Mkurugenzi mkuu bima ya afya amfwate Nyoni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkurugenzi mkuu bima ya afya amfwate Nyoni

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mkereketwakamil, Feb 10, 2012.

 1. m

  mkereketwakamil Member

  #1
  Feb 10, 2012
  Joined: Aug 27, 2010
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkurugenzi mkuu bima ya afya naye amfwate nyoni,

  Amesababisha kushuka kwa morali ya utumishi kwa Wafanyakazi wa Mfuko wa bima ya afya kwa kuwatengenezea nidhamu za woga kwasababu akikosolewa anawaadhibu kwa kuhamisha wafanyakazi kutoka vituo vyao. Kwa mfano alimuamisha aliyekuwa mkurugenzi wa fedha kwa kusikiliza maneno bila ya ushahidi. Amekuwa akiongoza ofisi kwa kutumia Informers ambao kazi yao kubwa ni kumpelekea habari nani anasema nini na nani anasema nini kuhusu yeye binafsi na uongozi wake.Anateua jamaa zake na watu anaofahamiana nao kutoka NSSF na kuwapa vyeo bila kuwa na sifa kamili.


  .


   
 2. H

  Huihui2 JF-Expert Member

  #2
  Feb 10, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 395
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Huyu jamaa na Blendina Nyoni lao moja. Si unajua mkataba wake uliisha mwaka 2009/10 lakini Blandina akamuuongezea kiushikaji tu. Wanachota fedha ndefu sana wawili hawa
   
 3. T

  TOWASHI JF-Expert Member

  #3
  Feb 10, 2012
  Joined: Nov 30, 2011
  Messages: 289
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Ah wapi! Huyo hawezi tolewa. Pinda alikuwa bestman wake. Itakuwa kesi ya kifamilia wewe.
  Kimsingi,tofauti ya Dotto na Ndina aliyepumzishwa ni jinsia tu
   
 4. Keynes

  Keynes JF-Expert Member

  #4
  Feb 10, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 493
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35

  Hoja yako mbona naona kama imekaa kimajungu zaidi ya kusema yale yanayofaa kuendeleza nchi?
  Kuhamishwa kwa wafanyakazi ni moja ya management techniques/procedures so kama kuna mtu yeyote anayejisikia vibaya kwa uhamisho huyo atakua si mzalendo mtanzania kwa maana kama kweli mtu ni mfanya kazi sahihi wa shirika fulani lazima awe tayari kulitumikia shirika mahala popote ukizingatia shirika kama la bima ya afya linachukua watu wa professional zote


   
 5. m

  mkereketwakamil Member

  #5
  Feb 10, 2012
  Joined: Aug 27, 2010
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mdau uliyecomment hapo juu umehongwa na nhif, maana wanasifika kwakutoa rushwa kwa waandishi ili waandike habari nzuri kuhusu mfuko. Dawa yake iko jikoni watu wanakusanya ushahidi.
   
 6. S

  Stuxnet JF-Expert Member

  #6
  Feb 10, 2012
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,016
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Hapo kuna shida sana NHIF huyu Humba ni dikteta, ukipishana naye kimtazamo anakutafutia zengwr
   
 7. m

  mkereketwakamil Member

  #7
  Feb 11, 2012
  Joined: Aug 27, 2010
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kabisaa ni dikteta vibaya ameirubuni mpaka bodi ya mfuko haimpingi kitu serikali inatizama wapi haioni viongozi uozo.
   
 8. kalaghesye

  kalaghesye Member

  #8
  Feb 11, 2012
  Joined: Jan 16, 2012
  Messages: 79
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Kwa kweli Keyness unaongea mambo ya vitabuni. Lakini kwa kuwa humu ndani tuko mchanganyiko basi inawezekana wewe ni mwenye kunufaika isivyo halali na NHIF. Nimefuatilia sana michango yako inayohusu NHIF. Usiwe unapinga kila kitu. Basi tupe SWOT/SWOC ya NHIF ili tuangalie kuwa wewe uko neutral.

  Ukisoma habari iliyopelekea mjadala huu inaonekana kuna chembe za ukweli. Ni kweli Humba alitoka NSSF. Hebu twende mtaani tujue ni nani hao kutoka NSSF waliojazana NHIF? Je, kuna movement ya kutoka NHIF kwenda NSSF? Kwa habari za awali, hili la Mkurugenzi wa Utawala na Fedha ni kweli. Ni mwanamama mwenye digirii mbili na CPA juu alihamishiwa Mbeya kuongoza Kanda. Sababu ya transfer ilikuwa ni kutokubaliana na uchotaji wa fedha. Mwenye shule yake akaona isiwe nongwa akaomba kazi NIC ambako ameshika nafasi ile ile. Hivi sasa mkurugenzi wa fedha na utawala ni jamaa aliyetokea NSSF ambako ndiko alikotokea Humba. Tukitoka mitaani tutaleta habari zaidi maana tumeamua kupambana kupinga matumizi mabaya ya vyeo. Jamani cheo ni dhamana.

  Naunga mkono hoja kuwa NHIF isafishwe. Kwanza hii ni sehemu ya Sekta ya Afya. Mh. Pinda fanya mambo hapa.
   
