Mkurugenzi Babati Mjini azidi kufunga makanisa

Huyo mkurugenzi atakuwa CHADEMA huyo huu ni mwaka wa uchaguzi na maeneo hayo ni ngome ya upinzani anachotaka ni kuchochea wananchi kwa kuwaudhi kwa kufunga makanisa yao ili oktoba uchaguzi ukifika wasiipe kura CCM

Hiki sio kipindi cha kuudhi makundi makubwa ya wapiga kura.

Huyo mkurugenzi ana agenda ya siri ya kuhakikisha CCM INASHINDWA .Kaanza kampeni zake za kuusaidia upinzani kushinda

Yaani niliposoma hoi comment nikakumbuka mbali mnamo mwaka 1984 huko USA Oregon kulikuwa na jamaa mmoja alianzisha dini yake anaitwa Rajneeshee au Osho
Ili kumchomeka mtu wao serikalini
Siwezi kuweka yote hapa ila jisomee kwa mda wako

Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Umesema kweli tupu
Hatakaa aibomoe kwa sababu wale husahau tofauti zao inapokuja kuguswa nyumba zao za ibaada. Sasa kwa kuwa wao huogopa mwanadamu basi inatakiwa hao wakristo wamlilie huyo Mungu wao awatetee mwenyewe.
Mungu asiyeweza hata kuwatetea hao kondoo wake nadhani mwacheni huyo. Kangi alimdhalilisha mtumishi na haukupita mwaka, pamoja na mauno yake hakufua dafu. Watumishi wa Mungu Babati, Zaburi 105: 4 Inasema; Mtakeni Bwana na nguvu zake. Je, huyo mkurugenzi ni mkuu kuliko Mungu ila ni mdogo kuliko Allah??
Kuna mahali mmekosea watumishi. Jikusanyeni upya muutafute uso wa Bwana. Usiseme ni hao sio sisi. Ukiona mwenzio ananyolewa, weye tia maji.He is coming for you. Alianza kidogo, sasa kazoea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya...bado misikiti sasa...

Salam kwenu,

Sina mengi ya kusema ila katika hali isiyo ya kawaida, Mkurugenzi wa H/mji wa Babati anaendelea KUFUNGA makanisa kisa "Ardhi yake sio kwa matumizi ya ibada".

Hali hii isipochunguzwa na kuleta suluhu inaweza kuleta situation isiyo ya kawaida kwakuwa kitendo cha kuingilia imani watanzania walio wengi hawajakizoea kitendo hiki.

NB: Mimi sina dini ila wenzangu wana dini.

Serikali isipochukua hatua za haraka moto unaweza kuwaka.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
China walinyonga kabisa lkn hadi leo yapo.
Unaweza kushinda vita vyote ila sio vita na makanisa.

Wao kibali hawakipati serikalini wanapewa direct na Mungu na Mungu ndiye anaweza kuruhusu kazi yao ikome sio mtu.

Sizungumzii fake pastors au gospel entrepreneurs
 
Tungeanza na jina la mkurugenzi ili kukamilisha habari na kujua namna ya kuanza kudeal nae .
 
China walinyonga kabisa lkn hadi leo yapo.
Unaweza kushinda vita vyote ila sio vita na makanisa.

Wao kibali hawakipati serikalini wanapewa direct na Mungu na Mungu ndiye anaweza kuruhusu kazi yao ikome sio mtu.

Sizungumzii fake pastors au gospel entrepreneurs
kweli kabisa
 
Ki ukweli haya makanisa ni shida. Kuna limoja lilifunguliwa jirani yangu likajitia ni libabe, likawa linafungulia mziki kuanzia saa sita usiku hadi saa kumi..mzee mzima nikaona hii ni dharau

Nikawaendea kwa balozi wakamnunua
Nikaenda serikali za mitaa nako wakanunuliwa
Nikaona mbwai na iwe mbwai

Nikawaendea kariakoo nikawajia (subufer) ya laki tano
Nikawavizia siku yao ya kuanza kupiga muziki ambayo mara nyingi wanaanza ijumaa

Mzee mzima nikajikoki na makonyagi ya kutosha nikabeba na safari lager nikajiendea nyumbani saa nne usiku, wakati wanatesti mitambo yao nikafungua (sabufer) langu hadi mwisho.
Wakaja kunigongea na kuniomba nipunguze mziki
Nikawajibu kama mnataka nipunguze na nyie kule sauti isinifikie nyumbani kwangu

Tangia hapo walibadilika na mtaa uko shwari, siku wakilianzisha hata kwa bahati mbaya watabaelezea.

