Mkukuta

Mwanafalsafa

Platinum Member
Jun 24, 2007
657
847
Wana JF,

Kuna huu mradi unaitwa Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kuondoa Umaskini Tanzania (MKUKUTA) ambao sielewi unafanyeje kazi. Ni kweli kuna midocument mingi wamepublish online kuhusu MKUKUTA lakini kwa kweli simple communication imewashinda manaake midocument yao ukiisoma utachanganyikiwa tu na utahisi unapoteza muda.

Kwa mtazamo wangu njia pekee ya kukuza uchumi na kuondoa umaskini ni kutengeneza pesa.

Na kuna njia mbili tu za kutengeneza pesa - uajiriwe (uwe unapata mshahara) au uwe mfanyabiashara (uwe unaingiza mapato kwa vitu unavyouza)

Sasa hawa watu wa MKUKUTA wananisaidia vipi mwananchi kutengeneza pesa?
 
Mwanafalsafa, pia kuna MKURABITA nad mengine mengi tu lakini ufanisi wake kidogo unakuwa mgumu kwangu kuelewa lakini jamaa wana wafanyakazi na wanalipwa mishahara, posho nk.... Twende taratibu na viSACCOS vyetu (hivi ni Ushirika zamani eee??), tutafika ndugu yangu (hata kama ni muda mrefu lakini tutafika tuuuu).... Si mchezo ni kaazi kweli kweli mambo ya Tz!!
 
Ok, hatimaye nimepata mwanga kidogo.

Nimekwenda ofisi ya MKUKUTA nikapata maelezo kuwa MKUKUTA ni "sera" ambayo inatekelezwa na taasisi nyinginezo.

Kwa hiyo kwa ufupi mwananchi wa kawaida hadeal na MKUKUTA moja kwa moja bali kuna taasisi ambazo zinaoperate under MKUKUTA ndio mwananchi anaweza ku-deal nazo.

Chini ya MKUKUTA kuna TASAF na Baraza la Uwezeshwaji (hili baraza liko pale Ofisi ya Wizara ya Uchumi, Mipango na Uwezeshwaji). TASAF inadeal na community project tu, na sio wajasiriamali binafsi.

Baraza la Uwezeshwaji ndio wanaopokea "Mabillioni ya Kikwete" na wamedai wanayapeleka kwenye benki zifuatazo - Akiba Commercial Bank, Azania Bancorp, Dar es Salaam Community Bank, CRDB na NMB kwa hiyo wakanishauri nifuatilie mabilioni ya Kikwete kwenye benki hizo ambako itabidi nifuate masharti ya benki husika.

Phewww!! Bado nina kibarua, ngoja nisikie benki zinasemaje.

Pia kuna tasisi nyingine inaitwa SELF hii iko pale Maarifa House (Ohio Street, Mkabala na Makao Makuu ya ATC). Hawa wanapokea fedha toka Africa Development Bank (ADB). Wao wanadai wanapeleka pesa kwenye SACCOS kwa hiyo kama ninahitaji mtaji toka kwao inabidi nipitie SACCOS. Ila kwa bahati mbaya kwa sasa SACCOS za Dar es Salaam haziruhusiwi katika mpango wao.

Kwa leo nimetoka bila bila, ngoja kesho nipitie kwenye mabenki yanayopokea "Mabillioni ya Kikwete" nisikie wanayagawa kwa utaratibu upi ili kutuwezesha wajasiriamali.
 
namna ya kujiendeleza katika biashara/ujasirimali kwa wale walioamua kuwa wafanyabiashara/wajasirimali ni tatu

1:Mtaji
2:Elimu/mbinu za biashara
3:juhudi

nikianza na mtaji hii ndo stata yenyewe, huwezi kufanya biashara bila kuwa na mtaji, lakini mtaji pekee bila kuwa na elimu/mbinu na juhudi ni kazi bure, kama huna Mtaji unaweza kuwekeza nguvu katika kutafuta mbinu za biashara huku ukitafuta mtaji, kamwe haitakiwi kuanza biashara bila ya kuwa na mbinu/elimu hata kama una mtaji tayari.

Elimu/mbinu inahusisha, uelewa wa unataka kufanya nini,je utawezaje kuvutia wateja, je utamudu vipi katika mazingira ya ushindani? hapa panahusisha plans na stratergy mbalimbali za kuendesha biashara yako.hii ni muhimu sana kama ilivyo mtaji, ukishakuwa na mtaji na huu uelewa unaweza kuanza ujasiri mali

3:Juhudi
hii nayo ni muhimu mno ,unajituma kiasi gani,je unafanya kazi masaa mangapi?. je juhudi unazoingiza ni juhudi sahihi? hii itategemea elimu na uelewa

nb:hii ni katika upembuzi wangu wa namna ya kuwa mjasirimali,nadhani wenzangu mna maoni zaidi namna gani ya kufanya hii kitu kufanikiwa?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom