Mkurugenzi Mtendaji BP ashtakiwa mahakamani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkurugenzi Mtendaji BP ashtakiwa mahakamani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Feedback, Aug 18, 2011.

 1. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #1
  Aug 18, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imemshtaki katika Mahakama Kuu ya Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya BP, Engelbert Kongolo ikiiomba aeleze kwa nini asifungwe kwa kukataa kufuata amri ya utii (Compliance Order) iliyotolewa na mamlaka hiyo.

  Ewura ilifungua jana kesi hiyo namba 130 ya mwaka huu, huku mamlaka hiyo ikiomba mkurugenzi huyo alipe gharama za kesi hiyo.Kesi hiyo ilifunguliwa na Ewura kupitia wakili James Kabakama wa kampuni ya GRK Advocates.

  Akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam hivi karibuni, Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Haruna Masebu alisema Katika uamuzi wake wa Bodi ya Wakurugenzi uliofikiwa Agosti 9 mwaka huu, “Imeagiza mkurugenzi mkuu na mwenyekiti wa BP kufikishwa mahakamani kwa kupitia kwa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Jinai (DPP).”

  Kabla ya kufikia hatua hiyo ya kuishtaki BP, Ewura ilikuwa imetoa amri kwa kampuni nne zinazosambaza mafuta kurejesha huduma hiyo mara moja huku ikizitaka kujieleza, kwa nini zisichukuliwe hatua za kinidhamu kwa kushindwa kutimiza wajibu wao kwa mujibu wa leseni zao za biashara. Ziligoma zikipinga punguzo la bei ya bidhaa hiyo iliyokuwa imetangazwa na mamlaka hiyo.

  Kampuni hizo ni pamoja na BP ambayo Serikali inamiliki nusu ya hisa pamoja na Engen, Oil Com na Camel. Tatu zilitii lakini BP ilikaidi kitendo ambacho kiliifanya Ewura kusitisha leseni yake ya biashara kwa miezi mitatu.

  Katika uamuzi huo wa kusitisha leseni, vituo vyote vya rejareja vyenye nembo ya BP viliruhusiwa kuuza mafuta kwa kununua bidhaa hiyo kwa wafanyabiashara wengine wa jumla.

  Source: Mwananchi
   
 2. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #2
  Aug 18, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,785
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  kama kuna jambo ambalo limenisumbua kuelewa na mpaka sasa naamini kwamba serikali yetu ina matatizo makubwa zaidi kuliko sisi wananchi tunavyohisi ni sakata la BP na EWURA. hii ni kampuni ambayo serikali kwa niaba yetu ina hisa 50% lakini mpaka sasa hatujamsikia msemaji wa serikali yetu akituelezea sisi wenye hisa nini kilitokea!!! juzi nimesoma ktk gazeti la Tanzania daima BP wakieleza kwamba baada ya bei elekezi za EWURA kutangazwa,mtendaji mkuu wa BP Tanzania aliwasiliana na wenye hisa,ambao ni serikali ya Tanzania na hao wengine akiwaambia kama watauza mafuta kwa bei hiyo kampuni itapata hasara,serikali yetu haikujibu. na mpaka sasa hatujasikia msemaji wa serikali akitueleza ni nini kinachoendelea BP.
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Aug 18, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,396
  Trophy Points: 280
  aah wapi? ni miongoni mwa kesi zisizo na kichwa wala miguu. Wanawashtaki kwa kosa gani? well the burden of proof iko kwa serikali na kwa kweli ni usumbufu tu.
   
 4. n

  niweze JF-Expert Member

  #4
  Aug 18, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kweli serikali ya Tanzania ni uewendawazimu tupu. Hivi niulize hapa, kama serikali ya Tanzania inamiliki half ya hii kampuni ya BP si maamuzi ya kutouzwa kwa hii bidhaa yalikubaliwa na waendeshaji wa kampuni ambao ni BP na serikali ya kikwete. Ujinga tunaoona hapa ni kama ule wa EPA hakuna tofauti yeyote ile.

  Hii inadhirisha wazi kumba haya makampuni yanayojiiingiza Tanzania kama investors wame-prove theory ya mafisadi wa Tanzania na sio lolote lile kwamba wanatoka nje ya nchi. Hapa nataka nielewe zaidi nani anafanya maamuzi ya uendesheaji wa BP katika shughuli za kila siku za kampuni at the same time serikali inatakiwa ijue kila kitu kinachoendelea ndani ya BP. Maybe sijaelewa umiliki wa hii kampuni Tanzania ina hisa kiasi gani, hata kama ni asilimia 20 lazima someone inside the government anajue kilichotokea. Any business person will tell you that the government of Tanzania and their joint ventures isn't business, pure mafia style. Hakuna kitu hapa ni uhuni wa kikwete na mtoto wake tu.

