namna ya kujiendeleza katika biashara/ujasirimali kwa wale walioamua kuwa wafanyabiashara/wajasirimali ni tatu
1:Mtaji
2:Elimu/mbinu za biashara
3:juhudi
nikianza na mtaji hii ndo stata yenyewe, huwezi kufanya biashara bila kuwa na mtaji, lakini mtaji pekee bila kuwa na elimu/mbinu na juhudi ni kazi bure, kama huna Mtaji unaweza kuwekeza nguvu katika kutafuta mbinu za biashara huku ukitafuta mtaji, kamwe haitakiwi kuanza biashara bila ya kuwa na mbinu/elimu hata kama una mtaji tayari.
Elimu/mbinu inahusisha, uelewa wa unataka kufanya nini,je utawezaje kuvutia wateja, je utamudu vipi katika mazingira ya ushindani? hapa panahusisha plans na stratergy mbalimbali za kuendesha biashara yako.hii ni muhimu sana kama ilivyo mtaji, ukishakuwa na mtaji na huu uelewa unaweza kuanza ujasiri mali
3:Juhudi
hii nayo ni muhimu mno ,unajituma kiasi gani,je unafanya kazi masaa mangapi?. je juhudi unazoingiza ni juhudi sahihi? hii itategemea elimu na uelewa
nb:hii ni katika upembuzi wangu wa namna ya kuwa mjasirimali,nadhani wenzangu mna maoni zaidi namna gani ya kufanya hii kitu kufanikiwa?