Mkuki kwa nguruwe na si kwa kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkuki kwa nguruwe na si kwa kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Godwine, Feb 8, 2010.

 1. G

  Godwine JF-Expert Member

  #1
  Feb 8, 2010
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  nimeshangazwa na kitendo cha kikwete kuzuia wenyeviti wa kata na wilaya wa ccm wasiwapigie kampeni wabunge katika kikao hicho hicho guninita na makamba wanampigia yeye kampeni za kuwa mgombea pekee , sijui wanasiasa wetu wanajisahau au wanatatizo la ubinafsi


  sijui na kikwete anajisahau au anapelekeshwa,

  naomba na kikwete azuiwe kufanya kampeni ndani ya chama la sivyo wote waruhusiwe
   
 2. G

  Gangi Longa Senior Member

  #2
  Feb 8, 2010
  Joined: Feb 5, 2010
  Messages: 195
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Kha baba umelonga
   
 3. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #3
  Feb 8, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,891
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  asante kwa kuliona hilo, hakika hatujawahi kumuona JK akiwakemea wanachama wanaofanya mambo yakipuuzi yakumtangaza kuwa mgombea pekee wakati kuna wanaCCM ambao wamejitangaza kugombea Urais 2010, wanawatisha, na kuna kampeni kubwa zinaendelea chini kwa chini juu ya kuzuia haki ya wanaCCM wengine kugombea, hakika mkuki kwa kunguruwe........Awaambie kwa kuwakaripia kina makamba, CHILIGATI waache kutisha wenzao
   
 4. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #4
  Feb 8, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 43,181
  Likes Received: 27,179
  Trophy Points: 280
  Yeye hata asipopiga kampeni si imeshatabiriwa? so hana mpinzani.
   
 5. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #5
  Feb 8, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,891
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Nyaniii utabiri ule wakuwa utakufa ghaflaa....aah jamani.
   
 6. Ninja

  Ninja JF-Expert Member

  #6
  Feb 8, 2010
  Joined: Feb 5, 2010
  Messages: 321
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 80
  Mbona sioni ulipoandika kwamba Kikwete anafanya kampeni . Mbona thread inaeleaelea tutachangia vipi sasa. Halafu facts hazipo kabisa kwenye hii thread au uko under 18; pengine uirekebishe hii thread au uifute kabisa inakuchoresha.
   
 7. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #7
  Feb 8, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 43,181
  Likes Received: 27,179
  Trophy Points: 280
  Aifute kivipi sasa? isome vizuri ndugu usidandie mshale.
   
 8. Ninja

  Ninja JF-Expert Member

  #8
  Feb 8, 2010
  Joined: Feb 5, 2010
  Messages: 321
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 80
  Nyani kwa kuogopa mishale! mwenzio mimi nadaka mishale. lakini bila kuwa na ajenda yako kichwani hii thread inahitaji marekebisho, imejichanganya mno. Anatakiwa aainishe mambo ili ieleweke tunachangia nini na kwa facts zipi.
   
 9. G

  Gangi Longa Senior Member

  #9
  Feb 8, 2010
  Joined: Feb 5, 2010
  Messages: 195
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  kafanya jana kwa kutangaza atashinda ila hajui kwa asilimia ngapi ilhali hajateuliwa bado kuwa mgombea kwa tiketi ya CCM
   
 10. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #10
  Feb 8, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 43,181
  Likes Received: 27,179
  Trophy Points: 280
  Wewe basi utakuwa ni mtambo. kama umeshindwa kuoanisha heading ya thread na maelezo aliyoyaandika jamaa.na basi utakuwa ushasahau na kiswahili chenyewe .rudi nyumbani hata mara moja cio mnazamia tu huko,cheki hata methali ushazisahau.
   
 11. Ninja

  Ninja JF-Expert Member

  #11
  Feb 8, 2010
  Joined: Feb 5, 2010
  Messages: 321
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 80
  Mpaka leo nimeamini hakuna ninja anaweza kukwepa jiwe la Nyani. Unarusha kama hurushi vile.

  Unapoandika thread lazima ujue wengine ni mitambo, sasa nyinyi mnaandikia ma-genius tu. Swali; Hao wanaojipendekeza kupiga kampeni ni kwamba wametumwa na kikwete? kuna facts?

  Bila facts tutarusha mishale tukute kumbe tunapiga Nyani wetu bure. Na tatizo la Nyani ukimkosa hama mji.
   