  Hapo mahakamani tutaona kama hii kesi itafika kokote pale au haikufutwa kimya kimya bila watanzania kujua kama dowans na richmond zilivyopotea. Tangu lini ccm wakakubali kushitakiana? Siku zote open justice system lazima docs zote zipelekwe mahakamani na hasa hii joint venture lazima details in contracts ziwe open, I doubt kikwete na ridhwani watakubali hili litendeke.

  Tatizo jingine halieweki ni hili kama serikali ya Tanzania imejisajiri katika word trade organization tangu lini serikali ikafanya maamuzi ya kampuni binafsi? Hakuna mandate yeyote ile yakulazimisha kampuni binafsi kuuza bidhaa au kutouza bidhaa kwenye market. Serikali ya kikwete inachokifanya na kukwepa ni kuishitaki BP na hao mafisadi wenye hisa kwa kosa la ku-manipulate prices. Kama wakienda kwenye hii angle, they have a wall to break and how kikwete na wanasheria wao empty head wataweza kupeleka hii kesi mahakani na kushinda? Wanasheria wa serikali ya kikwete ni bora watoto wa shule ya vidudu ni incompetent kama ccm ilivyo, all they care is pocketing money...

  "Wanasheria wa ccm prove us wrong again"
   
 5. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #5
  Aug 18, 2011
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,383
  Likes Received: 3,341
  Trophy Points: 280
  Nyie subirini kidogo mtakujakusikia EWURA imeshindwa kesi na inadaiwa matrillion ya shillingi kwa hasara waliyoisababishia BP na hatimaye hako ka-NGO ka-EWURA kufilisiwa na kufutwa kabisa.
   
 6. Mamaya

  Mamaya JF-Expert Member

  #6
  Aug 18, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 3,726
  Likes Received: 448
  Trophy Points: 180
  Hamna kitu hapo.serikali haiwez kujishtaki yenyewe maana ni part's of that company,na kwa kuwa ni share holder na inamiliki nusu ya shares,ni part of managment iliyochukua uamuzi wa kutokuuza mafuta.hii ni sarakas nyingine yaserikali yetu.
   
 7. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #7
  Aug 18, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Serikali ni Wendawazimu
  Ewura ni Wendawazimu

  Wanajaribu to pull a stunt which is absolutely stupid to me.
   
 8. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #8
  Aug 18, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Ujinga mwingine huu hapo unamfungulia mashtaka kwa kutaka kufuata amri ya utii (Compliance Order) au unamfungulia mashtaka ili alipe gharama za kesi???
   
 9. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #9
  Aug 18, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,076
  Likes Received: 7,566
  Trophy Points: 280
  Amri ya utii??? Huyo jamaa si mtumishi wa serikali wala si askari, hakuna suala la utii hapo.
  Kwa hiyo kesi title mimi naona tayari kesi imeisha na serikali imeshindwa
  Kwanza amri yenyewe haifuatiki wala kutkelezeka na kitendo cha serikali kuruhusu bei kuongezeka ni tena ndani ya wiki moja hiyo ni sehemu ya utetezi atakaoutumia jamaa katika kesi ile, achilia mbali kuporomoka kwa shilingi na nyinginezo......so the whole thing about going to the court is just a part of so many shows we have already seen and yet to be seen.
   
 10. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #10
  Aug 18, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ...Hivi nani msemaji wa serikali hii lege lege??? Mi naona kila mtu anajisemea tu hovyo hovyo utadhani wako kwenye klabu ya pombe ya mnazi..
   
 11. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #11
  Aug 18, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,793
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  nakuhakikishia hakuna mtendaji wa serikali anayejua kuwa hizo hisa zetu 50 % zina uhalisia gani kwa sasa!nakumbuka mramba au mkulo waliwahi kusema bungeni kuwa hiza za BP na NBC za serikali zitauzwa ktk IPO kisha DSE mpaka leo kimya!
   
 12. Ben Mugashe

  Ben Mugashe Verified User

  #12
  Aug 18, 2011
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 940
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Naomba kuhuliza eti " hii movie ni ya kihindi or kinigeria"
   
 13. s

  smz JF-Expert Member

  #13
  Aug 18, 2011
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 251
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hii move bwana inatatanisha. Waigizaji wamechanganyikana, wa- Nigeria na Wahindi. Sisi tusubiri mwisho wake ndo tutajua nani alikuwa starling, Mhindi au Mnigeria. Stay tuned.
   
Loading...