- Tumesikia mengi sana kuhusiana na nguvu walizonazo mafisadi katika taifa letu hasa wa Richimonduli, na kama kawaida hapa ya JF wananchi karibu wote hapa tunashuhudia one of the untouchables akifungua njia ya Kisutu, lakini kama kawaida kuna ma-intellectuals tayari wanaotaka kutuambia kua sio kweli tunayoyaona na kwamba eti Richimonduli itaishia na huyu Msomali tu, hivi mbona jana na juzi hamkutuambia kuwa leo kuna Msomali atatinga since mnaonekana kujua sana kinachoendelea kuliko hata serikali yenyewe? Eti mlijua lini kuwa serikali itamfikisha Msomali tu kuhusiana na Richimonduli? Mbona hamkutuambia mapema?

- I mean wananchi tunaona mbili, wengine mnatuambia ni tatu sasa tuambieni basi kesho ni zamu ya nani? au who is next? Yaani rais na serikali yake anaweza kuwa mjinga kiasi gani hasa cha kudiriki kumpeleka Msomali bila washirki wake?

Ninampongeza rais wa jamhuri kwa hili la kumfikisha huyu fisadi la Richimonduli kwenye sheria, na ninaamini kuwa wengine wote wako njiani, yaani kuanzia Mary Kejo, Msabaha, Karamagi, Lowassa, Rostam, Manji, Mwakapugi, na wengineo, tunaamini kwamba huyu Msomali ni mwanzo tu! Hapa Muheshimiwa sana Rais tuko pamoja, na Mungu Akubariki, lakini tunasubiri na wengine pia.

Mungu Aibariki Tanzania!
 
Quote:
"Akisoma mashtaka ya tatu ambayo ni ya kutoa taarifa za uongo kwa watumishi wa umma, Stanslaus alidai kuwa mshitakiwa huyo Machi 20, 2006 maeneo ya Ubungo alitoa taarifa za uongo kwa ujumbe wa Bodi ya TANESCO akidai kuwa Richmond ina uwezo wa kuzalisha umeme wa megawati 100, na kuwashawishi waipendekeze kampuni hiyo kuanza kazi.

Katika mashtaka ya nne, mshitakiwa anadaiwa kutoa taarifa za uongo Juni, 2006 kwa wajumbe wa timu ya majadiliano ya Serikali na kudai kwamba kampuni ya Richmond ina uwezo wa kuzalisha umeme wa megawati 100 na kuwafanya wafanyakazi hao wa Serikali kuamini hivyo."



Hii mbona inasukwasukwa kana kwamba hao so called "Watumishi wa Umma" ni victims na sio party to the corruption scandal?...
 
JK aamua kutumia political platform ya 2010. Sioni sehemu yeyote ya kumsifia yeye na serikali yake.haya yote ni mazingaumbwe. Tatizo lilianzia kwenye Tender. Ni jinsi gani hawa mabwana walipewa tenda ya kufunga vifaa vya dharura.Na je watoa tender walitumia vigezo gani kutoa kazi. Sasa hizi ngonjera za kwamba kampuni ilisema uongo ni kipi kilitangulia tenda au uongo wa kampuni ??? Wote wakamatwe sio tulishane peremende moja baada ya nyingine.......

"Mr Mohammed Gire, (750,000 shares), a Tanzanian born businessman currently living in the US, is the majority share holder while Mr Naeem Gire, who is believed to be his blood relative, holds the rest of 250,000 shares to make a total of a million shares. After flying in the generators, the firm’s financial director, Mr Zahoor Gire, announces that generation was expected to commence in December 2006, at the latest."

Nyangumi yupo Houston Texas katulia anatucheka. kesha kula bingo.
 
JK aamua kutumia political platform ya 2010. Sioni sehemu yeyote ya kumsifia yeye na serikali yake.haya yote ni mazingaumbwe. Tatizo lilianzia kwenye Tender. Ni jinsi gani hawa mabwana walipewa tenda ya kufunga vifaa vya dharura.

- Kesi ndio kwanza imeanza, sasa dawa ni kusubiri kuona inakokwenda na itakakoishia, kama una ushahidi kama unavyonyesha hapa, basi wakimbizie tu kule Sheria pale juu ya foreign, ndiko wako mawakili wa serikali wanaosiamia hizi kesi.

- Bado ninampongeza rais kwa hili la kuwafikisha mafisadi kwenye sheria, na tunajua kwua ni innocent until proven otherwise mbele ya sheria.

Sasa by the way who is next huko Kisutu mkuu maana kama unajua ya platform za 2010 basi unajua mengi sana kuhusu hizi kesi, au?
 
Ninawaheshimu sana watoa mada wa JF kwani mmeipeleka serikali kona. Field marshal , wako wengi wanakuja.Ila Kwangu mimi hii ni hadaa.Tusubiri tuone.Hakuna hata kimoja kimeguswa vizuri? kwanini tusishangae amri ya kukamata au kuto kamata inatoka ikulu.Nini kinakwepa na ni akina nani wanalindwa.watuhumiwa wote wanaendelea na kazi hata waliotumia madaraka vibaya bado wanashuhulika kwenye shughuli za serikali na siasa.Kwanini pawepo na special group kwenye haki na sheria.Utawala unafanya kazi kwa pressure kutoka nje ya utawala sio msukumo ndani ya utawala. Ni ubatili mtu.Hifadhi haya utayakumbuka.
Sakata la RDC lipo wazi tunaletewa usanii tunashangilia...........Sheria za makosa ya jinai zipo wazi kuanzia inapoaanza .Huwezi rukia tawi halafu ukasema nimekata mti. i dont buy it.
 
Hivi kama Gire anafikishwa mahakamani kwa kosa la udanganyifu na mkataba hewa, kwa nini basi Serikali na Tanesco bado zinailipa Dowans na kuna kesi Paris ya madai liyofunguliwa na Dowans dhidi ya Serikali ya Tanzania na Tanesco?

Does this make any sense?
 
Back
Top Bottom