Mkosamali: Mrema anajipendeleza alipwe mafao

R.B

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Posts
6,296
Reaction score
2,578
MBUNGE wa Muhambwe, Felix Mkosamali (NCCR-Mageuzi) amemshambulia mbunge wa Vunjo, Augustino Mrema, kwa madai kuwa anajikomba kwa serikali ili apatiwe mafao makubwa ya uzeeni kutokana na wadhifa wake aliokuwa nao serikalini wakati huo.

Mkosamali alitoa kauli hiyo bungeni jana alipokuwa akiuliza swali la nyongeza kwa kuitaka serikali ieleze ni kwa nini inatoa mafao makubwa kwa viongozi wastaafu kama vile mawaziri wastaafu na marais wastaafu wakati wastaafu wa ngazi ya chini pensheni yao ni kidogo.

Mkosamali alitoa mfano huo wa Mrema kutokana na kuwa Naibu Waziri Mkuu, cheo ambacho alikipata wakati wa utawala wa Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, japo cheo hicho hakipo kikatiba.

Wakati Mkosamali akiuliza swali hilo, mwenyekiti wa kikao cha Bunge, Jenister Mhagama, alimtaka mbunge huyo afute kauli yake dhidi ya Mrema kwa madai kuwa si sahihi kumtaja mbunge aliyeko ndani na badala yake ajielekeze katika kuuliza swali analotaka.

Katika swali la msingi, mbunge wa Viti Maalum, Felister Bura (CCM), alitaka kujua kama kuna utaratibu wowote unaoandaliwa na serikali kuhakikisha kuwa ukokotoaji wa hesabu za wastaafu hautofautiani kutoka mifuko ya hifadhi ya jamii.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Fedha, Janeth Mbene, alisema kinachosababisha wastaafu kwa ngazi ya Rais na mawaziri wakuu wastaafu kulipwa mafao makubwa ni kutokana na nafasi zao na kufanya kazi nyingi kwa wakati mmoja.

Alisema wastaafu hao wamekuwa wakifanya kazi katika mazingira hatarishi na nyingi, ikiwa ni pamoja na heshima kubwa waliyonayo katika kulitumikia taifa.

" Hatuwezi wastaafu wote tukawalipa viwango sawa na viongozi wastaafu kwa sababu serikali haina fedha za kutimiza hilo, na pia tunatakiwa kukubaliana kuwa lazima kuna matabaka," alisema.

Naibu waziri alisema serikali imeunda Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) ambayo mbali na jukumu la usimamizi, pia hufanya kazi ya uhuishaji wa uwiano wa ukokotaji wa hesabu za mafao.

Alisema mifuko inayohusika na ukokotoaji wa hesabu za wastaafu ni Mifuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Serikali za Mitaa (LAPF), Mfuko wa Pensheni wa mashirika ya Umma (PPF), Mfuko wa Akiba kwa Watumishi wa Serikali (GEPF) na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).
 
Mimi si mshangai mkosamali kutokana na kabila lake yani ni mtu anayejiona special anamadharau sana na kuongea vitu asivyovijua ilimradi apate sifa.
Ukweli ni kwamba mrema ni mpinzani mkongwe anayejua siasa wala hapalamii treni anajua nn anafanya na matokeo yake ktk uzalendo wa nchi yake.mkosomali ajiulize kazaliwa 1986 unafikiri atajifanananisha na mkongwe wa siasa wa 1945.ndo maana aliwashangaa walipotoka alisema sasa wanakimbilia wapi wakati wametumwa kuja hapa kuwatetea wananchi wao anasema yy hawezi kushikwa sikio na mtu wakati anajua nn kimemleta bungeni
 
safi sana mkosamali huyu mrema hana lolote jwanza hali aliyo nayo ni wa kumsamehe
 
Mimi si mshangai mkosamali kutokana na kabila lake yani ni mtu anayejiona special anamadharau sana na kuongea vitu asivyovijua ilimradi apate sifa.
Ukweli ni kwamba mrema ni mpinzani mkongwe anayejua siasa wala hapalamii treni anajua nn anafanya na matokeo yake ktk uzalendo wa nchi yake.mkosomali ajiulize kazaliwa 1986 unafikiri atajifanananisha na mkongwe wa siasa wa 1945.ndo maana aliwashangaa walipotoka alisema sasa wanakimbilia wapi wakati wametumwa kuja hapa kuwatetea wananchi wao anasema yy hawezi kushikwa sikio na mtu wakati anajua nn kimemleta bungeni

Wewe unalako jambo! Si bure! Hoja za Mkosamali kwa uelewa wako unadhani Mrema anafua dafu?

