Kwanini wamiliki wa viwanja wanalazimishwa kuwalipa fidia wenye mashamba yaliyo hukuliwa na Manispaa ya Sumbawanga?

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Feb 19, 2021
1,336
2,000
Mwaka 2004 Manispaa ya Sumbawanga ilichukua mashamba ya wananchi huko kizwite na kufanya uthamini na kuwalipa fidia wahusika.

Baadae ikapima viwanja na kuviuza kisha kuvimilikisha kwa walionunua na kuwapatia hati milki za miaka 66. Ghafla kumeibuka wimbi la watu wanavamia hivyo viwanja na kudai wazee wao walifariki kabla ya kulipwa fidia hivyo wanadai fidia.

Maafisa ardhi badala ya kujiridhisha kuwa wanaodai fidia ndio kweli wenye mashamba na pia kama kweli wazazi wao ndio walikuwa wenye hao mashamba na hawakulipwa fidia mwaka 2004 kwa kuangalia majedwali ya fidia ambayo yapo ofisini kwa mkuu wa wilaya wao wameamua kuwalazimisha wamiliki wawalipe fidia hao wanaodai.

Kama manispaa ndio iliyochukua hayo mashamba suala la fidia ni la manispaa na sio la wamiliki manispaa kama kweli hao wanaodai walisahaulika basi manispaa ni wajibu wao kuwalipa fidia isiwatwishe mzigo wamiliki.
 

babu bulicheka

JF-Expert Member
Mar 26, 2021
449
1,000
Hili linaenda kutokea Dodoma.

Nkuhungu broad acre ilishapimwa na kumilikishwa leo hii Jiji linaingia na kupima na kuwaingiza Wavamizi na kuwatambua Mwenye shamba unaambiwa utahamishwa sehemu ingine.

Hivi nisheria ipi inayo muhamisha mmiliki na mvamizi kumilikishwa Uvamizi wake.

Gharama za uhamisho anakulipa nani.

Jiji la Dodoma jitafakarini sana tamaa mbaya!
 

SN.BARRY

JF-Expert Member
Oct 12, 2012
3,925
2,000
Dah, halafu hapo ofisini/ halmashauri ya manispaa utakuta kuna wasomi kama kumi wenye Masters ila wanashindwa kutatua hili tatizo hadi Lukuvi aje. Wanafuga tu mavitambi utadhani hapo ofisini ni kliniki ya wajawazito. Nchi ngumu sana hii.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom