Mkurugenzi Babati Mjini azidi kufunga makanisa

MfalmewaKiha

JF-Expert Member
Feb 16, 2017
1,191
1,231
Salam kwenu,

Sina mengi ya kusema ila katika hali isiyo ya kawaida, Mkurugenzi wa H/mji wa Babati anaendelea KUFUNGA makanisa kisa "Ardhi yake sio kwa matumizi ya ibada".

Hali hii isipochunguzwa na kuleta suluhu inaweza kuleta situation isiyo ya kawaida kwakuwa kitendo cha kuingilia imani watanzania walio wengi hawajakizoea kitendo hiki.

NB: Mimi sina dini ila wenzangu wana dini.

Serikali isipochukua hatua za haraka moto unaweza kuwaka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siasa dini ukabila pengine ndivyo walivyofundishwa ni sehemu ya utendaji wao wa kazi
 
👏👏👏👏Safi sana Mkurugenzi funga uwezavyo kama Kagame ameyafunga 700 na huwezi kuwa na kanisa hadi uwe na degree ya theology

Fungia kabisa wachungaji wajanja wajanja wapigaji wanaoona makanisa ni sshemu ya kupiga hela na kila sehemu unafungua kanisa nakuweka miziki mikubwa usiku kucha watu hawalali

Watafute sehemu zilizotengwa kwa kujenga makanisa
 
Safi sana Mkurugenzi funga uwezavyo kama Kagame ameyafunga 700 na huwezi kuwa na kanisa hadi uwe na degree ya theology

Fungia kabisa wachungaji wajanja wajanja wapigaji wanaoona makanisa ni sshemu ya kupiga hela na kila sehemu unafungua kanisa nakuweka miziki mikubwa usiku kucha watu hawalali

Watafute sehemu zilizotengwa kwa kujenga makanisa
Waende sehemu zilizotengwa, wakati nia yao ni kufuata walipo watu,

wapige makelele msikie, muwafuate...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Salam kwenu,
Sina mengi ya kusema ila katikati Hali isiyo ya kawaida mkurugenzi wa H/mjii wa Babati anaendelea KUFUNGA makanisa kisa *Ardhi yake sio kwa matumizi ya ibada*
Hali hii isipo chunguzwa na kuleta suluhu inaweza kuleta situation isiyo ya kawaida kwakua kitendo Cha kuingilia imani watanzania walio wengi hawajakizoea kitendo hiki
NB mimi sina Dini ila wenzangu wanadini.
Serikali isipo chukua hatua za haraka moto unaweza kuwaka.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkurugenzi wa babati mji hongera sana sana,majanisa yajengwe kwenye maeneo yaliyopangwa kujengea majanisa.wakurugenzi wa Halmashauri zingine wajifunzie kutoka kwa mkurugenzi wa babati mji.safi kabisa.wanajenga makanisa vichochoroni ,land rent hawalipi Ila sadaka wanakusanya, mkurugenzi wa ilemela mwanza,singida mji, Hai na Moshi manispaa Kilimanjaro,Arusha jiji,ilala, morogoro manispaa wote muende babati mji mkajifunze nna ya kubomoa makanisa yaliyohengwa kwenye makazi ya watu na land rent hawalipi. Hongera sana mkurugenzi wa babati.
 
Amuulize mwenzie kangi Lugora tulimuomnya humu achana na dini wewe kakomalia walokole akawa anawadhalilisha na kufunga makanisa kiko wapi?

