Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, aamua kuvuruga uandikishaji, Dr. Slaa aingilia kati Kuokoa jahazi

Chademakwanza

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
6,346
1,871
BVR Arusha.

Mkurugenzi wa jiji la Arusha ameendelea kushupaa na kukandamiza demokrasia Jiji la Arusha.Itakumbukwa kuwa jana viongozi wa CHADEMA yaani Mbunge,madiwani,na wenyeviti wa serikali za mitaa waliandamana jana kupinga uhuni unaofanywa na mkurugenzi na NEC wakati huu wa kuandikishwa kwa BVR kwa wakazi wa Arusha awamu ya kwanza.

Miongoni mwa madai ya CHADEMA yalikuwa ni
1:Muda wa vituo kuwa wazi yaani iwe saa moja asubuhi hadi saa mbili usiku
2:Kuongezwa kwa mashine za BVR kwenye maeneo yenye watu wengi
3:Wananchi kuandikishwa kwa mujibu wa sheria yaani kwa mipaka ya kata na sio mitaa
4:Kukomeshwa kwa vitendo vya ubaguzi wa kikabila dhidi ya wakazi wa Arusha
5:Kuongezwa siku za uandikishaji

Mkurugenzi huyu aliahidi kuyafanyia kazi ila cha ajabu ni kuwa jana kituo cha Longdong kilivamiwa na askari na kufungwa saa kumi na mbili kinyume cha sheria.

Kama dhihaka kwa watu wa Arusha mkurugenzi ameongeza mashine nne tu kata ya sokon 1 badala ya mashine 20,kata hii ina wapiga kura 24 000 hadi jana walikuwa wameandikishwa wapiga kura 4,000tu na ni siku ya tatu.Je kwa siku nne NEC itaweza kuandikisha wapiga kura 20,000?

Kata ya Osunyai Jr ina wapigakura 19,500 hadi jana walikuwa wameandikishwa 3200 bado 16,000.

Taarifa za ndani ya NEC pamoja na mkurugenzi Id Juma zinasema kuwa wamepanga kuandikisha watu wachache maeneo ya mijini kwa njia ya kuikoa ccm na anguko kuu.Jiji la Arusha lina jumla ya wapiga kura 300,000(Laki tatu).

Hadi jana siku ya tatu kwenye awamu ya kwanza ni jumla ya wapiga kura 12,000 tu walikuwa wameandikishwa kwenye jumla ya vituo 56 kwenye awamu hii.

Ni wazi Idd Juma anatumika na anakubali kutumika kutokana na hofu ya mashaka hasa ikizingatiwa anastaafu mwakani
 
Tume hii ya CCM haiko huru kamwe.Inapokea maelekezo toka kwa mshindani mmojawapo kwenye uchaguzi.Wana Arusha katika hili ni vizuri mkaungana wote bila kujali itikadi zenu.
 
Sasa badala wakapange foleni!! Wanaandamana!! 😱😱
 
Sasa badala wakapange foleni!! Wanaandamana!! 😱😱

Watu wanakaa kwenye foleni kuanzia asubuhi halafu inafika jioni hujaandikishwa Kisha polisi wanafunga kituo kwa maelekezo ya mkurugenzi! Hatuwezi kuendelea hivi. Damu zitakazomwagika hakika huyu mkurugenzi hataishi kwa Amani!
 
Tume hii ya CCM haiko huru kamwe.Inapokea maelekezo toka kwa mshindani mmojawapo kwenye uchaguzi.Wana Arusha katika hili ni vizuri mkaungana wote bila kujali itikadi zenu.
Mbunge wa Arusha mjini ni hovyo kabisa. Mbona mikoa mingine wananchi hawapotezi muda kwa maandamano? Arusha mnapaswa kumpuuza Lema kama kweli mnataka maendeleo. Watu mnalilia muda hautoshi lakini hata huo muda mchache hamuutumii mnabaki kuadamana hovyo.
 
Watu wanakaa kwenye foleni kuanzia asubuhi halafu inafika jioni hujaandikishwa Kisha polisi wanafunga kituo kwa maelekezo ya mkurugenzi! Hatuwezi kuendelea hivi. Damu zitakazomwagika hakika huyu mkurugenzi hataishi kwa Amani!
Waliokaa kwenye foleni ndiyo hao wachache walioandikishwa, mnalalamika ndo muda wote mnarandaranda mtaani kwa maandamano.
 
Nyie potezeni muda kwa kuandamana badala ya kujiandikisha.

Kupoteza muda Ni pale unapodamka kituoni, mpo zaidi ya elfu mbili Kisha wanaandikishwa watu arobaini na Sana, mliobaki mnaambiwa mje kesho! Huko ndiko kupoteza Muda!
 
Kupoteza muda Ni pale unapodamka kituoni, mpo zaidi ya elfu mbili Kisha wanaandikishwa watu arobaini na Sana, mliobaki mnaambiwa mje kesho! Huko ndiko kupoteza Muda!
Ila kuandamana ni kutunza muda siyo?
 
Toka kwenye keyboard uje field ndio utaelewa.
Niko hapa hapa arusha, Sanawari unafikiri niko mbali, nawaona mnavyopelekeshwa na Lema kama gari bovu. Huyu Lema nawajulia sana utafikiri mnabwia unga bwana.
 
Siku za nyuma nilileta taarifa hapa kuhusiana na jaja ya ccm kwenye BVR ili kuwakomoa wapinzani.cha kusikitisha watu walinidhihaki hapa.

Ila ki ukweli kama zoeza bado halijakufkia uwezi kuona kero zilizopo,kuna kero zaidi nyingi sana ya hizi zinazoandikwa umu.!!watu wengi sana wameachwa bila kuandikishwa hasahasa kwnye ile mitaa inayoongozwa na wapinzani.!
 
Back
Top Bottom