Mkurugenzi na mbunge watofautiana kuhusu wamachinga

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,174
Mkurugenzi na mbunge watofautiana kuhusu wamachinga Saturday, 15 January 2011 08:41
wenje.jpg
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana (Chadema),Ezekiel Wenje

Frederick Katulanda, Mwanza

SIKU moja baada ya Mbunge wa Jimbo la Nyamagana (Chadema) Ezekiel Wenje kutaka wafanyabiashara ndogondogo (wamachinga) watengewe eneo maalumu ili waendelee na biashara katikati ya jiji, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza amewataka kuondoka mjini kabla ya Januari 17 mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana, mkurugenzi wa jiji hilo Wilson Kabwe amesema wamachinga wote wanatakiwa kuondoka haraka katika maeneo ya katikati ya jiji ambako wamekuwa wakifanyia biashara na kwenda katika maeneo maalumu yaliyopangwa kabla ya siku ya mwisho.

“Atakayekutwa akiendelea kufanya biashara baada ya siku ya mwisho atakamatwa na kuchukuliwa hatua kali kutokana na kuvunja sheria ya mipango miji na. 8/ 2007, sheria ya afya ya jamii na. 1/2009 na sheria ndogo za jiji la Mwanza ya mwaka 2000 na mwaka 2010 (GN 359 na GN 312)” lilieleza sehemu ya tangazo hilo.

Wafanyabiashara wameruhusiwa kufanya biashara zao katika maeneo maalumu ambayo yameidhinishwa na jiji yaliyoko Kiloleni, Buzuruga, Kitangiri, Nyegezi, Mlango Mmoja na Mabatini.

Tangazo hili limekuja siku chache baada ya kauli ya mbunge wa Nyamagana,Wenje kudai kuwa hakubaliani na mpango wa kutenga maeneo ya biashara nje ya mji ambako hakuna makazi kwa ajili ya wafanyabiashara hao na kutaka uandaliwe mpango mpya.

Wenje akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika juzi katika viwanjwa vya Ngokozi jijini Mwanza, alisema kuwa katika kipindi cha miaka zaidi ya 10 , halmashauri ya jiji ilipanga maeneo ya kufanyia biashara machinga katika maeneo ya nje ya mji kwa lengo la kuufanya mji kuwa safi, lakini wamachinga hawakuwahi kuyatumia maeneo hayo, basi mpango huo ulikuwa haufai.

Alisema, “Mpango za zamani wa kuwaondoa machinga ulikuwa na nia nzuri ambayo naiunga mkono, lakini kama maeneo ambayo yalitengwa huko nje ya mji hayatumiki, sasa kuna haja ya kubadili mpango huo na kuangalia mpango mpya ambao utakuwa na manufaa zaidi kwa jiji na wamachinga wenyewe.”

Alikaririwa akisema yeye akiwa mbunge amependekeza kutumika mpango wa kisasa ambao unatumika katika nchi za nje ambapo serikali kuwa kuzingatia umuhimu wa wamachinga kama hawa umekuwa ukitenga maeneo maalumu na kuweka muda wa kufanyia biashara ambao umekuwa ukizingatiwa na wote.

Licha ya tangazo hilo kutolewa wamachinga wameonekana kukaidi agizo hilo na kuendelea na biashara zao huku wakisema, hawako tayari kuondoka katikati ya mji kutokana na kuwa maeneo ambao wamekuwa wakitakiwa kufanyia biashara hayana tija kwao.

Akizungumza na gazeti hili mmoja wa machinga hao aliyejitambulisha kwa jina la John Samwel alisema wameshangazwa na hatua hiyo ya halmashauri kutambua uwepo wa sheria leo wakati wao wenyewe waliwaruhusu kufanyia biashara maeneo hayo wakati wa uchaguzi na kuhoji sheria zilikuwa likizo ama kwa vile Chama Cha Mapinduzi kilikosa ushindi ndiyo sababu ya wao kutimliwa.

"Atakayekutwa akiendelea kufanya biashara baada ya siku ya mwisho atakamatwa na kuchukuliwa hatua kali kutokana na kuvunja sheria ya mipango miji na. 8/ 2007, sheria ya afya ya jamii na. 1/2009 na sheria ndogo za jiji la Mwanza ya mwaka 2000 na mwaka 2010 (GN 359 na GN 312)" lilieleza sehemu ya tangazo hilo.

Ni jukumu ya serikali ya Chadema ya jijini Mwanza kuzifanyia marekebisho sheria zote kandamizi dhidi ya raia ili kujenga utawala bora na sikivu kwa mahitaji halisi ya jamii....................................
 
Back
Top Bottom