Mkurugenzi mkuu mfuko wa taifa wa bima ya afya ni mnyanyasaji na muonevu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkurugenzi mkuu mfuko wa taifa wa bima ya afya ni mnyanyasaji na muonevu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mkereketwakamil, Sep 25, 2010.

 1. m

  mkereketwakamil Member

  #1
  Sep 25, 2010
  Joined: Aug 27, 2010
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tumesikia malalamiko mengi kuhusu mfuko wa taifa wa bima ya afya unavyotumia vibaya pesa za wanyonge lakini watu wanasahau kuwa hata ndani ya ofisi ile kunamalalamiko mengi ya wafanyakazi na manyanyaso mengi ambayo wafanyakazi wanafanyiwa na yule fisadi mkurugenzi mkuu wao. Anaroho mbaya na anaupendeleo wa waziwazi kwa wafanyakazi. Hafai kuwa pale ameongoza shirika lile toka linaanza mpaka imefikia anaongoza watu na kutoa maamuzi kama vile ofisini ni nyumbani kwake.

  Amewajengea wafanyakazi nidhamu ya woga hata pale wanaponyimwa haki zao wasiseme, kwasababu wakisema tu anawachukulia hatua hata bila kuwaita na kusikiliza upande wao. Vyombo vya habari tusaidieni kuweka hili wazi ili viongozi wetu wa serikali watusaidie kumng'oa huyu fisadi aliyefichika.
   
 2. H

  HAKIITENDEKE New Member

  #2
  Sep 25, 2010
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hiyo ni asasi ya ccm lakini hao wafanyakazi washikamane kumtoa huyo fisadi ananufaika kupitia pesa zetu sisi wanyonge.
   
 3. DICTATOR

  DICTATOR JF-Expert Member

  #3
  Sep 25, 2010
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0


  Naunga mkono hoja yako mkuu, huyu jamaa ni mmoja wa mafisadi walio mafichoni na jamaa anatafuna pesa ile mbaya. Mimi ni mmoja wa wanachama nakatwa pesa nyingi karibu mshahara wa mwalimu wa shule ya msingi kwa mwezi kwa hiari yangu nikitegemea siku moja bima ya taifa itakuja kuwa mali huko usoni. Lakini muda wote situlii maana kashfa kibao.
   
 4. H

  HAKIITENDEKE New Member

  #4
  Sep 25, 2010
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dada yangu alikuwa anafanya kazi pale akaacha baada ya kumsingizia unaambiwa hata likizo tu haki ya mfanyakazi wanakataliwa.
   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  Sep 25, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Mtaje kwa jina lake, hakuna haja ya kumwogopa mtu wa aina hii!.Analindwa na nani huyu hadi ajiamini hivyo?..Hata hivyo kuna udhaifu mkubwa sana wa kiutendaji kwenye mfuko huu!...Ndio maana baadhi ya walimu wanakarahika hadi kwenda kubeba dawa na kutengenezea pombe ya kienyeji, ni baada ya kuona hawasaidiki na bima hii!
   
Loading...