Mkuki kwa nguruwe na si kwa kikwete

Wewe basi utakuwa ni mtambo. kama umeshindwa kuoanisha heading ya thread na maelezo aliyoyaandika jamaa.na basi utakuwa ushasahau na kiswahili chenyewe .rudi nyumbani hata mara moja cio mnazamia tu huko,cheki hata methali ushazisahau.

Huyu jamaa kweli ugaibuni kumesababisha kusahau kuoanisha maneno na kupata maana ya tungo, sasa anasema hii thread inaeleaelea, jamani mbona kila kitu kipo wazi, kamanda please come home at least once a year, usije sahau kabisa kiswahili, make wewe kwa sasa utakuwa na swahili-english.

Kikwete hajakosea sana make anajua watanzania ni wa kuwasukuma tu hata kama they are still standing, mimi nacholaumu sana ni ubinafsi ambao unataka kuitafuna Tanzania na watanzania wote, wanasema msipige kampeni muda bado lakini look what Kikwete is doing, anapiga kampeni still!!!

kweli kaka mkuki kwa nguruwe---------
 
siwezi nikasema chochote juu kwa bahati mbaya sikuweza kuhudhuria kiao hicho
 
nimeshangazwa na kitendo cha kikwete kuzuia wenyeviti wa kata na wilaya wa ccm wasiwapigie kampeni wabunge katika kikao hicho hicho guninita na makamba wanampigia yeye kampeni za kuwa mgombea pekee , sijui wanasiasa wetu wanajisahau au wanatatizo la ubinafsi


sijui na kikwete anajisahau au anapelekeshwa,

naomba na kikwete azuiwe kufanya kampeni ndani ya chama la sivyo wote waruhusiwe

Hapa umenena kweli kuna baadhi ya mikoa ukiwemo wa Dar wamekuwa wakimpigia kampeni Kikwete wazi wazi tena wakati mwingine mbele yake lakini sijawahi kusikia akikemea

ndani ya CCM hakuna wabunge au viongozi jasiri wanaoweza kusemea wazi jambo hili wanabaki kusema pembeni na kuanzisha makundi yasiyokuwa na sababu lakini ndiyo demokrasi ndani ya CCM ilivyo zidumu fikra za mwenyekiti wengine nyamazeni
 
Hapa umenena kweli kuna baadhi ya mikoa ukiwemo wa Dar wamekuwa wakimpigia kampeni Kikwete wazi wazi tena wakati mwingine mbele yake lakini sijawahi kusikia akikemea

ndani ya CCM hakuna wabunge au viongozi jasiri wanaoweza kusemea wazi jambo hili wanabaki kusema pembeni na kuanzisha makundi yasiyokuwa na sababu lakini ndiyo demokrasi ndani ya CCM ilivyo zidumu fikra za mwenyekiti wengine nyamazeni
Wana njaa, uwepo wao ndani ya Mfumo wa utawala unategemea uwepo wa JK madarakani, unadhani mtu kama Tambwe Hiza , Makamba, Gunninita, Makongoro, Nnchimbi, kukiwa na mwenyekiti wa ccm na rais mpya watakuwemo kwenye mamlaka yao ....thubutu, wanategemea kiongozi legelege kuwafana wao waendelee kukaa kwenye nyazifa hizo.
 
NINJA
Kama rais akizoea kufanya mazoezi ya vitu anavyotaka kusema je siku moja akishtukizwa maswali ya papo kwa hapo nani atamsaidia kujibu, au atajibiwa na wapigadebe wake? au ndio maana ameanza kampeni mapema hili iwe kama mazoezi binafsi ya kampeni zijazo?

Nop. Utaratibu huu upo na ni wa lazima. Rais huambiwa mapema na anafahamu. Hata ukimshtukiza anatakiwa ajue je swali hilo litamsababisha azungumzie mambo yaliyo nje ya mzingo kubalika wa mazungumzo yake kwa mujibu wa taratibu za kazi za wakati huo.

Na moja ya mambo sumu kwa Rais ni kutamka hadharani kuhusu yeye kushinda uchaguzi ambao hata kampeni zake rasmi hazijaanza. Isipokuwa kama chama chake kimetangaza rasmi baada ya kukubaliana kwenye vikao husika kuwa hakitagharimikia uchaguzi wa ndani wa Chama, mgombea wao ni huyo bila kupingwa.

Washauri wake vipi.

Lakini kuna wakati akiwa mahala fulani ziarani niliona timu yake ya kiofisi, wengi wao ni makinda makinda hivi. Sasa hapo lazima awe anajishauri mwenyewe. Wale sana sana watamshauri mambo ya Hip Hop, Yo whatsup, You Know You Know!