SICHEZEWI

Sent using Jamii Forums mobile app
Makanisa ya kilokole ni kero sana, hafu unakuta huo mtaa hata muumini wa hilo kabisa hayupo, wanatoka maeneo ya mbali wanakuja kuwapigia watu kelele tu
 
Kagame alikosea sana kwa hili anasahau upesi
mauaji ya kimbari yaliendeshwa na kanisa katoliki ambalo viongozi wake wote wana digrii za theolojia.Papa hadi aliomba msamaha hadharani kwa kilichofanywa na mapadri na maaskofu wa kanisa katoliki Rwanda.MAUAJI YALE wasomi wenye digrii za theolojia ndio waliendesha mauaji sasa unapotaka digrii za theolojia ziwe kila kanisa unajielewa?

Pia uwepo wa utitiri wa dini nyingi zenye Imani tofauti tofauti.Kuna faida kubwa Sana nchi kuwa na dini nyingi na madhehebu mengi utitiri yenye Imani tofauti tofauti na viongozi wa dini wenye upeo mdogo wa uelewa Ni muhimu katika kulinda amani ya nchi.Kupanga mapinduzi huwa Ni kugumu mno sababu ya tofauti kubwa za kiimani.

Nchi mfano zenye dini moja au mbili tu mfano rahisi mno kupanga mapinduzi.nchi Kama somalia ,nchi Kama Rwanda iliwezekana sababu ya tatizo Hilo Hilo .Mauaji ya kimbari yalikuwa rahisi kupangwa ndani ya kanisa Katoliki sababu ndio wako majority ndio dini ya wahutu walio wengi wengi ukiunganisha na nchi hiyo kuwa na makabila makubwa mawili tu ya wahutu na watusi unaona kabisa ilivyo rahisi kufanya mapinduzi kwa kutumia muundo mbinu wa kanisa Katoliki au wa kikabila wa kitusi au kihutu.

Ukiwa na dini nyingi zenye imani tofauti husaidia kutunza amani na kuzuia uasi mfano waislamu wa siasa Kali wakiianzisha uasi waislamu wenye msimamo wa wastani wanapinga,walokole wakilianzisha wakatoliki hawaungi mkono,wakatoliki wakilianzisha wasabato wanalikataa nk nk kwa hiyo amani inadhibitiwa kwa kuruhusu dini ziwe nyingi iwezekenavyo na zenye Imani tofauti tofauti.Hapa ndipo wanasiasa husema dini Zina mchango mkubwa katika amani ya nchi.Nchi zenye dini moja au mbili kubwa mapinduzi marahisi kuyapanga.Nchi za Latin America Ni moja ya mifano na nchi za kiarabu.Nchi Kama Iran nk

Nchi kuwa na amani Moja ya silaha kubwa inayotumiwa na wanasiasa Ni ya divide and rule.Na chombo kimojawapo kikubwa kinachotumika Ni dini .Serikali inahakikisha hakuna dini Moja inakuwa na nguvu kubwa mno katika nchi kwa kuruhusu dini zingine zianzishwe au makanisa mengine yaanzishwe Kama waanzishaji hamna serikali yenyewe kupitia shirika lake la ujasusi inatakiwa itoe watu wafungue makanisa mengine yenye imani tofauti na ku ya finance Kama state churches zake au dini zake.Kukiwa na utitiri wa makanisa Ni rahisi serikali nayo kuanzisha Yake au dini zake na kupandikiza viongozi wake wa dini kwa ajili ya kulinda usalama wa nchi .

SI wote wanaamini kwenye kiongozi wa dini lazima kusoma, hao wasioamini wanahitaji kuwa na groups zao ukiwaacha ukawatupa nje unaua network ya security ya kuwafikia as a group of idiots whatever you call them!!!

Their churches ziwe street churches or whatever za muhimu Sana kwenye usalama wa nchi hasa zikiwa open Sio hidden secret groups.Kuwafungia unatengeneza hidden secret groups sababu hawawezi Sali kwenye hizo zako unazotaka wewe wataingia mafichoni.Na huko mafichoni kuwafikia shughuli pevu sababu ukiwafungia usitarajie watasali kwenye hayo yako unayoyataka

Kagame alichofanya Ni ku consolidate much powers kwa few religious Giants na ku kick out minorities waliozagaa kila mtaa na interior rural areas ambao Ni watu muhimu hata kupandikiza mashushu wa mtaa au Kijiji wakijificha kwenye hivyo vikanisa vya uchochoroni.Vikifutika Sio kesi kubwa Kagame atakuwa na hard time ya KU monitor what is in the streets au porini kwenye rural areas sababu angekuwa na hidden representatives kwenye hivyo vikanisa vya uchochoroni.Sasa hivi anabidi ajikombe kwa Kanisa katolki limsaidie kujua ya vichochoroni kwa kupandikiza mashushu kwenye jumuiya ndogo ndogo za Kanisa katoliki tu au aombe maaskofu wawe wanampa taarifa kila siku za Nini kiko kule kwenye jumuiya zao wampe security secrets za jumuiya husika.Na hiyo haitakuwa na ufanisi sana sababu sio watu wote Ni Catholics atakaoweza kuwadukua vizuri ni wale catholics tu wanaosali jumuiya za kikatoliki maeneo yao the rest hamna system ya kuwadukua sababu hawana mfumo wa kuwakusanya Kama group

Kagame amekosea alitakiwa aache dini zibaki huko huko.Wao wafanye Kazi ya KU plant mashushu tu kwenye hizo religious groups.

