Euphransia
JF-Expert Member
- Jan 26, 2017
- 937
- 778
Nachukua nafasi hii kumpongeza Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Kwa juhudi kubwa anazozifanya katika Wilaya yake hasa kuhusiana Na migogoro ya Mashamba.Kwa kuwa Manispaa ya Ubungo ni mpya ni wakati sahihi Kwa Viongozi wake kuanza kuupanga Mji mapema kabla haujaharibika.Manispaa ya Ubungo ina Mashamba mengi Na makubwa.Ni wakati muafaka Mashamba hayo yakatwaliwa Na Serikali yakaandaliwa Michoro ya mipango miji Na kupimwa Viwanja badala ya kuyaacha Na kuwafanya wenye Mashamba wakayakatakata Na kuwauziwa watu bila kuwa Na Mpango Na kusababisha ujenzi holela.Wakati umefika Kwa Mkurugenzi wa Ubungo na Timu ya Watalaam wako kupitia Madiwani wako kuibadili Ubungo kuwa ya Viwanja badala ya Mashamba.