Mkulo, Maige, Ngeleja kikaangoni TAKUKURU

Mkulo, Maige, Ngeleja kikaangoni TAKUKURU

...unadhani kampuni zilizo nyimwa vitalu ndani kuna watanzania wangapi wanao tegemewa na familia zao? unatoa kwa mtu ambaye hata hajui wageni anapata lini je ni kuijenga nchi..............,si tuanalilia maslahi ya watanzania wenzetu ambao wanapunguzwa kazi.
BABU CHONDO,

Ni sisi wenyewe tuliolalamika kwamba sheria inawapendelea wageni kwenye biashara za vitalu na utalii. Ni sisi tuliotaka Professional Hunters na Guide wawe Watanzania. Maige alichofanya ni kuitikia kilio cha Wazawa.

Kama ajira walikuwa wanapata kwa kuajiliwa ktk makampuni za kigeni basi vilevile wangeendelea kuzipata kwenye Kampuni za Wazawa. Na kubwa zaidi mapato yanabaki nchini kukuza uchumi. Kwa nini Watanzania hatubebeki na hatutaki kuaminana?

Yaani kwa imani yako BABU CHONDO hatuwezi kuajiliana mpaka hao wageni kutoka nje? Suala la makampuni kutojua wageni wanakuja lini: wageni hawaji kutembelea Kampuni bali kuangalia vivutio vya nchi. Na hivi vivutio vinatangazwa na TTB kwa manufaa ya sekta nzima na si kampuni fulani.
 
Last edited by a moderator:
Ahsante robot kwa taarifa.

Kwa kifupi tu sitegemei kitu chochchote chanya hapa, ni zile zile sarakasi za takukuru na ccm.
Hapa tunazugwa ili tuwache kupiga kelele.
Nakubaliana na wewe ndugu, kuna madudu mengina yanamgusa hata baba Riz, hao "watuhumiwa" waliyasimamia!
 
....TAKUKURU hawatafanya chochote kile dhidi ya hawa mafisadi....

Watawachunguza kisha watadai hakuna ushahidi wa kutosha dhidi yao kuweza kuwapandisha kizimbani....

Hawa nao wanazijua siri nyingi za ndani ya Serikali kama wakiamua kuongea basi pale Ikulu patakuwa hapatoshi....

Tusubiri tuone kama Edward Hosea ataamua kuacha usanii wake anaofanya kuhusiana na mafisadi na wala rushwa wakubwa ndani ya Serikali tangu alipopewa Ukurugenzi wa TAKUKURU.
 
Tatizo ni kwamba Mkuu wa nchi si msafi ndiyo maana hawa jamaa wanadunda kwa sababu kuna deals ambazo zinamgusa hata yeye mwenyewe.

Mkuu hapo umemaliza yote. Mambo hayataweza kubadilika bila kupata rais msafi. Rais akiwa fisadi kama huyu wa sasa lazima na serikali yake itakuwa fisadi tu
 
Hosea aliwahi kuuliza UDSM kuhusu kesi za ufisadi akajibu " a dog can not bite his boss but atleast can bark at him"
Tumeshazoea ngonjera zao na hakuna jipya..
Yes. Angalau bweka na tutanyamaza!
 
Kama wako kwa fisadi Hosea futeni matumaini kwani Hosea ataomba chake na anawasafisha na jik wanakuwa weupeeeee
 
NOOOOO kama kweli majarada yapo kwa Hosea watafikishwa mahakaman,na pia inategemea na uzito na ushahidi wa tuhuma dhidi yao.PCCB is strong enough,subirin mtaona
Ni strong kwa rushwa za elfu kumi kumi na laki moja moja! Kwani na hao mawaziri walifanya ubadhilifu wa laki 1?
 
Inadaiwa Mkulo kakutwa na Vogue 2 na Land Cruiser 2 zote mpya hata nylon hazijatolewa kwenye magari yenyewe nyumbani kwake Mikocheni.

Mzee wa Megawatts (Ngeleja) kashfa yake ni ya zile Benz zake alizoleta na Air Cargo na madudu mengine wizarani.

Maige kauza Vitalu vya walafi serikalini kawazidi akili wenzake (isichukuliwe kama namtetea)

Habari zaidi zitafuatia...
Ningependa kufahamu vifungu vya sheria vinavyo criminalize kumiliki Vogue 2 na Land Cruiser mpya. Pamoja na vipengele vya sheria vinavyoongelea kuagiza magari mapywa kwa ndege, vilivyovunjwa. Ahsanteni.

(By the way, Invisible, usifute post zangu, huna sababu ya kuziogopa.)
 
Miezi 4 iliyopita Mkulo aliingiza Range Rover Vogue Brand New, O odometer...1 na New Land Cruiser Vx V8 1 kwa pamoja.... Ndani ya nylon hadi kwake Dar.... Iligharimu around Tshs 615 Million according to Kijana wake wa kiume... i saw too.... Mwizi mkubwa huyu Mkulo... Mwiziii kama Maige ndio usiseme, Ngeleja, wafungwe fasta...

Wakuu,

Taarifa zilizopenya kwenye viunga hivi zinadai kuwa mawaziri walioachishwa kazi [Mkulo, Maige na Mzee wa Megawatts (Ngeleja)] wako kikaongoni Takukuru na kwamba kila siku lazima waripoti saa tatu asubuhi.

Inadaiwa Mkulo kakutwa na Vogue 2 na Land Cruiser 2 zote mpya hata nylon hazijatolewa kwenye magari yenyewe nyumbani kwake Mikocheni.

Mzee wa Megawatts (Ngeleja) kashfa yake ni ya zile Benz zake alizoleta na Air Cargo na madudu mengine wizarani.