 12. G

  Godwine JF-Expert Member

  #12
  Feb 8, 2010
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  NINJA
  Kama angekuwa ajawatuma angewakataza kama anavyowakataza wenyeviti wa kata na wilaya lakini wakati makamba na guninita wanatoa hoja hiyo yeye alikuwepo pembeni akiendelea kutabasamu na mwisho wa hotuba ya makamba iliyomtangaza mgombea pekee walikumbatiana kwa furaha
   
 13. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #13
  Feb 8, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kikwete hagombei Chadema hivyo wewe mwana Chadema huna mamlaka ya kuhoji kampeni ya chama kisichokuhusu.Pilipili ipo shamba wewe yakuwashia nini?Au mmezoea udaku!
   
 14. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #14
  Feb 8, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 43,181
  Likes Received: 27,179
  Trophy Points: 280
  Mku Nguli heshima mbele,unaonekana wewe huna jazba.big up!! turudi kwenye thread yetu.
   
 15. Ninja

  Ninja JF-Expert Member

  #15
  Feb 8, 2010
  Joined: Feb 5, 2010
  Messages: 321
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 80
  Unaona sasa, mimi nasoma thread bila kusoma kichwa cha habari yenyewe. Kumbe ishu zinaanzia kichwani! Sasa nimekupata.
   
 16. G

  Godwine JF-Expert Member

  #16
  Feb 8, 2010
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  PENGO

  lengo si kuulizana wewe chama gani, lengo ni kujadili misingi ya siasa za haki na usawa kama mwenyekiti akitokea hawatendei haki wanachama wake hii ni hatari, na itadidimiza demokrasia ya nchi nzima kwani rais akitoka katika chama chochote basi anakuwa ni rais wa tanzania na si wa ccm,
   
 17. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #17
  Feb 8, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,302
  Likes Received: 1,137
  Trophy Points: 280
  Ndiyo maana amekataza[kistaarabu] maana muda wa shughuli hizo haujawadia.
   
 18. N

  Nanu JF-Expert Member

  #18
  Feb 8, 2010
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  UUUUMMHHH. this leaves a lot to be thought about. Preach Water and you drink milk and honey and wine!
   
 19. Ninja

  Ninja JF-Expert Member

  #19
  Feb 8, 2010
  Joined: Feb 5, 2010
  Messages: 321
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 80
  Hii ngoja niitafute sijaipata hiyo. Kama kafanya hivyo inabidi makamu wa Rais amsaidie kazi 'by reasons of being incapacitated'. Tunatarajia asilimia 90% ya anachozungumza kwenye hotuba kiwe kimefanyiwa re-hearsal kabla. Mfano wake ni brainstorming ambayo Rais hufanyiwa kabla ya kwenda ziarani na kuhutubia:

  '' mheshimiwa rais hakikisha hutaji neno fisadi kwenye hotuba yako, usizungumzie kabisa CCJ kwa kuitaja wala kuiashiria, usifanye jambo lolote litakaloashiria kwamba unapiga kampeni, waandishi wa habari utakaokubali maswali yao ni Andrew Mtekete, Bahati Hasanasamza na bi Havinisumbui Omari Mkakati. Picha zao ni hizo hapo, unawafahamu vizuri tu."

  Haya ni mambo ya itifaki na habari Ikulu, sasa haya makosa ya mara kwa mara yaliyozidi ukawaida, tatizo litakuwa ni nini. Isije kuwa kuna tatizo kubwa tunachelewa kulitatua, safari hii kwa mfano atakapoanguka tena kama ilivyo kawaida yake sasa huenda asiinuke tena.

  Kuchanganya mambo( ile thread ya hotuba za Kikwete,kwamba red cross ni serikali) + kuanguka anguka(wengine wana hizi picha kwenye simu zao kama ringtone) + kukosea kuchagua wasaidizi kwa makusudi (Angalia baraza la mawaziri aliloanza nalo na hili la sasa, kabadilisha mara ngapi; alikuwa hawajui?)=Alzheimer disease +incapacitated +co17

  Kama sivyo Ikulu ituambie nini kinaendelea. Hii inatushtua wananchi.
   
 20. G

  Godwine JF-Expert Member

  #20
  Feb 8, 2010
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  NINJA
  Kama rais akizoea kufanya mazoezi ya vitu anavyotaka kusema je siku moja akishtukizwa maswali ya papo kwa hapo nani atamsaidia kujibu, au atajibiwa na wapigadebe wake? au ndio maana ameanza kampeni mapema hili iwe kama mazoezi binafsi ya kampeni zijazo?
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...