Mkosamali ashikiliwa na Polisi kwa kufunga kituo cha kuandikisha wapiga kura

Ndugu zanguni, tuhamasishe watanzania kwenda kujiandikisha ktk daftari la kupiga kura kwani ni haki yetu.
Tusipuuzwe na swala la Escrow kwani ni njama ya ccm kuona watz wengi vijana hawajiandikishi ili kukosa sifa ya kupiga kura mwakani.
Nashangaa jinsi hili swala linavokwenda kiusiri kwani halijahamasishwa ipasavyo.
Tuwataarifu na wengine.Mwisho ni tarehe 29 November.
Kama kweli wewe c mnafiki na unaichukia serikali ya kifisadi ya Ccm basi wachukue vijana 10 waliofikia umri wa miaka 18 hadi serikali ya mtaa wako mkajiandikishe ili tuwe na sifa ya kupiga kura.
Tusiwe watu wa kulalamika tu bali kuonyesha tunachukua hata Kwa kujiandikisha
 
Ni Week la Uboreshaji wa daftari la kupiga Kura.

Watanzania wenzangu, tuhamasishane na hasa vijana kwenda kuboresha daftari la kupigia kura kwenye serikali zetu za mitaa.

Zoezi ni la week 1 na linaishia tarehe 29 November.Nasikitishwa na jinsi hili zoezi linavokwenda kwa usiri kwani halijapewa uzito sana na hasa ukizingatia na umuhimu wa zoezi lenyewe kwani watanzania wengi na hasa vijana hawajawahi kupiga kura Kwa kukuwa hawakutimiza umri wa kupigia kura yaani miaka 18.

Tusipuuzwe na mjadala wa Escrow unaoebdelea nchini na kusahau tukio la kihistoria litakalofanyika mwakani Kwa Watanzania kuamua kuirudisha serikali ya wizi,dhuluma, Ufisadi,uuaji,ubaguzi,hila na unafiki ya CCM.

Tusiwe watu wa kulalamika tu bali kuchukua hata.
Kama unachukizwa na hii nchi kwa kushindwa kukupatia mahitaji muhimu ya msingi na lazima kama afya,elimu,miundombinu bora n.k basi wahamasishe vijana zaidi ya 10 kwenda kujiandikisha kupiga kura.
Njia pekee ya kuibadilisha Tz yetu kutoka wizi wa kupindukia ni kupitia kupiga kura kwenye uchaguzi mwakani.

Mataifa mengi duniani yanatushangaa vijana wa Tanzania tulivokuwa wajinga,wazito na waoga wa kufanya maamuzi katika mambo muhimu yanayohusu taifa letu.Lakini utulivu wetu tuwadhihirishe hayo mataifa kuwa sie tumekomaa na tunachoshwa sana na huu ufisadi kwa kujiandikisha kwa wingi katika daftari la kupigia kura na mwakani kupiga
Kura kwa kulikataa taifa la kifisadi na kuanza kuijenga Tz mpya.

Tuwe wazalendo na nchi yetu, ukombozi wa taifa hili la kidhalimu lipo mikononi mwa Watanzania na hasa vijana na sio Kwa wazungu ingawa pia wamesaidia kuturudishia baadhi tu ya sehemu za fedha zilizowahi kuibiwa na huku viongozi tulionao wakichukia .

Ebu tujaribu kuonyesha kuwa tunachukizwa pia.

Tuipende Tz yetu, ni ujinga, kutojitambua na kutojielewa tunapoendelea kupuuza mambo ya msingi yanayotugusa.Ahsante
 
Back
Top Bottom