 9. D

  Danniair JF-Expert Member

  #9
  Feb 11, 2012
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 361
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Naunga mkono amfuate Nyoni kwani hafanyi ufuatiliaji kabisa. Pale Agha K unaandikiwa dawa za mwezi mzima na speshalisti lakini dirishani unapewa dawa za juma 1 tu. Zikiisha unakwenda kulipia 63,000/= ili kuandikiwa mwendelezo wa wiki ya 2 wa dawa ambazo ukizinunua dukani ni sh.1,500/- tu.
  Lakini ili kupata cheo hicho Humba alihonga. Na mchoro mzima ulipitia kwa mjombae/mpwae Kikwete ( Bw. Mtawa/ Mlawa) ambaye ni personal secretary wake, wakati huo wakiwa bado Home Affairs. Kwa hiyo ayafanyayo ni matokeo ya hongo.
   
 10. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #10
  Feb 11, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,849
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Hoja yako imekaa kimajungu zaidi,umeshindwa kutushawishi kwa hoja ni kwa namna gani huyu jamaa hafai!
   
 11. kalaghesye

  kalaghesye Member

  #11
  Feb 11, 2012
  Joined: Jan 16, 2012
  Messages: 79
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Nimeipenda stahili yako maana unachokonoa. Kwa kuanzia mpango mkakati wa Bima ya Afya na angalia utekelezaji wake. Je, unajua kuwa hospitali za Dar es Salaam ikiwemo Mikocheni Hospital 30% ya madai yao kwa mfuko ni hewa, na cha ajabu yamekuwa yanalipwa. Pale pana technical problem. Na ikiwa hivyo anayewajibika ni Mkubwa. Nimekwambia tunaingia mtaani kutafuta data zaidi usije kukimbia Tukutu. Subiri .....
   
 12. T

  Topical JF-Expert Member

  #12
  Feb 11, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,177
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Humba ametoka NSSF, hivyo anaajiri waliotoka NSSF ni dhaifu kwasababu ajira inatangazwa na kila mtanzania ana haki ya kupata bila kujali kama alifanya kazi wapi? kufanya kazi NSSF inaweza ikwa na advantage si kwasababu ya Humba bali uzoefu wa kuendesha Social insurance scheme

  Uwizi mkubwa ambao utaufilisi shirika hili ni malipo kwa hospitali binafsi na za kanisa; wanapeleka bill za uwongo na wanafanya over pricing; kingine ukienda na kadi NHIF dr. anakuandikia dawa unaweza kubeba na mfuko salfeti kw auwingi kisa wanata kuuza madawa yao;

  Ku-solve hiyo problem ni trick kwasababu ukigombana na wenye hosptali wanaanza kuwabagua wanachama wako hence malalamiko kwa mfuko..

  Mimi ningewashauri kina Humba wasihangaike na hospitali ya kanisa wala binafsi; wao walenge huduma za kwa hospitali ya serikali na waziboresha hospitali hizo (ni hii very possible) maana pesa wanayo na wao ni goverment scheme, private sector na church projects ni uwizi mtupu kwa mfuko na wanachama..
   
 13. N

  Nansawa Senior Member

  #13
  Feb 12, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 191
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  hii si mara ya kwanza kwa Humba kuandikwa humu. Kwa wakereketwa wa ufisadi inapaswa kuyafanyia kazi. Si kukimbilia kusema ni majungu. Natumaini aliesema haya ni majungu ni MWONGO mkubwa. Ni saa ngapi ameyafanyia kazi? na kugundua ni majungu kama si miongoni mwa wanaopewa ALAMBA ice krim za azam?
  Na nashangaa sana wakati Mh Shelukindo alipomuibua katibu mkuu wa Nishati na Madini kwa nini NHIF haikupitiwa. Kuna mambo mengi machafu yamefichika pale. Na nashangaa kina Zito huko kwenye hesabu za mashirika ya umma huwa wanfanya nini? au ndo mwahongwa matibabu ya bure kupitia michango yetu walala hoi?
  CHADEMA mbona mmepakalia kimya sana wakati mwajua fika pesa inavyochotwa.
  Watu wanjipangia mishahara minono na marupurupu manono kwa michango ya walalahoi ambao hata huduma hiyo ya matibabu kupata ni nadra kwa kweli NHIF IS AS GOOD AS CCM. chadema what are you waiting for?
  mh. Mbowe ni kweli unakubali pesa za wagonjwa kuchukuliwa kiulaini na kuchezewa kama afanyavyo Humba. Tafadhali fuatilieni matumizi ya pesa pale.
  Humba elewa wewe si Mungu. Na kumbuka hata katika vitabu nitakatifu hakuna falme ilyosimama milele. Siku yako ya aibu iko njiani.
  Amaaa kweli sura yako yasadifu tabia zako.
  Hivi huwa unasali au ndo Bagamoyo sana?
   
 14. N

  Nansawa Senior Member

  #14
  Feb 12, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 191
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Halafu wewe Humba hivi una miaka mingapi hata hutaki kustaafu? haujajiandaa kimshiko? Elewa money is never more than enough. Just quit usijeondoka kwa aibu. Yaani kidevu chako chaonesha kimenyolewa sana kama ndevu zilikuwahi sana basi kwa uchache ulianza kunyoa ndevu ukiwa na 18. Lakini kidevu chasoma umetumia wembe for 44 years. Brother that is enough. Kama ni totoz hata nje ya maofisi wapo. Ushauri wa bure hizo pesa zikuweke basi hata smart jamani. Unadhani kwa kuwa mchafu ndo tutasema we huibi?
   
Loading...