Uzuri vikanisa vidogo huwa Ni shock absorber pia kukitokea Tatizo.Mfano makanisa makubwa hutoa nyaraka za kupinga serikali na kuitisha maandamano.Vikanisa vidogo huibuka kupinga na kuwa upande wa serikali.Ukiyapa more powers Giants iko siku utalia kilio Cha mbwa.

Waliomshauri Kagame wana agenda ya Siri dhidi Yake atakuja ijua mbele ya safari.

Tanzania Ni nchi ya amani kwa sababu kuu mbili ya kwanza Nyerere aliposhika nchi alivunja ukabila kwa hiyo.kukawa hakuna kabila linalojitutumua dhidi ya mengine

Mwinyi alipokuja akavunja udini kwa kuruhusu dini huria za imani nyingi tofauti kuanzishwa ambazo haziivi kiimani na zingine kwa pande zote za ukristo na uislamu.

Kikwete alivypingia akapiga marufuku mtu akiajiriwa kujaza kabila lake au dini kwenye fomu.za maombi ya Kazi

Kenya walipata machafuko sababu ukabila wameshindwa kusambaratisha

Rwanda pia ilipata matatizo sababu ukabila walishindwa kusambaratisha na udini walishindwa kusambaratisha.Baada ya Kagame kushika madaraka ukabila anausambaratisha vizuri mno ila kwenye udini kumemshinda. Aliposhika MADARAKA watu walikuwa tayari kufanya Kazi ya kusambaratisha udini kwa kuanzisha dini na makanisa lukuki kila Kona ili kuua nguvu kubwa ya udini kwenye dini kubwa uliokuwepo Sasa Kagame anafanya kazi ya KU consolidate dini kubwa ziwe more strong na kusambaratisha zinazoibuka!!!! Kwa hili Kagame na bunge lake hawako vizuri.Walitakiwa waache ziendelee kuchipuka tu hata zifikie milioni Ni vizuri tu Tena zikifikia mahali ambapo kila mtu ana dini Yake nyumbani tu hapo inakua POA zaidi
sorry sir sijasoma ulichoandika.
 
Salam kwenu,

Sina mengi ya kusema ila katika hali isiyo ya kawaida, Mkurugenzi wa H/mji wa Babati anaendelea KUFUNGA makanisa kisa "Ardhi yake sio kwa matumizi ya ibada".

Hali hii isipochunguzwa na kuleta suluhu inaweza kuleta situation isiyo ya kawaida kwakuwa kitendo cha kuingilia imani watanzania walio wengi hawajakizoea kitendo hiki.

NB: Mimi sina dini ila wenzangu wana dini.

Serikali isipochukua hatua za haraka moto unaweza kuwaka.

Sent using Jamii Forums mobile app
Def wa babati, uko sawa 100% , yafunge kabisaa
 
Attachments

  • IMG-20200202-WA0000.jpg
    IMG-20200202-WA0000.jpg
    75.3 KB · Views: 1
Mkurugenzi wa babati mji hongera sana sana,majanisa yajengwe kwenye maeneo yaliyopangwa kujengea majanisa.wakurugenzi wa Halmashauri zingine wajifunzie kutoka kwa mkurugenzi wa babati mji.safi kabisa.wanajenga makanisa vichochoroni ,land rent hawalipi Ila sadaka wanakusanya, mkurugenzi wa ilemela mwanza,singida mji, Hai na Moshi manispaa Kilimanjaro,Arusha jiji,ilala, morogoro manispaa wote muende babati mji mkajifunze nna ya kubomoa makanisa yaliyohengwa kwenye makazi ya watu na land rent hawalipi. Hongera sana mkurugenzi wa babati.

Pambana na watu wanaoipotosha injili ya Kristo na sii Kanisa,,
Kanisa ni Mwili wa Kristo my Friend!!!!
Hakuna mtu aliyepambana na Kanisa akabaki salama rafiki,,,,hata wewe unabwabwaja kwasabbu una mdomo wakubwabwaja,,,endelea kung’ang’ana na KANISA LIFUNGWE UTAKUWA HISTORIA....
 
Back
Top Bottom