Alifanikiwa kuvuruga upinzani miaka hiyo ya giza si leo............ akapalilie kahawa kiraracha.
 
Ndugu watanzania wenzangu kwa kijana yeyote aliye kuwa anajitambua kati kati ya miaka 1980 na 1995 atakubaliana nami kuwa mhe, Mrema amelifanyia mambo mengi Taifa hili hususani ktk nafasi yake ya uwaziri wa mambo ya ndani na hata akiwa naibu waziri mkuuu, sasa kitendo cha mkosa mali kumtusi mzee huyu wa makamo kuwa anabembeleza mafao yake kwa kuwaunga mkono CCM kikanifanya nijiulize kuwa hivi mkosa mali hatambui kazi zilizo fanywa na huyu mzee kubwa nikajiuliza hivi hawa wabunge huwa wanalipwa mishahara tofauti hadi wanadharauliana kiwango chakuwafanya viongozi wenzao ni maskini? Kwa umri, heshima na hata umaarufu wa mhe, Dkt Mrema mimi nilikuwa namshauri Mkosamali asijitafutie umaarufu kwa kumtusi mzee Mrema na badala yake amuombe radhi mzee Mrema wakulaumiwa ni CCM ndio walio leta hoja.
 
Acheni ujinga na ushamba bana...kila mtu dr..dr...mnajua watu wanavyosota kupata huo udr....acheni kabisa bana....yule ni bwana mrema....tena mnafki na msaliti...!!!

Wakulaumiwa ni wale walio mpa huo u doctor na sio mleta mada, mimi ninaona kuna hoja yakujadili hapo!
 
Kumbu kumbu zangu zinanionyesha kuwa Mzee Mrema anakumbukwa kwa uhodari wake ktk utumishi wake wa wizara ya mambo ya ndani hakuna aliye mfunika kama naongopa nikosoeni. Mimi naona ni ujinga kumbeza Mrema kwa kudai haki yake, je yule mbunge wa CUF aliyebaki bungeni na Shibuda naye anadai mafao? Uzuri wa CDM hadi hao wakina Mkosamali, Mbatia, Machali huitwa CCM B uunganeni wawatumie kama Condom, mbona Machali na wenzake ndio waliungana na CCM kule uvinza kuunda halmashauri vipi na wao wana mafao wanadai? Mleta mada upo sahihi labda matumizi ya Dkt yanamsumbua huyu ajiitaye Dr. Mo pasipo kujua yeye aliipataje!
 
Udokta sio hoja hapa, kila mtu anajua kuwa udokta wa mrema ni wa heshima ambao viongozi wengi wanao wakiwepo hata vijana
 
Ndugu watanzania wenzangu kwa kijana yeyote aliye kuwa anajitambua kati kati ya miaka 1980 na 1995 atakubaliana nami kuwa mhe, Mrema amelifanyia mambo mengi Taifa hili hususani ktk nafasi yake ya uwaziri wa mambo ya ndani na hata akiwa naibu waziri mkuuu, sasa kitendo cha mkosa mali kumtusi mzee huyu wa makamo kuwa anabembeleza mafao yake kwa kuwaunga mkono CCM kikanifanya nijiulize kuwa hivi mkosa mali hatambui kazi zilizo fanywa na huyu mzee kubwa nikajiuliza hivi hawa wabunge huwa wanalipwa mishahara tofauti hadi wanadharauliana kiwango chakuwafanya viongozi wenzao ni maskini? Kwa umri, heshima na hata umaarufu wa mhe, Dkt Mrema mimi nilikuwa namshauri Mkosamali asijitafutie umaarufu kwa kumtusi mzee Mrema na badala yake amuombe radhi mzee Mrema wakulaumiwa ni CCM ndio walio leta hoja.

Mrema amesha jichokea
 
Acheni ujinga na ushamba bana...kila mtu dr..dr...mnajua watu wanavyosota kupata huo udr....acheni kabisa bana....yule ni bwana mrema....tena mnafki na msaliti...!!!
Mbona na wewe unajiita Dr na wewe ni mjinga?
 
