Mkulo anatuongopea?


dah...!!hesabu zako zinaleta mantiki.hizo pesa zingine wanapeleka wapi hawa watu?
 
Hata mimi ningeweza kumsaidia Zitto kwenye hilo. Kuna thread niliwahi kuweka hapa ya kuipongeza benki ya NMB kama miezi 3 iliyopita watu hawakuilewa vizuri. Serikali yetu ina OD facility ikae kimya tu itaumbuka.

Nakumbuka niliisoma na kutoa comment zangu ulieleza visuri sana.Tunaomba wahusika wailete
 
Naombeni namba ya JK nimpigie ili nimwambie aingie JF asome hizi hoja na kuzifanyia kazi dhidi ya MKULO!!
 
Jana kwenye hotuba yake Dodoma JK alidai kuna waziri alimpigia simu akimuuliza eti ananushe habari fulani baada ya Salva Rweyemamu kuitwanga barua hiyo wizara. Mie nadhani huyo waziri atakuwa Mkulo kwahiyo hakumwamini Salva hadi akamuuliza JK, na jana JK akaamua kumuumbua huyo waziri bila kumtaja jina, then baada ya hapo Bw MKULO akaamua kuitisha hiyo Press Conference kukanusha madai ya Zitto. But Zitto yuko sahihi 100%
 

Mkulo anafikiri watanzania hatujui kinachoendelea serikali kwani kazi yake ni kulipa mishahara? Tunamuomba atupe mapato ya nchi kwa mwaka mzima wa fedha, kilichotumika na kilichopatikana ndio tutafahamu nani mkweli nani muongo. Kutupa mapato ya nchi na kiasi gani kimelipwa katika mshahara ni usanii au serikali kazi yake ni kulipa mishahara tu? Pesa za ulinzi, shughuli za maendeleo, posho za wakubwa, matumizi ya ikulu, safari za viongozi, hospitali, akiba ya chakula, na akiba ya baadae .
 

Hivi kwenye hii semina elekezi walielekezwa kufanya nini vile? Ndiyo job description yao mzee kama hukujua basi sasa elewa hilo!
 
Mimi japo si mchumi naomba kuelimishwa kidogo.
Hivi bajeti hupangwa vipi? ama mishahara ya wafanyakazi hupangwa kulingana na fedha tulizo nazo ama tunazotegemea kukusanya. Sijui uchumi lakini naona huu uchumi wa nchi hii ni uchumi kichaa, yani wanakusanya mwezi huohuo ndo wanalipa wafanya kazi mwezi huo huo?
Na je ikitokea walipa kodi waka-jongo kwa siku 20 ina maana na mshahara utachelewa kwa siku 20? Mhhhh kuna tatizo kubwa mno. Hata kama kweli ndo wamekusanya kama anavyoeleza , lakini mie bado naona kuna tatizo la msingi kabisa.

Japo sina data ama uthibitsho wowote lakini naona uchumi wa Tanzania utafika kuzimu hata kama sio leo
 

Mkuu mimi pia unajua nimeshtushwa sana na huu mwenendo! Hata tutumie maneno mazuri vp, lakini we have a problem, big problem.
 
Mkuu mimi pia unajua nimeshtushwa sana na huu mwenendo! Hata tutumie maneno mazuri vp, lakini we have a problem, big problem.

Mkuu,
Tena sana kuna tatizo kubwa mno, yawezekana jamaa kataja namba kisahihi. Lakini hizo namba ukizitia ktk stochastic process hazikubali kabisa.
Na hata hivyo, yani nchi inaendeshwa kama familia kule kijijini yani baada ya mlo unaenda kutafuta kubahatisha mlo mwingine mafuta ya kupikia ktk kibaba. Kuna tatizo la msingi sana nchi haiwezi kwenda kwa staili hiyo
 

Nyambala, kumbuka mwaka jana tu May 3, Mweshimiwa alisema ana "Mbayuwayu" 350,000. Leo May 10 ni mwaka mmoja tu serikali haiwezi tengeneza ajira kwa mbayuwayu wengine (200,000) zaidi ya 50%! Inaonesha pesa nyingi inaishia kwenye ufisadi.
 
Kwa maana hiyo Mheshiwa Mkullo anataka kutuambia kuwa Serikali ya Tanzania ni mchumia tumbo? Makusanyo ni kwa ajili yao tu serikalini? This is very dangerous kwa ustawi wa Tanzania yenye neema!!
 
