DOKEZO Ubadhirifu unaofanyika kwenye shule zenye vituo vya elimu maalumu jiji la Mwanza

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

rsinangila

New Member
Nov 28, 2023
3
1
Hbr za asbh ndg zangu wanaJF,

Naomba kuingia kwenye mada moja kwa moja kuhusu hili suala la vituo maalum mkoa wa Mwanza hususan mwanza jiji.

Ndg wanaJF vituo hivi vya elimu maalumu kwa Mwanza jiji limekuwa ni vituo haswa vya walimu wakuu.

Ikumbukwe kuwa kila mwezi Serikali hutuma pesa kwa kila kituo ili kuweza kununua chakula kuanzia chai hadi chakula cha mchana kwa wanafunzi wenye uhitaji maalum ambao ni pamoja na viziwi, wasioona na wenye mtindio. Lakini imekuwa ni tofauti sana na maelekezo ya serikali kuhusu matumizi ya jinsi fedha hizi zinavyotumika.

Kisheria fedha inapofika kwenye kituo kila mwezi ni lazima kila kituo chenye watoto wenye mahitaji maalumu walimu wanaohusika lazima wakae kikao kupitisha bajeti ya chakula kinachotakiwa kuliwa kwa mwezi husika lakini imekuwa ni tofauti kabisa na maelekezo yanayotolewa maana walimu wakuu ndio wamekuwa wakizihodhi fedha hizo na kuzitumia wao watakavyo na hata bajeti tena haziandaliwi kwa maana walimu husika hawashirikishwi kabisaaaa. Matokeo yake watoto wenye mahitaji maalum wamekuwa wanakosa chakula.

Nimefanya uchunguzi wa sakata hili kwa shule za msingi Bugando, Buhongwa, Iseni, Igoma na Mirongo hali ni ile ile.

Nimeongea na baadhi ya walimu wa shule hizo wamethitisha ni kweli wao huwa hawashirikishwi kwani walimu wakuu wamekuwa ni wababe kupita kiasi maana ukifutilia tu maslahi yake anakufanyia figisu unahamishwa kwa maana baadhi ya maofisa wa jiji la Mwanza wamekuwa wanashirikiana na wakuu wa shule hizi zenye vitengo kula pesa za watoto hawa wenye mahitaji maalumu.

Afisa elimu wa elimu maalumu dada yangu Zakia Ahmed kwanini hufuatilii hili ilhali na ww ulikuwa mwalimu wa elimu maalumu iseni kabla hujawa bosi. Wakati upo mwalimu wa kawaida ulikuwa unapenda sana haki ila sasa hivi kwa nini hutaki kufuatilia?

Umekuwa afisa wa mambo ya likizo za walimu badala ya jukumu lako la uafisa elimu maalumu. Fuatilia mashuleni ili kujua ukweli usione nakusingizia ww nenda mashuleni ongea na mwalimu mmoja mmoja tena bila mwalimu mkuu kuwepo hapo utajua ukweli niyasemayo. Mashuleni kuna ratiba ya chakula kwa kila shule ila ratiba haifuatwi kwa kuwa chakula ni cha magumashi!!!

Waonee huruma hawa watoto na onea huruma pesa za wananchi zitolewazo na serikali. Usiwaonee huruma hawa walimu wakuu wenye vitengo wanaokula pesa hizi za watt. Kwa upande mwingine huwa naona ni bora pesa hizi zisingetolewa kabisaaaa maana haziwafikii walengwa.

Mkurugenzi wa jiji ndg Kagurumjuli fuatilia hili kwani jiji la Mwanza wewe walijua nje ndani kwani ushawahi kuwa afisa elimu wa jiji hili hivyo kila kona unajua nakuomba fuatilia pesa hizi zinazoliwa na walimu wakuu wako wa shule zenye vitengo.

Naomba kuwasilisha.
 
Ni vyema JamiiForums mkawa mnafanya uchunguzi kwanza wa taarifa kama hizi kabla ya kuzipost hewani.

Vipi ikibainika hakuna ukweli wowote wa tuhuma hizi, hamuoni mtakuwa mnaharibu credibility yenu kama sehemu sahihi ya mtu kupata habari.

Hatuwezi jua, huenda mdau akawa na ugomvi au bifu na miongoni mwa hao maafisa au mwalimu wake mkuu.

Kwa uelewa wangu, tenders zote za serikali huwa zinatolewa kwa wazabuni. Wazabuni ndiyo huwa wanakuwa na kazi ya kuhudumia mfano ishu ya chakula mashuleni.

Sasa sote tujiulize Je, ishu ya chakula kuhusu shule hizo hufanywa na wazabuni au serikali hutoa pesa cash kwa wakuu wa shule?

Mdau anadai ameongea na walimu wa shule hizo husika, je Anaushahidi wa mazungumzo yao?. Bilashaka mdau atakuwa ni mwalimu pia.
 
Back
Top Bottom