Maige kauza Vitalu vya walafi serikalini kawazidi akili wenzake (isichukuliwe kama namtetea)

Habari zaidi zitafuatia...
 
Labda tuibinafsishe takukuru iwe sehemu ya sfo ya uingereza na walipwe kwa commission ya hela watayookoa, otherwise, takukuru ni aina ya ufisadi mwingine kwa nchi hii.
 
CCM - Takukuru Branch at work, let see if not artistic work!!!
 
PCCB ni vilaza tu. Kazi kubwa ni kukamata rushwa za ngono na matrafic barabarani. Hao former ministers ni maji marefu mno kwao. 2015 hiyo taasisi ifutwe
 
Natumaini hatua zitachukuliwa kweli manake hawa jamaa huwa wanaanza hivyo na mwishowe kimyaaaaaaa kama kesi za kina mzee wa Rombo aka Mramba ramba!!!!
 
hii ilipokuwa inaitwa takuru tulisema haina meno tukaiongeza ku nyingine ili iwe na meno,sasa ili iweze kuwapata na hatia hawa jamaa nashauri iongezewe meno iwe kama simba, iitwe takukukukukukukukukukukukukukukukukukukukukukukukukukukukukukukukuru.

Nimeweka ku 32 ambayo ni meno ya mtu mzima kwa sababu hayo mawili yalishashindwa.
Lolest!
 
Miezi 4 iliyopita Mkulo aliingiza Range Rover Vogue Brand New, O odometer...1 na New Land Cruiser Vx V8 1 kwa pamoja.... Ndani ya nylon hadi kwake Dar.... Iligharimu around Tshs 615 Million according to Kijana wake wa kiume... i saw too.... Mwizi mkubwa huyu Mkulo.
"Mwizi mkubwa" amemuibia nani hayo magari? Kusema "Mkullo ana Vogue tatu na VX mbili nyumbani kwake mikocheni" haiwezi kumfunga mtu.

Tuimarishe vyombo vyetu vya uchunguzi, turekebishe sheria kuziba mianya ya ufujaji, tuwanoe ma akauntanti wetu, tudai ma directors of prosecution ambao wana pursue and prosecute corruption in high places, tuwapeleke shule mapolisi wetu, tuwajengee uwezo hawa maafande, tupigane na rushwa kwenye vyombo vya sheria. Tuchague marais wanaochukia rushwa. Nyerere alisema haitoshi kusema fulani ni msafi, hapendi rushwa. Je, yeye unamjua kwamba binafsi anachukia rushwa popote anapoiona? Anaweza kumshitaki waziri mahakamani?

Mwizi ana ma Vogue, ok, na wale wezi ambao hawana usharobaro wa ku import ma Vogue mtawajua vipi? I mean, Andrew Chenge anatembelea Toyota pick up truck ambalo halina hata insurance na kila Mama Tarimo analo kusombea mashudu, je kuna ofisa wa serikali aliyewahi kui rape nchi hii kinyume na maumbile kama Andrew Chenge in the history of this republic? Anaendesha Vogue?
 
Issue apa kapataje izo dola million 615!
Yaani still kuna watu wanawatete wezi wa mali zetu sitashangaa kuwa mnafaidika na huo wizi
 
Ningependa kufahamu vifungu vya sheria vinavyo criminalize kumiliki Vogue 2 na Land Cruiser mpya. Pamoja na vipengele vya sheria vinavyoongelea kuagiza magari mapywa kwa ndege, vilivyovunjwa. Ahsanteni.

(By the way, Invisible, usifute post zangu, huna sababu ya kuziogopa.)

Hakuna anayemtuhumu MM au Mzee wa megawati kwa kumiliki magari brand new hata kama wameyaingiza nchini kwa ndege.

Tatizo na kinachotakiwa kujulikana, wamepata wapi hizo pesa?

Hata kama wapo wezi wanaotembelea bajaji na kukaa kwenye vibanda vya nyasi.... watatafutwa na sheria itachukua mkondo wake as kwa nini waliiba hata kama waliwekeza bar.

Botttom line mwizi lazima achukuliwe hatua bila kujali kuna mwizi ambae hajakamatwa.
 
TAKUKURU ipi ya Edward Hosea au mwingine? hakuna kitu hapa serikali imeshakuwa corrupt, kama takukuru imeshindwa kwenye suala la rada, kagoda na mengineyo inataka kuchunguza nini?

Siyo kweli kwamba takukuru wamezishindwa hizo kesi hila mfumo ulokuwepo ndo unaifanya isiwe na meno hila tukitaka ifanye hivyo tunavyotaka tutoe maoni katika katiba hili wawe na uwezo wakupeleka kesi mahakamani moja kwa moja hila kwa sasa hv pccb wakishamaliza uchunguzi wanapeleka kwa dpp huko ndo akishalipata analiweka uvunguni na kuna kesi nyingne km za mawaziri lazma apelekewe the president akiridhia ndo inapelekwa mahakamani kwahyo akiamua kukausha asisaini tak
 
Ningependa kufahamu vifungu vya sheria vinavyo criminalize kumiliki Vogue 2 na Land Cruiser mpya. Pamoja na vipengele vya sheria vinavyoongelea kuagiza magari mapywa kwa ndege, vilivyovunjwa. Ahsanteni.

(By the way, Invisible, usifute post zangu, huna sababu ya kuziogopa.)
Mkuu, jamaa hatuhumiwi kwa kumiliki hayo magari, ila tuhuma ipo kwenye upatikanaji wa hayo magari yenye thamani na yeye akiwa mtumishi wa umma. TAKUKURU wanamchunguza jinsi alivyoyapata hayo magari ukilinganisha na kipato chake. Vifungu vitakuja baadae akipatikana na hatia, na moja ya vifungu ni uhujumu uchumi.
 
Back
Top Bottom