makanisa ni zaidi ya makanisa asione yamezagaa kila kona akachukulia wajinga fulani shauri yake wacha ajitie mjuaji

huyo mkurugenzi wa babati anachezea moto
 
Mkurugenzi wa babati mji hongera sana sana,majanisa yajengwe kwenye maeneo yaliyopangwa kujengea majanisa.wakurugenzi wa Halmashauri zingine wajifunzie kutoka kwa mkurugenzi wa babati mji.safi kabisa.wanajenga makanisa vichochoroni ,land rent hawalipi Ila sadaka wanakusanya, mkurugenzi wa ilemela mwanza,singida mji, Hai na Moshi manispaa Kilimanjaro,Arusha jiji,ilala, morogoro manispaa wote muende babati mji mkajifunze nna ya kubomoa makanisa yaliyohengwa kwenye makazi ya watu na land rent hawalipi. Hongera sana mkurugenzi wa babati.
Huyo mkurugenzi atakuwa CHADEMA huyo huu ni mwaka wa uchaguzi na maeneo hayo ni ngome ya upinzani anachotaka ni kuchochea wananchi kwa kuwaudhi kwa kufunga makanisa yao ili oktoba uchaguzi ukifika wasiipe kura CCM

Hiki sio kipindi cha kuudhi makundi makubwa ya wapiga kura.

Huyo mkurugenzi ana agenda ya siri ya kuhakikisha CCM INASHINDWA .Kaanza kampeni zake za kuusaidia upinzani kushinda
 
Ki ukweli haya makanisa ni shida. Kuna limoja lilifunguliwa jirani yangu likajitia ni libabe, likawa linafungulia mziki kuanzia saa sita usiku hadi saa kumi..mzee mzima nikaona hii ni dharau

Nikawaendea kwa balozi wakamnunua
Nikaenda serikali za mitaa nako wakanunuliwa
Nikaona mbwai na iwe mbwai

Nikawaendea kariakoo nikawajia (subufer) ya laki tano
Nikawavizia siku yao ya kuanza kupiga muziki ambayo mara nyingi wanaanza ijumaa

Mzee mzima nikajikoki na makonyagi ya kutosha nikabeba na safari lager nikajiendea nyumbani saa nne usiku, wakati wanatesti mitambo yao nikafungua (sabufer) langu hadi mwisho.
Wakaja kunigongea na kuniomba nipunguze mziki
Nikawajibu kama mnataka nipunguze na nyie kule sauti isinifikie nyumbani kwangu

Tangia hapo walibadilika na mtaa uko shwari, siku wakilianzisha hata kwa bahati mbaya watabaelezea.

SICHEZEWI

I see
 
Nampongeza sana kwa kazi hiyo! Hapa jirani kwangu kuna kikanisa cha mbao chenye waumini watatu ila kina speaker ambazo siyo za nchi hii sasa kutwa nzima ni makelele, yaani hatulali huku! Mimi ni mkristo ila naunga mkono hoja.
 
Hayo makanisa ndo Yale yanayoweka benders ya Israel kwenye altare wakati waisrael si wakristo..if ndo hao yafungwe tu
 
Huyo mkurugenzi atakuwa CHADEMA huyo huu ni mwaka wa uchaguzi na maeneo hayo ni ngome ya upinzani anachotaka ni kuchochea wananchi kwa kuwaudhi kwa kufunga makanisa yao ili oktoba uchaguzi ukifika wasiipe kura CCM

Hiki sio kipindi cha kuudhi makundi makubwa ya wapiga kura.

Huyo mkurugenzi ana agenda ya siri ya kuhakikisha CCM INASHINDWA .Kaanza kampeni zake za kuusaidia upinzani kushinda
Kwenye issue ya mipango miji hakuna Cha chadema Wala ccm .hakuna Cha walokole.wajenga makanisa hovyo marufuku.hakuna Cha uchaguzi.makanisa yajengwe maeneo husika
 
👏👏👏👏Safi sana Mkurugenzi funga uwezavyo kama Kagame ameyafunga 700 na huwezi kuwa na kanisa hadi uwe na degree ya theology
Kagame alikosea sana kwa hili anasahau upesi
mauaji ya kimbari yaliendeshwa na kanisa katoliki ambalo viongozi wake wote wana digrii za theolojia.Papa hadi aliomba msamaha hadharani kwa kilichofanywa na mapadri na maaskofu wa kanisa katoliki Rwanda.MAUAJI YALE wasomi wenye digrii za theolojia ndio waliendesha mauaji sasa unapotaka digrii za theolojia ziwe kila kanisa unajielewa?

Pia uwepo wa utitiri wa dini nyingi zenye Imani tofauti tofauti.Kuna faida kubwa Sana nchi kuwa na dini nyingi na madhehebu mengi utitiri yenye Imani tofauti tofauti na viongozi wa dini wenye upeo mdogo wa uelewa Ni muhimu katika kulinda amani ya nchi.Kupanga mapinduzi huwa Ni kugumu mno sababu ya tofauti kubwa za kiimani.

Nchi mfano zenye dini moja au mbili tu mfano rahisi mno kupanga mapinduzi.nchi Kama somalia ,nchi Kama Rwanda iliwezekana sababu ya tatizo Hilo Hilo .Mauaji ya kimbari yalikuwa rahisi kupangwa ndani ya kanisa Katoliki sababu ndio wako majority ndio dini ya wahutu walio wengi wengi ukiunganisha na nchi hiyo kuwa na makabila makubwa mawili tu ya wahutu na watusi unaona kabisa ilivyo rahisi kufanya mapinduzi kwa kutumia muundo mbinu wa kanisa Katoliki au wa kikabila wa kitusi au kihutu.

Ukiwa na dini nyingi zenye imani tofauti husaidia kutunza amani na kuzuia uasi mfano waislamu wa siasa Kali wakiianzisha uasi waislamu wenye msimamo wa wastani wanapinga,walokole wakilianzisha wakatoliki hawaungi mkono,wakatoliki wakilianzisha wasabato wanalikataa nk nk kwa hiyo amani inadhibitiwa kwa kuruhusu dini ziwe nyingi iwezekenavyo na zenye Imani tofauti tofauti.Hapa ndipo wanasiasa husema dini Zina mchango mkubwa katika amani ya nchi.Nchi zenye dini moja au mbili kubwa mapinduzi marahisi kuyapanga.Nchi za Latin America Ni moja ya mifano na nchi za kiarabu.Nchi Kama Iran nk

Nchi kuwa na amani Moja ya silaha kubwa inayotumiwa na wanasiasa Ni ya divide and rule.Na chombo kimojawapo kikubwa kinachotumika Ni dini .Serikali inahakikisha hakuna dini Moja inakuwa na nguvu kubwa mno katika nchi kwa kuruhusu dini zingine zianzishwe au makanisa mengine yaanzishwe Kama waanzishaji hamna serikali yenyewe kupitia shirika lake la ujasusi inatakiwa itoe watu wafungue makanisa mengine yenye imani tofauti na ku ya finance Kama state churches zake au dini zake.Kukiwa na utitiri wa makanisa Ni rahisi serikali nayo kuanzisha Yake au dini zake na kupandikiza viongozi wake wa dini kwa ajili ya kulinda usalama wa nchi .

SI wote wanaamini kwenye kiongozi wa dini lazima kusoma, hao wasioamini wanahitaji kuwa na groups zao ukiwaacha ukawatupa nje unaua network ya security ya kuwafikia as a group of idiots whatever you call them!!!

Their churches ziwe street churches or whatever za muhimu Sana kwenye usalama wa nchi hasa zikiwa open Sio hidden secret groups.Kuwafungia unatengeneza hidden secret groups sababu hawawezi Sali kwenye hizo zako unazotaka wewe wataingia mafichoni.Na huko mafichoni kuwafikia shughuli pevu sababu ukiwafungia usitarajie watasali kwenye hayo yako unayoyataka

Kagame alichofanya Ni ku consolidate much powers kwa few religious Giants na ku kick out minorities waliozagaa kila mtaa na interior rural areas ambao Ni watu muhimu hata kupandikiza mashushu wa mtaa au Kijiji wakijificha kwenye hivyo vikanisa vya uchochoroni.Vikifutika Sio kesi kubwa Kagame atakuwa na hard time ya KU monitor what is in the streets au porini kwenye rural areas sababu angekuwa na hidden representatives kwenye hivyo vikanisa vya uchochoroni.Sasa hivi anabidi ajikombe kwa Kanisa katolki limsaidie kujua ya vichochoroni kwa kupandikiza mashushu kwenye jumuiya ndogo ndogo za Kanisa katoliki tu au aombe maaskofu wawe wanampa taarifa kila siku za Nini kiko kule kwenye jumuiya zao wampe security secrets za jumuiya husika.Na hiyo haitakuwa na ufanisi sana sababu sio watu wote Ni Catholics atakaoweza kuwadukua vizuri ni wale catholics tu wanaosali jumuiya za kikatoliki maeneo yao the rest hamna system ya kuwadukua sababu hawana mfumo wa kuwakusanya Kama group