Ndugu watanzania wenzangu kwa kijana yeyote aliye kuwa anajitambua kati kati ya miaka 1980 na 1995 atakubaliana nami kuwa mhe, Mrema amelifanyia mambo mengi Taifa hili hususani ktk nafasi yake ya uwaziri wa mambo ya ndani na hata akiwa naibu waziri mkuuu, sasa kitendo cha mkosa mali kumtusi mzee huyu wa makamo kuwa anabembeleza mafao yake kwa kuwaunga mkono CCM kikanifanya nijiulize kuwa hivi mkosa mali hatambui kazi zilizo fanywa na huyu mzee kubwa nikajiuliza hivi hawa wabunge huwa wanalipwa mishahara tofauti hadi wanadharauliana kiwango chakuwafanya viongozi wenzao ni maskini? Kwa umri, heshima na hata umaarufu wa mhe, Dkt Mrema mimi nilikuwa namshauri Mkosamali asijitafutie umaarufu kwa kumtusi mzee Mrema na badala yake amuombe radhi mzee Mrema wakulaumiwa ni CCM ndio walio leta hoja.
kwa mtazamo wangu mkosamali amemsaidia mrema kudai mafao yake ambayo serikali ni kama imegoma kumlipa. mrema ameadai mpaka amechoka sasa kaamua kujipendekeza kwa serikali lakini pia haijasaidia. jimboni kwake hakuna cha maana anachofanya.
 
hivi ukimchamba bata utakuwa kweli umefanya kazi?ndio mda utapoteza,usafi utaonekana ila reward hautakuwa nayo kwani utaonekana taira!
ndio bata desturi yake kutotunza usafi kwani uchafu desturi yake!

QUOTE=kimeta cha ufisadi;7272119]Ndugu watanzania wenzangu kwa kijana yeyote aliye kuwa anajitambua kati kati ya miaka 1980 na 1995 atakubaliana nami kuwa mhe, Mrema amelifanyia mambo mengi Taifa hili hususani ktk nafasi yake ya uwaziri wa mambo ya ndani na hata akiwa naibu waziri mkuuu, sasa kitendo cha mkosa mali kumtusi mzee huyu wa makamo kuwa anabembeleza mafao yake kwa kuwaunga mkono CCM kikanifanya nijiulize kuwa hivi mkosa mali hatambui kazi zilizo fanywa na huyu mzee kubwa nikajiuliza hivi hawa wabunge huwa wanalipwa mishahara tofauti hadi wanadharauliana kiwango chakuwafanya viongozi wenzao ni maskini? Kwa umri, heshima na hata umaarufu wa mhe, Dkt Mrema mimi nilikuwa namshauri Mkosamali asijitafutie umaarufu kwa kumtusi mzee Mrema na badala yake amuombe radhi mzee Mrema wakulaumiwa ni CCM ndio walio leta hoja.[/QUOTE]
 
Amemsaidia Mrema. Alichofanya mkosamali ni kulisema lile ambalo Mrema mwenyewe asingelisema kamwe ingawa lipo kwenye mawazo na analipractice. Mrema ni kwelli anadia mafao yake na hawezi kusema "Jamani serikali ya CCM nipo chini ya miguu yenu na nipo tayari kufanya lolote hata kuwa mshirika wenu (ndio kujipendekeza kwenyewe) ila tu nipeni changu". Sasa serikali watajua kupitia mkosamali kuwa jamaa anawatumikia inexhange wao inatakiwa wamlipe mafao hata kama cheo cha unaibu Waziri mkuu hakipo kikatiba.
 
Ndugu watanzania wenzangu kwa kijana yeyote aliye kuwa anajitambua kati kati ya miaka 1980 na 1995 atakubaliana nami kuwa mhe, Mrema amelifanyia mambo mengi Taifa hili hususani ktk nafasi yake ya uwaziri wa mambo ya ndani na hata akiwa naibu waziri mkuuu, sasa kitendo cha mkosa mali kumtusi mzee huyu wa makamo kuwa anabembeleza mafao yake kwa kuwaunga mkono CCM kikanifanya nijiulize kuwa hivi mkosa mali hatambui kazi zilizo fanywa na huyu mzee kubwa nikajiuliza hivi hawa wabunge huwa wanalipwa mishahara tofauti hadi wanadharauliana kiwango chakuwafanya viongozi wenzao ni maskini? Kwa umri, heshima na hata umaarufu wa mhe, Dkt Mrema mimi nilikuwa namshauri Mkosamali asijitafutie umaarufu kwa kumtusi mzee Mrema na badala yake amuombe radhi mzee Mrema wakulaumiwa ni CCM ndio walio leta hoja.
Hacha ushekunaku wewe! Amuombe radhi kwa lipi? Yule mzee keshacchoka anajipendekeza kwa CCM mnafiki mkubwa yule. Kenges!
 
kwa mtazamo wangu mkosamali amemsaidia mrema kudai mafao yake ambayo serikali ni kama imegoma kumlipa. mrema ameadai mpaka amechoka sasa kaamua kujipendekeza kwa serikali lakini pia haijasaidia. jimboni kwake hakuna cha maana anachofanya.

MKOSA MALI yeye anafanya nini jimboni kwake!
 
Back
Top Bottom