Ana kajamaa fulani nilikuwa nakaona na Mwalimu Nyerere Rip enzi hizo, kidogo haka kajamaa kanaonekana kamekula chumvi lakini hakaongeagi maneno mengi, ni mambo ya ulinzi na usalama tu wakati wa matukio labda hakana interest sana na Rais anahutubia nini, sasa vile vicheck bobu vile vingi vingi, sijui ndo vimetoka mbweni juzi au kuna kilichokwenda japo china tu. Ila huku kwangu havijafika, ningeweza ku-assess kama zaidi ya sarakasi na gwaride kuna chochote kingine cha maana wanachoweza ili tuone kama nchi ina wasaidizi wazuri wa kumsaidia bwana mkubwa.

Wazee ni muhimu sana Ikulu. Chonde chonde
 
NGUVUMALI

Jamii inatakiwa ishiriki kwenye siasa na mambo mengine bila vitisho kwani wakiogopa vitisho nani atakuja kuendeleza taifa letu, babu zetu wangeogopa kutafuta uhuru leo tungekuwa wapi? nasi pia hatuna budi kupigania demokrasia ya kweli ili kizazi kijacho kinufaike na uwepo wetu, wenye uwezo wa kuliokoa taifa wasitishwe na kifo, kwani kifo kitaweza kukuteketeza wewe lakini hakina uwezo wa kubomoa misingi mizuri ulioiweka duniani
 
jamani hivi kuna sheria ambayo wanachama wanaweza kumshitaki mwenyekiti wao kwa TENDWA?
 
Kikwete hagombei Chadema hivyo wewe mwana Chadema huna mamlaka ya kuhoji kampeni ya chama kisichokuhusu.Pilipili ipo shamba wewe yakuwashia nini?Au mmezoea udaku!


Tatizo si kwamba wewe ni chama gani na yeye ni chama gani ila asizuie wengine kufanya kampeni wakati yeye anafanya huo ni udikteta ndani ya chama mwenzako unamfunga kamba halafu unasema muanze mbio
 
ndugu mjumbe hiyo ni njia mbadal ya kuonyesha yuko kwennye vita dhidi ya rusdhwa katika ubaguzi..... ni siasa tu hizo, anakula kama panya......
 
Hapa umenena kweli kuna baadhi ya mikoa ukiwemo wa Dar wamekuwa wakimpigia kampeni Kikwete wazi wazi tena wakati mwingine mbele yake lakini sijawahi kusikia akikemea

ndani ya CCM hakuna wabunge au viongozi jasiri wanaoweza kusemea wazi jambo hili wanabaki kusema pembeni na kuanzisha makundi yasiyokuwa na sababu lakini ndiyo demokrasi ndani ya CCM ilivyo zidumu fikra za mwenyekiti wengine nyamazeni
Watapata wapi ujasiri wa kulisemea hilo, wakati wamejaa unafiki na kujipendekeza? Na tabia hii hurudi kuwa gharama kwa umma (wananchi) maana huathiri hata watendaji ndani ya taasisi za serikali.
 
Asante kwa kuliona hilo. Inaonyesha kwamba most people cannot see what is in front of their noses. Wenyeviti wa Mikoa wanakutana na kusema kwamba Kikwete ni mgombea pekee. Labda hata katiba ya CCM inavunjwa kwa kitendo kama hicho.
Sasa Makamba atatangaza sasa hivi kwamba wana CCM wanaruhusiwa kuchukua fomu na kwamba wasikatishwe tamaa na wale waliosema Kikwete ni mgombea pekee,kwamba hiyo,ha ha ha ,haina maana kwamba hakuna demokrasia ndani ya Chama. Lakini inakatisha tamaa.
Marekani kipindi cha Rais ni miaka minne tu. Lakini wanaanza Kampeni za Urais miaka miwili kabla. Hapa hakuna uwazi. Sasa hivi wanataka kufanya hizi closed door mettings na kufukuzana kutoka katika Chama au sijui kufanya nini. Hatuwezi kutoa maoni yoyote. Hatufahamu kama Chama cha CCM kikiparaganyika, kuna viable alternative. Hatufahamua mpaka sasa ufisadi utakuwa ni kikwazo kikubwa kiasi gani kwa CCM katika Uchaguzi wa Oktoba. Hatuna hakika kama tatizo la ufisadi linaweza kusingiziwa matatizo yote ya Nchi hii.
Mafisadi wote wakikamatwa na hela zote zikirudishwa bado matatioz ya Nchi yatakuwepo. HATUJUI ccm au Serikali inawea kufanya nini kuhusu mafissadi wanaoiba hela na kuziweka katika Swiss Bank. Kwa sababu hela ukishaziweka katika Swiss Bank,hata kama umezipata kwa kuuza cocaine,siyo rahisi kwa mtu yoyote kukupokonya.
Kwa hiyo,ina maana kuna System ya kifisadi ya Kimataifa ambayo inaleta corruption Duniani kote.
 
jamani wameshabatilisha kumbe sasa kikwete atakabiliana na wagombea wengine, lakini cha msingi bado hakuna uwezekano wa ushindani wa haki ndani ya ccm kama yeye ataendelea kupigiwa debe na viongozi wa chama cha msingi ni viongozi wa chama waache uchaguzi huru ndani ya vyama vyao,
 
Back
Top Bottom