AmaniKatoshi
Senior Member
- Mar 31, 2009
- 158
- 14
Mkuu nakupongeza kwa namna ulivyoweza kujengea hoja maswali ya AmaniKatoshiMkuu umeuliza maswali ya msingi sana. Mimi nadhani ni vyema tukiangalia maneno ya Mkulo kwa maana zaidi ya mbili.
1. Imechukua siku 3 kwa kuwa;
a. Hajui kinachoendelea hivyo wasaidizi wake walilazimika kutafuta sababu
b. Walikuwa wamechakachua na ilibidi watunge sababu.
2.Bajeti inaandaliwa na watu wengi ana maanisha;
a.hakuna coordination nzuri ya ku-reconcile data kutoka pande husika (inefficiency)
b.timu ya wachakachuaji ilihusisha watu nje ya wataalam wa wizara, hivyo mahesabu hayakwenda sawa
3. Kwa nini hajiuzulu? Kwa sababu;
a. haoni kosa ni hitlafu ndogo tu iliyotokea.
b. kosa halikusababishwa na yeye bali ile timu ya wachakachuaji walioharibu mahesabu
4. Je bajeti si makadirio?
a. nothing is set in stone, lkn bajeti ni realistic projection
b. hawezi kukubali kuwa ni makadirio kwani itazua maswli mengi.
Kama jibu ya maswali yako yote ni (a) basi Mkulo ni incompetent arrogant unreliable leader.
Kama jibu ni (b) basi Mkulo ni scapegoat na anajua hilo hivyo anatuma ujumbe kwa wahusika - he is not taking this lying down!
Nawasilisha.
Mkulo: Kilichoenda kwa wahisani si bajeti
Mwananchi, Wednesday, 08 December 2010
Raymond Kaminyoge
SIKU tatu baada ya Kundi la nchi wahisani wa maendeleo ambalo zinachangia kwenye bajeti ya Tanzania (GBS) kuibua kashfa kuwa Serikali iliwapelekea bajeti tofauti na iliyopitishwa na Bunge, Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustapha Mkulo, ameibuka na kusema kilichokua kimepekwa kwao ni makadirio.
Alisema bajeti iliyowasilishwa kwa Shirika la Fedha Duniani (IMF) yalikuwa makadirio ambayo yalibadilishwa katika mchakato wa kuiandaa na kwamba bajeti iliyopitishwa na Bunge ndiyo inayotambulika.
Mkulo alisema hayo jana jijini Dar es Salaam mara baada ya kumalizika mkutano wa kitaifa wa mwaka wa majadiliano ya kisera na bajeti.
"Kuna mchakato mrefu wakati wa kuandaa bajeti, tuliwapa makadirio ya bajeti yetu mwezi Aprili mwaka huu, baada ya hapo bajeti ilipitia kwenye Baraza la Mawaziri ambalo lilifanya marekebisho. Katika kipindi hicho kuna marekebisho yalifanywa hivyo kutofautiana na makadirio tuliyowapelekea wahisani," alisema Mkulo na kuongeza:
"Ndiyo maana nasema sijawahi kupeleka kwa wahisani bajeti tofauti na iliyopelekwa bungeni. Nasisitiza kuwa bajeti ni moja tu ambayo ndiyo hiyo niliyowasilisha bungeni baada ya kuidhinishwa na Baraza la Mawaziri," alisema.
Alisema ni utaratibu wa kawaida wahisani kupelekewa makadirio mapema, lakini mambo hubadilika kutokana na gharama eza kuendesha Serikali kubadilika".
"Msidhani Mkulo ndiye anayeandaa bajeti pekee yake, Baraza la Mawaziri ndilo lenye kauli ya mwisho kuhusu bajeti ya nchi, wanaweza kubadilisha chochote wakati wahisani mlishawapelekea bajeti yenu mapema," alisema Mkulo.
Jumatatu wiki hii, Mwenyekiti wa kundi la wahisani wa maendeleo ambalo linachangia kwenye bajeti kuu ya Tanzania (GBS), Svein Baera, katika hotuba yake ambayo Mwananchi ina nakala, alisema serikali ilipeleka IMF, bajeti tofauti na iliyopitishwa na Bunge.
Taarifa hiyo ilitolewa huku wahisani hao wakiwa wamezuia theluthi moja ya zaidi ya dola za Marekani 800 milioni ambazo zinatakiwa zichangiwe na wahisani kwenye Bajeti Kuu ya 2010/11, wakiishinikiza Serikali iharakishe utekelezaji wa programu ya mageuzi, yakiwemo ya mfumo wa usimamizi wa fedha za umma.
Baera alibainisha maeneo sita kuwa ndiyo mhimili wa mjadala wao na serikali.
"Napenda kuainisha maeneo sita ya ujumbe wetu ili kuweka sawa jukwaa la majadiliano yetu haya ya mwaka. Kuna tofauti kati ya bajeti iliyowasilishwa kwa bodi ya (Shirika la Kimataifa la Fedha) IMF na ile iliyopitishwa na Bunge Julai 2010," alisema Baera.
Alisema bajeti ambayo serikali iliwasilisha kwa wahisani hao ilibeba matumaini makubwa ya kuzaa matokeo mazuri na kufanywa kama sababu ya kupitisha matumizi makubwa ya fedha zinazotokana na mapato ya ndani".
Baera alisema kukosekana kwa uwazi katika matumizi, vipaumbele, mapato na mfumo mzima wa fedha kunapunguza kuaminika kwa bajeti hiyo mbele ya wafadhili.
My take:
1. Kwa nini imemchukua Mh Mkulo siku tatu kujibu shutuma wakati jibu alikuwa nalo kwa kuwa alihusika kwenye mchakato wote?
2. Je, kwa nini Mh Mkulo anasema budget inaandaliwa na watu wengi? Ina maana anataka kusema kosa hilo sio la kwake?
3. Kwa kuwa ofisi yake inahusika moja kwa moja kwa nini anatoa majibu ya kujihami badala ya kuchukua uamuzi wa kuijuzulu?
4. Je, Mkulo anataka kutuambia kuwa bajeti sio makadirio?
Hebu tuliangalie hili wana Jf
1. Imechukua siku 3 kwa kuwa;
a. Hajui kinachoendelea hivyo wasaidizi wake walilazimika kutafuta sababu
Kwa nnavyoifahamu Tanzania hii hasa ndiyo sababu kuu. Yaani hawa mawaziri walio wengi ni kupiga siasa tu, hawajui hata kinachoendelea. And guess wht in just this one month napata picha awamu hii ya Kikwete na serikali yake itakuwa kwenye defensive mode mpaka 2015. Hawajajiandaa kufanya lolote. I just can't believe eti JK yule yule tunayemjua will do, act or plan anaything different. Wao kazi yao kubwa ni kushinda uchaguzi tu!!!
Kweli kabisa, kila mara JK anazungumzia juu ya kwa nini CCM imeshindwa katika majimbo kadhaa na eti ufanyike utafiti kujua hilo! Wanachofikiria hawa jamaa ni kubaki madarakani tuu na kufanya ufisadi!