GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 63,587
- 127,935
Mkurugenzi wa shirika la kijasusi nchini Marekani CIA amemuonya rais mteule wa Marekani Donald Trump kwamba kusitisha makubaliano ya mpango wa nyuklia na Iran itakuwa ''hatari na upuuzi''.
Katika mahojiano na BBC ,John Brennan pia alimshauri rais huyo mpya kuwa na tahadhari kuhusu ahadi mpya za Urusi akiilaumu Moscow kwa mateso yanayoendelea nchini Syria.
Katika kampeni yake , Trump alitishia kufutilia mbali mpango wa mnyuklia nchini Iran mbali na kuashiria kufanya kazi kwa karibu na Urusi.
View attachment 441451
Trump alaumu wanahabari kwa utata.
Brenan atajiuzulu mnamo mwezi Januari baada ya kuhudumia shirika hilo kwa kipindi cha miaka minne.
Katika mahojiano ya kwanza na vyombo vya habari vya Uingereza, Brennan alitaja maswala kadhaa ambapo alisema kuwa utawala mpya unafaa kuzingatia kwa busara na heshima, ikiwemo lugha inayotumiwa kuhusu ugaidi, uhusiano na Urusi, mpango wa kinyuklia wa Iran na vile siri za shirika hilo hutekelezwa.
Chanzo: BBC
Nadhani Marekani haijawahi kupata CIA Director very ' bogus ' kama huyu wa sasa Mr. Brennan. Ni Mtu asiyeeleweka nini anachokifanya na amekuwa pia akimchanganya mno hata Rais Obama kwa ' taarifa ' zake kadhaa za ' Kipuuzi ' ambazo kuna muda zilitaka ' kuigharimu ' Marekani hasa Kijajusi na Kijeshi. Kizuri tu ni kwamba mwakani mwezi January anaondoka na natumai US elect President Donald Trump anamteua Mtu ' makini ' na ' mahiri ' sana ili aweze kuitendea haki hiyo nafasi. Brennan hawezi kukwepa ' Ujasusi ' wa ' kutukuka ' ambao tayari Urusi kupitia ' Wataalam ' wa Rais Putin wameshaifanyia nchi yake ya Marekani na ' ugumu ' ambao sasa Marekani wanaupata na kukutana nao huko Syria ambao kwa kiasi ' kikubwa ' tu unaratibiwa na Urusi ndiyo umeichanganya mno Marekani kwani japo wao ' wanajigamba ' kuwa wapo vizuri ' Kijeshi ' na ' Kijasusi ' ila ukweli kwa sasa haupo hivyo na Warusi wameweza ' kupenyeza ' Watu wao wengi sana nchini Marekani tena katika Idara zao ' Nyeti ' kama NSA, CIA kwenyewe na hata PENTAGONE katika ' ngome ' yao kuu ya Kijeshi. Putin sasa baada ya kupata ' info ' zao zote sasa ameanza kupambana nao katika Psychological War huku akiwadhoofisha kwa ' kuwachokoza ' huko Syria.