Mimi kama mfanyakazi wa serikali naidai serikali hela zangu za mshahara. Nilipanda daraja kazini tokea July mwaka jana, hatua iliyoambatana na kupanda kwa mshahara kwa difference ya zaidi ya laki mbili. Hata hivyo hadi sasa bado imekuwa nyimbo kuhusu kulipwa mshahara stahiki, na kupewa malimbikizo yangu (AREAS). Nimejaribu kuuliza mara kadhaa kwa cashier lakini jibu limekuwa serikali bado haina hela za kulipa mshahara mpya. Najua tupo mamia ya watu wenye case kama yangu kwenye taasisi hii ninayofanyia kazi.
Sasa kama Mkullo anasema kuwa serikali haijaishiwa na inalipa mishahara kama kawaida, then watulipe hela zetu. Najua hata huku JF wapo watu wengi wanye case za malimbikizo ya mishahara, posho za likizo, posho za safari na masomo, malipo ya overtime n.k.

Mkullo asitudanganye...
 
na wewe hujui usanii wa Serikali hiii!
 
Mkulo ni muongo tena wa kuogopwa kama KIMETA

Mimi nina miezi sita tangia nimerudi kutoka likizo na bado sijalipwa pesa zangu za likizo kisa serikali HAINA pesa.

Taasisi ninayoifanyia kazi ina miezi mitatu sasa haijapa OC (Other Charges) kisa serikali haina pesa.

Mwezi wa February (kama sikosei) Serikali ilikata OC kwa zaidi ya 25% ya Wizara, Idara na Taasisi za serikali, OC ambayo ilipitishwa na bunge sababu eti ni kubana matumizi kisa serikali haina pesa. Tatizo Mi-bunge ya CCM haiwezi kumuuliza Mkulo alipata wapi mandate ya kukata OCs zilizopitishwa na Bunge.

Kama kweli Mkulo una ubavu tunaomba ukutane na Mh. Zitto kwenye mdahalo aidha TBC1, ITV or Ch10 tujue bivu ni zipi, kwa ulivyo nanga huwezi kuthubutu.
 
mimi naungana na mwenzangu mmoja kuwa baada ya kuwashukia mawaziri kuwa kwanini wamekuwa kimya kuhubiri mazuri na kujibu hoja na za wapinzani matokeo yake wapinzani ndio wanaoteza hivyo kusidisha uamini wa serikali kwa wananchi kupungua mwanzo wake ndio huu mkulo anakurupuka huku anajaribu kuwaaminisha watanzania kuwa wanachoongea wapinzani haina ukweli wakati hapa mimi mwenyewe shahidi kuwa dada yangu kashindwa kumtumia mdogo wangu hela kisa hawajalipwa mishahara sasa mkullo anakutuaminisha upumbavu wake na serikali yao hongera zitto umesema ukweli
 

anasema kwa sababu za kupenda nchi Zitto anatakiwa kukaa kimya kwani tutakosa misaada mingi sana wakijua tumefilisika wakati wao wanatoa pesa. Yaani, eti ndio Waziri anajibu hivyo!!!:A S cry::A S cry::A S cry::A S cry:
 
Topic zingine Bana..hata hujui vipi tuzijadili.... Hadithi za muuza kahawa hizi.
Nimesema toka mwanzo wewe ni mgonjwa, hujui tujadili vipi????????? Watu hawajalipwa mishahara na wabunge hawajalipwa posho,umee elewa jadili sasa!!!!!!! Au wewe pia ni mmoja wao????????
 
Nikisoma thread kama hii huwa najiuliza, waandishi wa habari sio great thinkers kama wana JF? Mbona hoja zinazojadiliwa hapa hawakumuuliza na kisha kutuhabarisha majibu yake?

Mfano: mbona waandishi wa habari hawakumuuliza baada ya kulipa mishahara kilichobaki kwa nini anaita ziada as if serikali haina matumizi mengine?

Nashindwa kuelewa!!!!!?
 
Mkuu soma bajeti 2010/2011 utayajua hayo yote. Kwani serikali iliisha sema itakopa kwa ajili ya pesa za maendeleo (development expenditures) na hilo ndilo wanalo fanya

Unaweza ukasema halafu usitekeleze na hii ndio aina ya serikali ya kj, maneno kibaoooo no vitendo. Semina elekezi, safari, sijui ziara.....wacha nijinyamazie manake hasira tupu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…