Mheshima Rais wa JMT amesema jambo jema kuwa hataingilia bei ya mazao ya wakulima wanyonge na kuwachombeza kuwa sasa ndio wakati wa kuwalangua wale wasiolima. Hofu yangu ni kuwa waliona mahindi sasa ni walanguguzi ambao waliyanunua zamani kwa shs 270/- kwa kilo toka kwa wakulima miezi 4 iliyopita na sasa wanawauzia wakulima walioyalima kwa 900/= kwa kilo.