Kagame amekosea alitakiwa aache dini zibaki huko huko.Wao wafanye Kazi ya KU plant mashushu tu kwenye hizo religious groups.

Uzuri vikanisa vidogo huwa Ni shock absorber pia kukitokea Tatizo.Mfano makanisa makubwa hutoa nyaraka za kupinga serikali na kuitisha maandamano.Vikanisa vidogo huibuka kupinga na kuwa upande wa serikali.Ukiyapa more powers Giants iko siku utalia kilio Cha mbwa.

Waliomshauri Kagame wana agenda ya Siri dhidi Yake atakuja ijua mbele ya safari.

Tanzania Ni nchi ya amani kwa sababu kuu mbili ya kwanza Nyerere aliposhika nchi alivunja ukabila kwa hiyo.kukawa hakuna kabila linalojitutumua dhidi ya mengine

Mwinyi alipokuja akavunja udini kwa kuruhusu dini huria za imani nyingi tofauti kuanzishwa ambazo haziivi kiimani na zingine kwa pande zote za ukristo na uislamu.

Kikwete alivypingia akapiga marufuku mtu akiajiriwa kujaza kabila lake au dini kwenye fomu.za maombi ya Kazi

Kenya walipata machafuko sababu ukabila wameshindwa kusambaratisha

Rwanda pia ilipata matatizo sababu ukabila walishindwa kusambaratisha na udini walishindwa kusambaratisha.Baada ya Kagame kushika madaraka ukabila anausambaratisha vizuri mno ila kwenye udini kumemshinda. Aliposhika MADARAKA watu walikuwa tayari kufanya Kazi ya kusambaratisha udini kwa kuanzisha dini na makanisa lukuki kila Kona ili kuua nguvu kubwa ya udini kwenye dini kubwa uliokuwepo Sasa Kagame anafanya kazi ya KU consolidate dini kubwa ziwe more strong na kusambaratisha zinazoibuka!!!! Kwa hili Kagame na bunge lake hawako vizuri.Walitakiwa waache ziendelee kuchipuka tu hata zifikie milioni Ni vizuri tu Tena zikifikia mahali ambapo kila mtu ana dini Yake nyumbani tu hapo inakua POA zaidi
 
Salam kwenu,

Sina mengi ya kusema ila katika hali isiyo ya kawaida, Mkurugenzi wa H/mji wa Babati anaendelea KUFUNGA makanisa kisa "Ardhi yake sio kwa matumizi ya ibada".

Hali hii isipochunguzwa na kuleta suluhu inaweza kuleta situation isiyo ya kawaida kwakuwa kitendo cha kuingilia imani watanzania walio wengi hawajakizoea kitendo hiki.

NB: Mimi sina dini ila wenzangu wana dini.

Serikali isipochukua hatua za haraka moto unaweza kuwaka.

Sent using Jamii Forums mobile app

Safi sana kama anafungia makanisa yaliyojengwa kwenye makazi ya watu bila kufuata mipango miji.
 
Kwenye issue ya mipango miji hakuna Cha chadema Wala ccm .hakuna Cha walokole.wajenga makanisa hovyo marufuku.hakuna Cha uchaguzi.makanisa yajengwe maeneo husika
Misikiti vipi mbona huongelei ambayo iko kila eneo la makazi na biashara umekomalia makanisa tu nenda kabomoe au kuifungia hiyo misikiti ambayo haijajengwa kufuata mipango miji tukuone kama wewe kidume kweli
 
Back
Top Bottom